Kuhusu nani anastahili kiatu mskie Othman Kazi, refa wa Mstaafu wa FIFA

Smart AJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2022
Posts
5,564
Reaction score
5,884
Ukishasoma jijibu tu mwenyewe nani apewe golden boot.

====

EPUKENI U BUSH LAWYER
Msimu wa Ligi Kuu 2022-23 umekamilika rasmi Leo kwa Wananchi Young Africans kutawazwa kuwa Mabingwa. Hongera sana Eng. Hersi, Rais wa Young Africans pamoja na GSM Kwa jitihada ya kuijenga team imara.

Sasa Niwape elimu ndogo tu kuhusu UFUNGAJI BORA NA KANUNI YAKE. Ifuatayo ni Kanuni ya Kombe la Dunia kuhusu UFUNGAJI BORA.

The Golden Boot is primarily decided on total number of goals scored by an individual player at the tournament, but should there be any level-pegging at the summit come the close of play then the award is settled using tiebreaker criteria: first assists, then fewest minutes played.

UFUNGAJI BORA Kimsingi huamuliwa kwa idadi ya jumla ya magoli yaliyofungwa na mchezaji mwenye magoli yanayo wazidi wapinzani wake kwenye shindano husika, ila inapotokea zaidi ya mchezaji mmoja kulingana kwa UFUNGAJI BORA a anayeongoza Mwisho wa shindano husika, basi vipengele vifuatavyo vitatumika kubaini Mfungaji Bora
1. Idadi ya assist
2. Dakika chache zaidi alizocheza.

KANUNI hii ilitungwa tarehe 15 December 2022 a Shirikisho la
Soka Ulimwenguni FIFA kwa ajili ya Mashindano ya kituo kama
Kombe la Dunia.
 
Ukishasoma jijibu tu mwenyewe nani apewe golden boot.

View attachment 2651876
Takataka tupu hizi, magoli kwenye timu zipi?

Mayele alikuwa anakabwa na kukamiwa na mabeki wa timu yoyote sababu ndiye 2022 aliyeipatia Yanga ubingwa, halikadhalika 2023 ni huyo huyo, utaanzaje kumnyima tuzo kwa Saidoo aliyejipigia timu 1 magoli ya michongo tele?

Assits, seriously? Ila Bongo kwa fitina hakuna kinachoshindikana maana si kwa kumkatalia Mayele magoli mengi sana 2022 kuwa ni offsides [emoji1]

Amkeni Mbumbumbu mnatuchosha bure tu Yanga FC [emoji57]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Ushajijibu,inatosha.
 
Hiyo ndiyo kanuni inayotakiwa kutumika. Kama magoli ya penati yanatumika kutafuta bingwa na hayaondolewi ikitokea timu zimelingana pointi, na badala yake wanaangalia sifa nyingine za timu husika, iweje uyatoe kwenye mfungaji bora badala ya kuangalia sifa zingine za hao wafungaji?

Yaani umpe tuzo bora mchezaji ambaye anajirekodi analalamika kwa nini mchezaji mwenzake kamnyima nafasi ya kufunga ili apate tuzo wakati yeye mwenyewe msimu mzimu ana assist 3?
 
Unahangaika kama kuku mtetea
 
Kila mashindano yana kanuni zake mwelewe hilo. Sheria za mpira huamuliwa na FIFA ndo regulater lkn kwenye kanuni inadepend na mashindano yenyewe mfano kanuni za mashindano ya FA (Azam sports) inaweza kuwa tofauti na kanuni za ligi (NBCPL) kwasababu ni mashindano mawili tofauti japo yanasimamiwa na chombo kimoja yaani TFF.
So mpaka sasa tff ndo wenye hizo kanuni ndo wataamua kwa kuzingatia kanuni husika
 
Mayele alikuwa anakabwa na kukamiwa na mabeki wa timu yoyote sababu ndiye 2022 aliyeipatia Yanga ubingwa, halikadhalika 2023 ni huyo huyo, utaanzaje kumnyima tuzo kwa Saidoo aliyejipigia timu 1 magoli ya michongo tele?
Kwa hiyo kigezo cha mfungaji bora ni mchezaji aliyekuwa anakabwa zaidi? 😁
 
Leo Mayele alikuwa akiona mchezaji ameanguka anashika kichwa, Aziz Ki akipoteza mpira anashika kichwa, Bangala anafunga yeye anasikitika, unadhani kwa nini? Hii ni tuzo binafsi ya mchezaji, usijizime data.
KANUNI ndogo za TFF.

Mkilingana Magoli, basi yanaangaliwa magoli ya Penati.

Hakuna la ziada hapo. Kanuni za Mashindano ya FIFA hazifanani na za CAF. Mfano CAF hakuna Goal Difference wao hutumia H2H kwanza kama SPAIN.

USIKARIRI.
 
Mayele ana advantage dhidi ya Saido, kwanini? Mayele kaiwezesha timu yake kuchukua ubingwa, ila Saido hakufanya hivyo, so Mayele ndio anastahili kupewa Golden Boot.

Saido mechi moja ameshinda magoli 5 ya kimchongo, huyo hastahili golden boot
 
Mkeka wa wafungaji bora EPL wa kwanza ni Halaand magoli 36, wa pili ni Harry Kane magoli 30, ........................................................wa saba ni Martin (arsenal) magoli 15 na assist 7, wa nane ni Ollie (Aston Villa) magoli 15 na assist 6, wa tisa ni Gabriel (Arsenal) magoli 15 na assist 5, wa kumi ni Saka (arsenal) magoli 14 na assist 11, wa kumi na moja ni Aleksandar (Fulham) magoli 14 na assist 1, wa kumi na mbili ni Lodrigo (Leeds) magoli 13 na assist 1 michezo 31, wa kumi na tatu ni Harvey (Leicester city) magoli 13, assist 1, michezo 34.

Angalia nafasi ya saba, nane, na tisa wote wana magoli 15, lakini wamezidiana assist. Ila bongo watu hawashindwi kujitoa ufahamu kwa kitu kilicho wazi!!
 
Huyo nae ni kilaza hebu tafuta reference nyingine, Kwenye suala la ufungaji bora hizo assist ni magori?, Sijui dakika chache Sasa kama ulikuwa hupiwi umhimu wa kucheza inahusianaje na ufungaji bora?. Uzuri Kuna reference ya sauti za maafisa wa tff zinaaeleza toka msimu jana ko kamati ya tuzo wamekumbatia bomu lao wenyewe.

Ila saido ni mzee wajamenii apewe tu ndio kwanza jua limeshazama🙄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…