Sauti ya Mwakalabela
Baada ya Mwamba Haji Manara kuunguruma leo Wasafi Fm, majibu yameanza kutoka. Niwashauri viongozi wa Yanga waache kujidhalilisha wanaposhindana na Haji. Nasema hivyo kwa sababu chanzo cha haya yote ni baada ya Haji kumtakia Happy Birthday Papy Shishimbi,wao wakaumia sana. Lakini hakuna sehemu yeyote ambayo uongozi wa Simba ikiwepo Haji waliotamka kumsajiri Shishimbi,zaidi ya mashabiki pekee
"Nichukue nafasi hii kuwaomba msamaha Simba Sports Club na wanachama wa Yanga SC kuhusu kauli yangu juu ya kutaka kumsajili Claotous Chama, nilikuwa nafanya utani kama wao walivyokuwa wanafanya kwa Tshishimbi ila kiukweli mchezaji huyo sijazungumza nae. Nilizidisha utani na naahidi jambo hili halitojitokeza tena."
Fredrick Mwakalebela