Uchaguzi 2020 Kuhusu suala la kuichagua CCM na sio Upinzani Dkt. Magufuli yupo sahihi

Uchaguzi 2020 Kuhusu suala la kuichagua CCM na sio Upinzani Dkt. Magufuli yupo sahihi

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
510
Reaction score
839
Kampeni zinazidi kushika kasi ambapo kila chama kinachanja mbuga kusaka kura kwa kila namna. Gumzo kubwa lililojili leo ni kauli ya Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwaasa Wananchi kuichagua CCM kinyume na hapo watapata tabu.

"Mkijidanganya hapa mkachagua wa chama kingine, majuto yake mtayaona, wala siwadanganyi, siwafichi." - Dkt. John Pombe Magufuli

Naweka wazi kauli aliyoitoa Dkt. Magufuli ni sahihi kabisa, twende sawa hapa. Miaka ya 1970's Tanzania ya Nyerere ya TANU na ASP na China ya Mao ya Chama Cha Kikomunisti ilikuwa katika hali sawa ya kiuchumi kutokana na nchi zote kuamini na kusimamia mfumo wa chama kimoja cha kisiasa kushika hatamu ndio maana utawala wa awamu ya kwanza wa Mwalimu Nyerere ulikuwa na mafanikio makubwa sana, shida ilianza tulipoanza kuingiza mifumo ya vyama vingi ambayo ni sera ya ukoloni mambo leo wenye lengo la kutugawa ili waweze kututawala.

Mahali ambapo Wananchi wamechagua Wapinzani pamekuwa na ucheleweshaji wa kimaendeleo. Mathalani tumekuwa na Wabunge wa upinzani ambao asilimia kubwa kazi yao ni kususia vikao na hata kwenye Halmashauri napo pia ni vurugu tupu za kupinga kila kitu.

Tumekuwa na viongozi wa upinzani ambao ajenda yao kuu ni kupinga kila kitu hata bajeti za kuwaletea maendeleo wamekuwa wapingaji. Waliochagua Wapinzani wanayajua majuto haya.

Chama tawala na Chama pinzani kamwe hawawezi kukaa meza moja kujenga Taifa kwa sababu mmoja yupo kimaendeleo, mwingine yupo kupinga maendeleo akiamini ni sehemu ya kumnyima ama kumpunguzia umaarufu wa kisiasa mwenzie.

Vyama vingi vya upinzani bado ni vichanga, havijajiimalisha na kutwa ni kugombana wao kwa wao wakigombea madaraka. Unaweza kuta Mwenyekiti haelewani na Katibu wake, kisa wana makundi ya kimaslahi ya kimadaraka. Muda wa kuwatumikia Wananchi hawana zaidi ya kulumbana wenyewe kwa wenyewe. Waliochagua Wapinzani wanayajua majuto haya.

Kauli ya Dkt. Magufuli si ya vitisho wala ya kibabe bali imejaa upendo wa dhati kwa Watanzania akiwa na lengo la kuwaasa Wananchi kuchagua Watu atakaoweza kuongea nao lugha moja na endapo atakosea yeye kama kiongozi wa chama na Serikali pia ataweza kumwadhibu aliyekosea.

Narudia tena kusema kauli ya Dkt. Magufuli ni sahihi kabisa. Ni afadhali ukosee kuoa au kuolewa kwani unaweza kumuacha mwenzio kuliko kukosea kuchagua kiongozi, majuto yake ni miaka mitano.

Shilatu, E.J
 
JPM na serikali ya awamu ya tano wamefanya mambo mengi hadi mengine yana sahaulika. Madawati ni moja ya kero ambazo zilipatiwa mwarobani wake. Mh Rais tukumbushe na hili ili zile kura kiduchu za upinzani zilizo bakia huko, wasizipate kabisa. Mwanza wametisha ama kwa hakika, kwa jinsi walivyoonesha mahaba yao kwa JPM na CCM.

Huu ni mfano bora kwa wengine, Rais JPM amefanya mambo mengi kwa taifa hili katika kipindi hiki cha miaka5. Hebu Watanzania na tuioneshe dunia nzima kwa hakika ya kuwa umma wa Watanzania uko nyuma yake. Tarehe 28/10/2020 kishindo cha matokea ya kura za uchaguzi kwa Rais na CCM mwangwi wake ukasikike mpaka katika miisho ya dunia hii. Dunia ikajue na kuelewa ukoloni mamboleo hauna nafasi Tanzania.
 
Siwezi kumchagua mtu mbaguzi kama huyu.

IMG-20200906-WA0023.jpg
 
Ingekuwa unafanyika uchaguzi wa Mbunge tu maneno hayo yangeweza kueleweka. Huu ni uchaguzi mkuu ukijumuisha rais na madiwani. Mgombea wa urais yeyote asijipe uhakika wa moja kwa moja kushinda.
 
JPM na serikali ya awamu ya tano wamefanya mambo mengi hadi mengine yana sahaulika. Madawati ni moja ya kero ambazo zilipatiwa mwarobani wake. Mh Rais tukumbushe na hili ili zile kura kiduchu za upinzani zilizo bakia huko, wasizipate kabisa. Mwanza wametisha ama kwa hakika, kwa jinsi walivyoonesha mahaba yao kwa JPM na CCM...

Hiyo tarehe 28 Oct hakuna uchaguzi, bali ni kilele cha maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Pumba kabisa hivi kongwa kuna wapinzani? Nchemba je? Tabora vipi kuna maendeleo?
 
Mlishawahi kuwapa nchi wapinzani wakaharibu au ndo zile kauli za kusema ETI MKIMKOSA RAIS JOHN SIDHANI KAMA TUTAPATA MWENYE MOYO KIZALENDO KAMA,HUYU"
Ni nini wamefanya kinachoweza kutufanya tuwaamini na kuwapa nchi, au unataka tuwape kwa majaribio? We can do better than being a 'kichwa cha mwendawazimu'.
 
Ni nini wamefanya kinachoweza kutufanya tuwaamini na kuwapa nchi, au unataka tuwape kwa majaribio? We can do better than being a 'kichwa cha mwendawazimu'.
Mnataka wapinzani wafanye kipi kama mwenyekiti wenu anaonesha wazi kutenga majimbo yaliokaliwa na upinzani kimaendeleo as if maendeleo yanafanywa na hela zake za mifukoni?
 
Mnataka wapinzani wafanye kipi kama mwenyekiti wenu anaonesha wazi kutenga majimbo yaliokaliwa na upinzani kimaendeleo as if maendeleo yanafanywa na hela zake za mifukoni?
Toa mfano ambako wamenyimwa miradi ya maendeleo kwa sababu ya kuchagua upinzani
 
Siku chache zilizopita namba two katoa kauli tate na sasa tena rais anatoa kauli tete zaidi . Kuna nini ccm?
 
Back
Top Bottom