Kuhusu nani anastahili kiatu mskie Othman Kazi, refa wa Mstaafu wa FIFA

Halafu nimekuja kugundua Mayele wamemuhesabia assist kwenye goli la Bangala mechi ya jana na Prisons, ile technically siyo assist, kwa hiyo technically ana assist 3, daah πŸ€£πŸ˜‚πŸ€£
 
Simba ni genge la wahuni kama ilivyo kwa TFF.

Mchezaji mmoja anafunga magoli 7 kwenye mechi 2 mfululizo za mwisho!

Hapa kuna upangaji wa matokeo, wahusika fanyeni kazi zenu
 
Mayele apewe uchezaji bora kwenye magoli ndio hivyo asubiri next season
 
Hivi case kama hii ndiyo ya kwanza kwenye ligi yetu? Iliamriwaje?

Zingekuwepo kanuni ambazo zipo wazi hii isingekuwa topic wala.

Kuanza kuchambua aina ya magoli ni ujuha tu,wangeligana na idadi ya penati?

Siyo rahisi kulingana dakika walizocheza.

Kama kanuni hakuna basi zitungwe kwa ajili ya misimu ijayo na ziangaliwe Assists na Muda.

Kwa sasa watajua cha kufanya.
 
Unabishana na sheria?Wewe ni wa kuzabuliwa makofi.
 
Mayele ana advantage dhidi ya Saido, kwanini? Mayele kaiwezesha timu yake kuchukua ubingwa, ila Saido hakufanya hivyo, so Mayele ndio anastahili kupewa Golden Boot.

Saido mechi moja ameshinda magoli 5 ya kimchongo, huyo hastahili golden boot
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nacheka km mazuriiii, woiiiiiiih
 
Endeleeni tu kubishana. Sisi wengine kwa sasa tunasubiria tu kuangalia mchezo wa fainali hiyo kesho, na hivyo msimu wa ligi kutamatika rasmi.
 
Wamezoea kumdhulumu mayele.....mwaka jana hivyohivyo....
 
MBUMBUMBU hawataki mayele achukue kiatu.
 
Mayele ana advantage dhidi ya Saido, kwanini? Mayele kaiwezesha timu yake kuchukua ubingwa, ila Saido hakufanya hivyo, so Mayele ndio anastahili kupewa Golden Boot.

Saido mechi moja ameshinda magoli 5 ya kimchongo, huyo hastahili golden boot
Sasa kama magoli ya Saido ni ya mchongo, kwa nini TFF haichunguzi upangaji matokeo?
 
Para yako ya mwisho inasema kanuni hiyo ilitungwa na FIFA kwa ajili ya kombe la Dunia. Sio lazima kila mashindano waifuate. TFF wanaweza kuamua vigezo vyao.
 
Usilete hisia bwa mdogo.
 
Huwezi kuwa na ushahidi wa magoli ya kimchongo!! Kuwezesha timu kuwa bingwa siyo kigezo kwenye ufungaji bora popote duniani. Ungekuwa unazungumzia mchezaji bora hapo sawa!! Kubalini Mayele amepigwa knock out round ya mwisho na asubiri msimu ujao!!
Na msimu ujao baleke anamsubiri. Watembeze bahasha tiefuefu apate kiatu bila hivyo atatetemeka sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…