Kuhusu Muungano, Wazanzibari wametuzidi ujanja

Kuhusu Muungano, Wazanzibari wametuzidi ujanja

Kichuchunge

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2020
Posts
384
Reaction score
970
Nimeitazama kwa makini hii nembo ya Muungano nikagundua kuwa Wazanzibari wametuzidi ujanja sana. Hebu cheki kwenye hiyo nembo, Tanganyika pamoja na ukubwa wake wote na idadi kubwa ya watu lakini amewekwa Mtanganyika mmoja na Wazanzibari watatu why?

437516389_1445566642723043_189597713193336027_n.jpg
 
Nyerere 6 -0 Karume.
Nimeitazama kwa makini hii nembo ya Muungano nikagundua kuwa Wazanzibari wametuzidi ujanja sana. Hebu cheki kwenye hiyo nembo, Tanganyika pamoja na ukubwa wake wote na idadi kubwa ya watu lakini amewekwa Mtanganyika mmoja na Wazanzibari watatu why?
 
Sasa shehe hapo si wameweka Waanzilishi na marais wa sasa hivi ? au

Ulitaka wajae na wakina Nkapa hapo, hiyo nafasi ingetosha na Nkapa alivyo mnene vile
Kwani Nyerere na Karume hawakutosha hadi wawekwe hawa wa sasa?
 
Naunga mkono hoja bora wangeweka na Kofia ya Magufuli kwa pembeni.
 
Sheikh mohamed said yule member maarufu jukwaa la historia akihojiwa na tbc tv anasema wazanzibar ndio wa kupata ardhi bara na si mmbara apate ardhi zanzibar. Anasema mbara haiwezekani kupata ardhi zanzibar kwa sababu ni ndogo. Wazanzibar waje bara kujipatia ardhi ni kubwa
 
Ni mjinga ama anajifanya mjinga Mohamed Said ??
 
Sasa hapa blaza ulitaka nani atoke nani aingie?

Kama ni Samia Suluhu yeye ni rais wa nchi kwa vyovyote huwezi kumuweka pembeni

Kama ni Hussein Mwinyi huwezi mkwepa yeye ndio Rais wa Zanzibar

Karume yeye na Nyerere ndio maana halisi ya Muungano kwa vyovyote lazima wawepo sasa hapo nikuulize wewe swali ulitaka nani atoke na nani aingie?
 
Swala la Muungano ni mipango ya hayati JK1 inawezezekana ikawa ni maagizo kutoka UK, maana kuna mahojiano alifanyiwa Mke wa Mzee Abeid Karume anasema mumewe aliamrishwa atangaze mapinduzi amri ikitoka kwa JK1 nae Karume hakuwa na pingamizi maana alishtukizwa tu,sasa baada ya mapinduzi ndani ya miezi 3 muungano ukazaliwa hii inafikikirisha sana,kwa nini Zanzibar haikupata kujitawala yenyewe!!!
 
Allen...
Hata kama ningependa kuwa mjinga ningeshindwa.

Kipi cha kuwafanya watu kutoka Bara kutaka wapewe ardhi Zanzibar ilhali Bara kuna ardhi ya kutosha?

Hii ndiyo hoja yangu.
Mzee wangu Kwa hiyo wao wanakuja kumiliki upande wa pili Kwa kigezo kipi? Kama inawatosha wao peke yao wabaki nayo lakini na ardhi ya Tanganyika wasiisogelee. Kama Kuna usawa basi wote waruhusiwe kutafuta maisha wapendapo. Pia ardhi kama ni Mtanzania aruhusiwe kumiliki unless mseme Kuna Mtanzania daraja la kwanza na daraja la pili.
Mzanzibar ni daraja la kwanza..anamiliki ardhi Tanganyika na Zanzibar
Mtanganyika ni daraja la pili. Anamiliki ardhi Tanganyika tu, Zanzibar ni off limit kwake. Au?
 
Back
Top Bottom