Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 229
- 250
Utamu wa ngoma ingia mwenyewe ucheze. Na ukitaka kujua ayafanyayo Dr John P Magufuli wewe ishi Tanzania na ukiwa nje ya Tanzania hakikisha ngoma ya masikio yako iko vizuri na kingine zaid kula mchicha wa kutosha ili mboni ya macho yako iwe na uwezo wa kuyaona ayafanyayo.
Wakati Dr John P Magufuli yuko kwenye kinyanganyiro cha Urais alipotumia kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu wengi tuliona ni kama kibwagizo tulichozoea kama cha Maisha bora kwa kila mtanzania. Wengi tulibeza lakini kwa kipindi cha muda mfupi tumeona tafsiri pana ya Hapa Kazi tu.
Nilitamani nipate nafasi nikutane na wizara ya elimu niwaambie wanasubiri nini kwenye mitaala ya masomo ya Historia na Uraia kuwafundisha wanafunzi juu ya uongozi wa Dr John Magufuli katika nchi yetu ni kwamba umekuwa dira ya viongozi wengine kwa mataifa mengine
Kama kukusifia ni dhambi acha hiyo dhambi initafune. Wakati wa harakati zangu za Kilimwengu niliwahi kusoma kitabu cha gwiji wa fasihi Maalim Shaaban Robert kwenye Kusadikika alisema shujaa ni mtu anayejitolea kwa nguvu zake zote kwa ajili ya kuwakomboa watu wengine.
Hakuishia hapo akasema Shujaa kwa mtu ni ngao kwa nchi ni tunu na kwa taifa ni Hisani. Yale maneno yaliyoandikwa na Shaaban Robert Mlimwengu mimi nayashuhudia kupitia kwa Dr John Magufuli. Wewe ni shujaa kwetu kwangu mimi wewe ni ngao ninajivunia popote kule kuwa nina baba imara.
Leo hii upande wa pili waliozoea kupinga kila kitu watapinga nini? Waliposema ufisadi ikawa ajenda yako kubwa kuwaondoa, waliposema uzembe maofisini leo hii kila ofisi ni heshima, wakasema uongozi mbaya ila leo hii kila mteule wako ana nidhamu ya juu katika utendaji. Wakasema viongozi wanasafiri ovyo ovyo ila sasahivi tunaenda kukamilisha mwaka wa tano umetemebelea nchi mbili nazo ni majirani ila wao ndio wanakufuata wewe.
Mlimwengu mimi nitazidi kusema na wala sitasita kusema kazi uzifanyazo. Waliposema Miundombinu mibovu leo hii shangazi yangu wa Mbeya anafanya biashara zake Chunya to Tabora kwa uharaka zaidi. Umerahisisha mawasiliano leo hii rafiki yangu niliyesoma naye Bwiru Boys yupo Kazira mimba anasoma ujumbe huu kwa uharaka kutokana na miundombinu bora ya mawasiliano.
Sasa hivi wale watoto wa miaka 4 wanaochezea makopo wanakuambia Magufuli ni baba lao mimi mlimwengu nipinge kama nani kuwa wewe siyo baba lao wakati tunaamini watoto ni malaika.
Suala la Corona sitaki nizungumzie sana maana Trump anaposikia hotuba yako anamuambia mkalimani umefanya kitu gani na umetoa dira gani.
Mambo uliyoyafanya hatuwezi kuyamaliza yote ndio maana kila mtu anaamua kusema yale ayawezayo kuyasema.
Tulipokuwa tunaambiwa Rais ni Amri jeshi mkuu wengi hatukuelewa ila kupitia utawala wako na uongozi wako nimejifunza maana ya Urais. Naomba niombe msamaha kwa ajili ya walimwengu wote tunaomba utusamehe kwa makosa ya watanzania wenzetu ambao wameamua kuwa makuadi wa mataifa ya nje. Wewe ndio kioo chetu na tunakutegemea katika kuifanya Tanzania iwe ya asali na maziwa.
Wako
MO Mlimwengu
Email: [email protected]
29/05/ 2020