Kuhusu Rais wetu na wenzake kupanda basi kwenye msiba wa Malkia Elizabeth II

Kuhusu Rais wetu na wenzake kupanda basi kwenye msiba wa Malkia Elizabeth II

Chura

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2009
Posts
1,385
Reaction score
2,402
Wanajamvi habarini? Nisiwachoshe sana ngoje nitoe madini kidogo kuhusu itifaki ilitomika kuwabeba vichwa vya dola (Head of states ) huko kwenye msiba wa bi Elizabeth na kuwa ngumzo huko mitandaoni.

Tuanze kwanza kwa kuangalia kitu kinaitwa "order of Seniority and precedence" hii maana yake kwenye itifaki kila mtu anakuwa treated kutokana na ukubwa wake jinsi unavyokua senior ndo unavyozidi kupendelewa kuliko yule less senior ama junior.

Mfano kukiwa na hafla senior ataingia wa mwisho less ataingia wa mwanzo (hapa ni kuhakikisha kuwa senior anapata mda wa kujiandaa zaidi pia hatakiwi kumsubiri mtu yani yeye akishafika tu hafla inaanza ndo sababu hata kwenye maadhimisho mfano wa kilele cha mwenge Rais Samia alivyoingia tu pale Chato stadium milango ikafungwa na shuhuli ikaanza).

Hata ikitokea hatari senior atakua wa Kwanza kuwa evacuated afu kina junior watafuata, mfano mwingine ni kwenye kutoka senior ataanza(Yes senior hatakiwi kuchoka hovyo😂) afu kina junior watafuata nk.

Sasa kuna wakati inatokea hafla moja inakua na watu wenye hadhi sawa unafanyaje kumpata senior ili awe treated kwa maraha zaidi tofauti na wengine? Hapo sasa inakuja issue inaitwa PRECEDENCE kwanza host wa shuhuli husika mwenye title sawa na wageni anakuwa senior over waalikwa, alafu wengine wataangaliwa kwa mda waliotumia kuassume ofisi zao.

Mf Tanzania Rais samia akiandaa sherehe tuseme labda birthday party yake afu akawaalika Marais wa E.Africa samia atakua senior akifuatiwa na Mseveni afu Kagame ......Ruto atakua junior kwa wote.

Aim ya protocol duniani kote ndugu wana jamvi ni kuhakikisha shuhuli inaenda kama ilivyokusudiwa, pili kuhakikisha wahusika wana enjoy shuhuli

Mazishi ya malkia tena wa uingereza kama tulivyoona yana tuvitu vitu twingi kwa kuhofia kutumia muda mwingi kupokea delegates via their presidential convoys wakaamua kuwabeba kwa pamoja hiki ni kitu cha kwaida kabisa kwenye protocol.

Yes hapa itifaki ilifanikiwa kwa angle moja maana hata huku kwetu Mf Siku ya Uhuru top layers wanaingia uwanjani kwa convoys zao ila waliobakia ie mawaziri, wabunge mabalozi hawa wanaingia kwa collective transportation(pool) lengo ikiwa kuokoa mda.

Ila hiyo hiyo itifaki imefeli kwa angle ya pili ku avoid "Embarrassment" fedheha wale ni marais angalau wangewatreat wote sawa bila kujali hadhi ya taifa husika isingeleta tabu maana itifaki inaprivilege kutokana na title na sio taifa unalotekea ndo maana unaona kwenye UNGA pale UN, TZ pamoja na umasikini wake Rais wake anakua adressed kwa EXELLENCY title sawa sawa na Biden au Macron.

Ila ile ya kwamba wengine wanaingia kwa misafara yao binafsi kwa kigezo cha Usalama wakati wengine wanakusanywa kama nyanya ilihali wote wana hadhi ya URAIS, hapana maana yake umedevalue hadhi ya Urais wa wengine hivyo kusababisha fedheha, kwanza imewafanya wajihisi inferior na kuwapunguzia kujiamini.

Basic treatment za privileges kwenye protocol zinatoka kwenye order of Seniority and presidence, provided wote Macron+Biden wana hadhi ya marais sawa na ukilinganisha na ya wale wa Africa akiwemo Mama mwenye Kaya yetu, kuwatenga ni kuleta fedheha kwao.

kwa kumalizia duniani huko Seniority ipo hivi Senior kabisa duniani ni PAPA》Wafalme/Sultan》Marais

Ni hayo tu wenU CHURA MAVITUVITU
 
kwani marais wa afrika ni watu wa aina gani Ulaya?

kila siku nasema huwezi kuwa ana akili kwenye wajinga
 
Biden anatua na the beast, ambulance, jammer na gari zingine kadhaa afu umuweke kwenye yutong 😀

Nani Kati ya hao kaenda na usafiri wake wa chini kama Biden?
 
Naskia bwana ruto kachafua hali ya hewa ile mbaya kwenye basi
Sema bi maza akalipa nauli ya mabraza wake wote from EAC hana baya anapiga mwingi mpaka bukingamu
 
Back
Top Bottom