mbona kama lilipita?Friday, June 7, 2013
haki at Friday, June 07, 2013
Mwenyekiti wa Makampuni ya
IPP, Dk. Reginald Mengi
Awakabidhi Zawadi Washindi Wa
Shindano la 'TWITI" Wazo Jipya
La Kuondoa Umaskini
Mshindi wa tatu akipokea kitita
cha sh. laki 3.
Mshindi wa pili, Peter George
akipokea kitita cha sh. laki 5
Mwenyekiti wa Makampuni ya
IPP, Dk. Reginald Mengi
akimkabidhi kitita cha sh. milioni
1 mshindi wa kwanza wa
shindano la Twiti Wazo Jipya
Kuondoa Umaskini, Jilly Gaudence
Kyomo katika hafla iliyofanyika
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Institute
Of Management and
Enterprenuership, Dk. Donath
Olomi. Kulia ni mshindi wa pili,
Peter George na mwanafunzi wa
chuo cha CBE, Ludovick Angelino.
Mwenyekiti wa Makampuni ya
IPP, Dk. Reginald Mengi
akifafanua jambo wakati wa
hafla ya utoaji zawadi kwa
washindi shindano la Twiti Wazo
Jipya Kuondoa Umaskini jijini Dar
es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Institute
Of Management and
Enterprenuership, Dk. Donath
Olomi akizungumza wakati wa
hafla hiyo.
---
Na Mwandishi Wetu
VIJANA watatu wa jijini Dar es
Salaam, wameibuka washindi
katika shindano la Dk. Reginald
Mengi la Kutwit kuondoa
umasikini nchini.
Mshindi wa kwanza katika
shindano hilo lililopewa jina la
Twiti Wazo Jipya Kuondoa
Umasikini ni Jilly
. ambaye
aliibuka na kitita cha sh milioni
moja, Peter George (sh 500,000)
na Ludovick Angelino (300,000).
Akizungumza katika hafla ya
kukabidhi zawadi kwa washindi
iliyofanyika katika Ofisi za Makao
Makuu ya IPP, Dk. Mengi alisema
shindano hilo lina lengo la
kuibua mawazo mapya jinsi ya
kupambana na umasikini.
Alisema washiriki wa shindano
hilo lililozinduliwa Mei 13 na
washiriki wengi walijitokeza
kuibua mawazo mapya na
washiriki watatu ndio
walioshinda.
Dk. Mengi ambaye ni Mwenyekiti
Mtendaji wa Kampuni za IPP,
alisema mchakato wa kupata
washindi, ulisimamiwa na
Kiongozi wa Taasisi ya Chuo cha
Uongozi na Ujasiliamali (IMED),
Donath Olomi na jopo lake.
Akizungumza jinsi washindi hao
walivyopatikana, Dk. Olomi
alisema jumla ya Twits 481
zimepokelewa kati ya Mei 13
hadi 31.
Alisema vigezo vilivyotumika
katika mchakato huo ni wazo
lililoeleweka na kuelezeka
kirahisi, lisiwe wazo ambalo
limeshasikika mara nyingi na
liwe linaweza kutekelezeka.
Alisema mshindi wa kwanza Jilly
alitoa wazo lililosema Tuwe na
utamaduni wa kupenda kile
tukifanyacho, tukifanya kwa
moyo, uadilif, heshima na kujali
muda hata kama its self
employed.