Kuhusu TUHUMA za uzushi za Kitenge naomba wana SIMBA kwa umoja wetu tuamue kifuatacho

Kuhusu TUHUMA za uzushi za Kitenge naomba wana SIMBA kwa umoja wetu tuamue kifuatacho

Airmanula

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
3,527
Reaction score
5,762
Imekua ni kasumba kwa huyu mtangazaji anajiita Kitenge ambaye anafanya kazi Radio ya Wasafi, kuja na tuhuma mbalimbali kuhusu SIMBA na zaidi tunajua anatumiwa na watu wasioitakia mema SIMBA sababu wanaumia na MAFANIKIO ya SIMBA na wengine roho zinawauma kupita kiasi wakiona SIMBA anafanya vizuri.

Naomba kwa UMOJA wetu, tuache kusikiliza WASAFI FM na zaidi kuangalia WASAFI TV hadi pale atakapofukuzwa kabisa. Wapo waandishi wa habari za michezo wenye WELEDI, hawana kazi au hawapo kwenye media house kubwa nchini, wapewe nafasi. Najua kuna wana SIMBA ni wapenzi wakubwa wa WASAFI lakini kwa hili naomba tuwe WAMOJA. Tupambane na hawa MAMLUKI na wanaotumwa kuja kutuchafua.
 
Sasa wasafi watajuaje kama hamskilizi radio yao na wala hamuangalii television Yao, kikubwa aonywe Tu
 
🤣🤣😂
20210307_084408.jpg
 
Huyo Kitenge anapoteza muda, apuuzwe, sasa hivi Simba inatangazwa kwa matokeo yake uwanjani, hizo kelele za Kitenge hakuna anayejielewa atapoteza muda wake kumsikiliza, zaidi anaonekana chizi mwenye wivu tu.
 
Imekua ni kasumba kwa huyu mtangazaji anajiita Kitenge ambaye anafanya kazi Radio ya Wasafi, kuja na tuhuma mbalimbali kuhusu SIMBA, na zaidi tunajua anatumiwa na watu wasioitakia mema SIMBA sababu wanaumia na MAFANIKIO ya SIMBA, na wengine roho zinawauma kupita kiasi wakiona SIMBA anafanya vizuri...
Haha hahah hahah hoja ya kitoto sana hiyo
 
Susa...! susa...! susa nasema suusa...! Isome kwa sauti ya Haji!
 
Maulid Kitenge anajua nguvu ya uchawi wa maneno. Anatumia vizuri nafasi aliyo nayo kutengeneza maneno ya fitna dhidi ya Simba. Hii ni kwa vile timu yake imeshindwa kupambana ndani ya uwanja.

Hana namna zaidi ya kuleta fitna na kuzipandikiza kwa wana Simba ili ikitokea mitafaruku, apate sababu ya kuchekelea kwa vile anajua mtafaruku wowote utaigharimu Simba.

Dawa ya mtu kama huyu ni kumpuuza tu. Ila pale wasafi sio mahali pake. Hafai kuendelea na kazi huyu jamaa kwani hana weledi.
 
Maulid Kitenge anajua nguvu ya uchawi wa maneno.Anatumia vizuri nafasi aliyo nayo kutengeneza maneno ya fitna dhidi ya Simba.Hii ni kwa vile timu yake imeshindwa kupambana ndani ya uwanja...
Huu uzushi ni upi? Nimeona thread nyingi lakini mpaka sasa sijabahatika kukutana na huo uzushi

Mkuu hebu tuwekee
 
Acha roho mbaya mkuu
Kumbuka anao watu nyuma yake wanamtegemea

Hoja ya kipuuzi Sana hii, kabla huja mjudge mtu jitazame kwanza wewe Kama upo Bora Sana kuliko mwenzako....

Mind ur business mkuu
Hao watu nyuma yake wanamfanya nini? Kumbe ni kweli!
 
Huu uzushi ni upi? Nimeona thread nyingi lakini mpaka sasa sijabahatika kukutana na huo uzushi

Mkuu hebu tuwekee
Mashabiki wa simba wanadeka sana. Halafu wanapenda muda wote timu yao kusifiwa tu hata katika mambo ya hovyo hovyo.

Mbaya zaidi kwenye miaka ya karibuni, wamejigeuza kuwa misukule ya Haji Manara! Akisema Manara chochote, basi wote huitikia "hewalaaa" Huyo Manara akitukana, na wenyewe wanatukana!

Hata sishangai Rage alipo waita mbumbumbu! Na natambua fika mtakuja. Hivyo nawasubiri kwa hamu. Mbumbumbu wakubwa nyinyi! aka 😾😾 mapaka fc.
 
Watanzania hawapendi kabisa kukosolewa au kukosoa, ila wao wapo kutwa mitandaoni kukosa na kuwakosoa wenzao...wakikosolewa wao utaskia huo ni uzushi, uchonganishi, tumsusie, tumsomee albadil na mengineyo mengiiii...hivi nyie mnavyowafanyia wenzenu huko mitandaoni nani hua anawasusia au kuwasomea albadili.

Now naanza kupata picha kua ht wanasiasa wasiopenda kukosolewa au kusemwa its our self reflection, na ht tukibadilisha uongozi 100 times still watu hawata taka kusemwa maana hii kitu ipo kwenye damu ya watz.
 
Uzi tayari dah kuna mbwa ni vivu kuandika
 
Imekua ni kasumba kwa huyu mtangazaji anajiita Kitenge ambaye anafanya kazi Radio ya Wasafi, kuja na tuhuma mbalimbali kuhusu SIMBA na zaidi tunajua anatumiwa na watu wasioitakia mema SIMBA sababu wanaumia na MAFANIKIO ya SIMBA na wengine roho zinawauma kupita kiasi wakiona SIMBA anafanya vizuri.

Naomba kwa UMOJA wetu, tuache kusikiliza WASAFI FM na zaidi kuangalia WASAFI TV hadi pale atakapofukuzwa kabisa. Wapo waandishi wa habari za michezo wenye WELEDI, hawana kazi au hawapo kwenye media house kubwa nchini, wapewe nafasi. Najua kuna wana SIMBA ni wapenzi wakubwa wa WASAFI lakini kwa hili naomba tuwe WAMOJA. Tupambane na hawa MAMLUKI na wanaotumwa kuja kutuchafua.
Kaka usitake wote kutufananisha na akili za Manara..kwani kitenge kakosea wapi?kama ni owongo kinachotakiwa ni kukanusha na sio kuanza kubwabwaja na kuongelea mambo yasiyo ma miguu wala mikono. Kwanza nani kamtuma Manara kumjibu Kitenge? Pengine Manara hajui nini kinachoendelea ndani ya uongozi kuhusu huo mgogoro . Ni wakati sasa Simba kumuonya manara kuwa anatakiwa kuzungumza alichotumwa na Club na si vinginevyo..
 
Back
Top Bottom