Uzima Tele
JF-Expert Member
- Jan 20, 2023
- 1,270
- 2,822
==Makala hii kwa njia ya video imeletwa kwenu kwa hisani ya SK Media Online TV na Ansbert Ngurumo==
Jaji Joseph Sinde Warioba (CCM): Wakati wote msimamo wake uko very consistent kuhusu muungano wa Tanganyika & Zanzibar wa mwaka 1964 kuwa suluhu yake ni serikali tatu ya muungano, Tanganyika na Zanzibar.
Walifanya utafiti na asilimia kubwa ya wananchi walitaka hivyo. Utafiti wao unaungwa mkono na tume mbalimbali za CCM ikiwemo ya Jaji Francis Nyalali, Jaji Robert Kissanga na Jaji Mark Bomani. Muungano wa serikali moja hauwezekanigi, wazanzibari hawako na hawajawahi kuwa tayari kuutema utaifa wao na kulifutilia mbali taifa lao la Zanzibar kama sisi Watanganyika tulivyoingizwa mkenge na Hayati Julius K. Nyerere..!
Prof. Palamagamba Kabudi (CCM): Huyu ni kigeugeu. Huyu Prof. Palamagamba Kabudi wa leo si yule aliyekuwa mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba mwaka 2014 chini ya uenyekiti wa Jaji Joseph Sinde Warioba. Ktk video wakati huo anakiri kuwa suluhu ya mgogoro wa muungano wetu ni serikali tatu kama ilivyo kwa Jaji Joseph Warioba . Lakini leo Profesa huyuhuyu kakubali kuuza utu na heshima yake kwa kuwa chawa asiye na msimamo kwa sababu ya njaa ya tumboni mwake na kuikana haki...
Freeman Mbowe: Huyu yeye katika video hii anavunja "taboo" ya kusema yasiyo ya kawaida na mwiko kusemwa ukiwa ndani ya CCM yaani U - zanzibari na u - Tanganyika kwa kigezo cha eti ni ubaguzi. Anapigilia msumari kilichosemwa na Tundu Lissu siku chache zilizopita huko Babati na kwingineko na kuzua taharuki kubwa huko kwenye kambi ya wa - kijani - CCM...
Advocate Tundu Lissu: Kama kawaida yake, yeye huwa hakopeshi, haogopi na hamuenei haya mtu awaye yeyote hata kama ni Rais na udikteta wake. Humwaga kila kitu waziwazi katika ukweli na uhalisia wake. Anarudia kilekile alichokisema akiwa Babati na kuzua taharuki kwenye kambi ya CCM na kuwaibua wana CCM kadhaa hata wale wasio na ushawishi wowote na waliokuwa wamejificha kwa miaka mingi kama vile Ally Hapi, Kinana na wengine wadogo wadogo wasiofahamika sana ktk siasa za Tanganyika...
===========================================
Tazama na sikiliza video hii hadi mwisho.
Na kwa wasio na MB poleni na nawashauri kutokomenti chochote ktk kujenga hoja yako kama hutakuwa umeitazama na kumsikiliza kila msemaji ktk video hii