Kuhusu nyongeza ya mshahara

Rashda Zunde

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2022
Posts
204
Reaction score
231
Ni hivi nyongeza ya mshahara kwa 23.3% inaanza kwa watumishi wa Umma wenye kima cha chini 300,000.. so approximately mtu huyo anapokea 70,000 extra!! Hizo asilimia zinakuwa zinapungua kadri mshahara unavyopanda!! The purpose is kulinda gap kwa wafanyakazi lisiwe kubwa.

Hivyo basi hii inamaanisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais SAMIA SULUHU HASSAN imetekeleza ahadi ya kuboresha maslahi ya watumishi wa Umma wenye kipato cha chini kwa maslahi makubwa ya Taifa na jamii kwa ujumla.

 
TGOS C Mshahara 58,000/= 😁😁
 
Hata mjitetee vipi! 2025 mtakalia kaa la moto nawaambia. Maana hakuna namna. Wacha tujaribu na wengine. Nyinyi tumewachoka kwa kweli na hizi bla bla zenu.

Yaani mnamlipa tu mwenye cheti alicho sotea chuo kwa mwaka 1, au 2! Shilingi laki 3! Halafu wakati huo huo Mbunge anayejua tu kusoma na kuandika analipwa milioni 12 kwa mwezi kwa kupiga tu vigelegele, kuruka sarakasi na kugonga meza kule Bungeni! Hapo ni nje ya posho ya zaidi ya laki 2 kwa kila kikao anacho hudhuria!

Kama mnataka kupunguza gap, kwa nini msianzie kwa wale wenye mishahara mikubwa ili mje kuwalipa sasa hao wa laki 3 kwa mwezi?
 
Yaani mnamlipa tu mwenye cheti alicho sotea chuo kwa mwaka 1, au 2! Shilingi laki 3! Halafu wakati huo huo Mbunge anayejua tu kusoma na kuandika analipwa


Unacho shangaa ni kujua kusoma nakuandika tu, au kulipwa vinono?

Kama ni vinono, nawewe pambana uingie mjengoni ,maana hawana mpango wa kupunguza zaidi wanapendekeza waongezewe.
 
Subutu nani wa kusumbua Wazanzibari. Nasikia wao hata mwaka Jana waliongezewa mshahara kwa asilimia mia moja.

Hii ni tatizo la Wadanganyika tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…