Kuhusu ujamaa nasema hapana

Kuhusu ujamaa nasema hapana

CCM MKAMBARANI

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2017
Posts
2,031
Reaction score
1,514
Kwa jinsi nimechukia sina haja ya kutoa salamu, moja kwa moja katika mada.
Ni kuhusu mkutano wa leo mjini Dodoma kati ya wana CCM wakongwe wakijaribu kutuvisha vijana koti la ujamaa kwa nguvu. Ni kuwa suala hili haliwezekani tena, huyu mzee anaeshupalia ujamaa inapaswa atuambie kwa namna gani serikali inaweza kutupeleka mbali kupitia ujamaa wa akina Mzee Nyerere na wenzie.

Babu Butiku anajenga Hoja ya kutupotosha na kutufanya vijana kuwa hatujui hasara za ujamaa. Labda mzee atuambe kuwa anataka ujamaa wa kizazi kipya lakini si ule wa mzee Nyerere. Kwa hakika uchumi hauendeshwi na serikali badala yake huendeshwa na watu binafsi huku serikali ikiwa na macho makali kwa ajili ya kuweka sawa mizani flaniflani ya kiuchumi.

Katika nadharia za kijamii yaani sayansi ya jamii ni kuwa Taifa hili haliwezi tena kuwa na ujamaa, hii inatokana na mambo mengi mosi, mfumo wa elimu haujaandaa watu haswa wanafunzi kuja kuwa wajamaa, pili, dunia ya leo imejaa vitu ambavyo kwa hakika kila mtu angetamani apate.

Hebu nikuulize Mzee Butiku, Mtoto wako Peter yuko wapi na anafanya nini? Je ni Mjamaa wa maneno au porojo? Je umewahi kupunguza zile billion 19 zako ambazo umehifadhi benki kwa kusaidia watz wenzio? Mbona unakuwa mnafiki mzee, kwanini lakini?.

Mwisho; Mzee Butiku usidanganye vijana,unachotakiwa kufanya ni kusema tufanye kazi na kuhamasisha serikali iweke mazingira safi, usiturudishe katika wimbi la umasikini, mzee Butiku unadanganya. Huu ni msimamo wangu na si Uvccm.
Ahsanteni.
 
Sio tu hatuna eleimu ya ujamaa, bali hata waliokuwa na hiyo elimu ya ujamaa walifeli vibaya sana.
ikiwa walioanzisha ideology ya ujamaa walifeli, sisi tunaotaka kukopy tena ideology hiyo ndo tutafaulu kweli!!.

Tulifeli, tena wanataka kuturudisha katika felia hiyo!.

Ujamaa ni mfumo wa unyonyaji kuliko ubepari..
 
Failed state kila siku matamko

Hata china nayenyewe haipo kwenye ujamaa ivi sasa.

Ila uzuri hii ikianzishwa vijana tujiandaye kugawiwa wale ngombe wa mzee baba. Na ile hotel yake ya chato inakua mali ya umma
 
KILA SIKU POLEPOLE ANAONGEA KUWA TANZANIA SIO YA KIJAMAA .....BALI WATU WAKE NI WAJAMAA.......ELEWA HILO ....THATS Y TANZANIA MTU UKIPATA AJALI .....WATU NDIO HUWA WA KWANZA KUKUSAIDIA ........BUT UKIENDA LETSAY USA ...UKIPATA AJALI HAKUNA ANAEKUJALI. ....BALI ITAPIGWA TU SIMU HOSPITALI
 
Ccm uruhusiwi kufikiri kinyume na fikra za mwenyekiti.Wwe ni nani unapinga ujamaa
 
KILA SIKU POLEPOLE ANAONGEA KUWA TANZANIA SIO YA KIJAMAA .....BALI WATU WAKE NI WAJAMAA.......ELEWA HILO ....THATS Y TANZANIA MTU UKIPATA AJALI .....WATU NDIO HUWA WA KWANZA KUKUSAIDIA ........BUT UKIENDA LETSAY USA ...UKIPATA AJALI HAKUNA ANAEKUJALI. ....BALI ITAPIGWA TU SIMU HOSPITALI
Ukipata ajali hapa Tanzania, watu wa kuanza kufika eneo la ajali watakuibia kila kitu. Haijarishi watu hao ni vijana, wazee, wanaume, wanawake, mapadri, masheikh, askari polisi nk.
Hili ni taifa la vibaka.
Haya ndio matunda ya miaka 44 ya CCM.
 
Awamu hii ili uwe Mzalendo wa kweli basi uwe maskini(ujamaa).
𝐍𝐢 𝐯𝐢𝐥𝐞 𝐭𝐮 𝐭𝐮𝐧𝐚𝐤𝐚𝐫𝐢𝐫𝐢𝐬𝐡𝐰𝐚 𝐮𝐛𝐚𝐲𝐚 𝐰𝐚 𝐔𝐣𝐚𝐦𝐚𝐚 𝐝𝐡𝐢𝐝𝐢 𝐲𝐚 𝐮𝐳𝐮𝐫𝐢 𝐰𝐚 𝐮𝐛𝐞𝐩𝐚𝐫𝐢, 𝐭𝐮𝐦𝐞𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐰𝐚𝐭𝐮 𝐰𝐚 𝐤𝐮𝐮𝐜𝐡𝐮𝐤𝐢𝐚 𝐮𝐣𝐚𝐦𝐚𝐚!

𝐋𝐚𝐤𝐢𝐧𝐢 𝐦𝐢𝐬𝐢𝐧𝐠𝐢 𝐲𝐚 𝐮𝐣𝐚𝐦𝐚𝐚 𝐧𝐢 𝐦𝐢𝐬𝐢𝐧𝐠𝐢 𝐢𝐧𝐚𝐲𝐨𝐣𝐞𝐧𝐠𝐚 𝐮𝐭𝐮, 𝐮𝐬𝐚𝐰𝐚 𝐧𝐚 𝐡𝐚𝐤𝐢 𝐤𝐰𝐚 𝐤𝐢𝐥𝐚 𝐦𝐰𝐚𝐧𝐚𝐝𝐚𝐦𝐮!

𝐋𝐚𝐤𝐢𝐧𝐢 𝐧𝐚𝐦𝐧𝐚 𝐭𝐮𝐧𝐚𝐯𝐲𝐨𝐮𝐳𝐮𝐧𝐠𝐮𝐦𝐳𝐢𝐚 𝐥𝐞𝐨 𝐭𝐮𝐧𝐚𝐮𝐨𝐧𝐚 𝐤𝐚𝐦𝐚 𝐧𝐢 𝐦𝐛𝐚𝐲𝐚 𝐤𝐮𝐥𝐢𝐤𝐨 𝐮𝐛𝐚𝐲𝐚 𝐰𝐞𝐧𝐲𝐞𝐰𝐞.

𝐖𝐚𝐭𝐮 𝐡𝐚𝐬𝐚 𝐯𝐢𝐨𝐧𝐠𝐨𝐳𝐢 𝐧𝐚 𝐰𝐚𝐭𝐨𝐚 𝐦𝐚𝐚𝐦𝐮𝐳𝐢 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐧𝐠𝐚𝐳𝐢 𝐲𝐚 𝐊𝐢𝐦𝐚𝐭𝐚𝐢𝐟𝐚 𝐧𝐚 𝐤𝐢𝐧𝐜𝐡𝐢 𝐡𝐮𝐭𝐮𝐦𝐢𝐚 𝐮𝐝𝐡𝐚𝐢𝐟𝐮 𝐰𝐚 𝐔𝐣𝐚𝐦𝐚𝐚 𝐤𝐮𝐰𝐚𝐧𝐲𝐨𝐧𝐲𝐚 𝐰𝐚𝐥𝐢𝐨 𝐰𝐞𝐧𝐠𝐢 𝐤𝐰𝐚 𝐦𝐢𝐬𝐢𝐧𝐠𝐢 𝐲𝐚 𝐮𝐛𝐨𝐫𝐚 𝐰𝐚 𝐔𝐛𝐞𝐩𝐚𝐫𝐢.

𝐘𝐚𝐦𝐤𝐢𝐧𝐢 𝐥𝐞𝐨, 𝐔𝐣𝐚𝐦𝐚𝐚 𝐮𝐧𝐠𝐞𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐮𝐦𝐞𝐬𝐭𝐚𝐰𝐢 𝐤𝐮𝐟𝐢𝐤𝐢𝐚 𝐧𝐠𝐚𝐳𝐢 𝐚𝐦𝐛𝐚𝐲𝐨 𝐔𝐛𝐞𝐩𝐚𝐫𝐢 𝐦𝐚𝐞𝐧𝐝𝐞𝐥𝐞𝐨 𝐮𝐦𝐞𝐟𝐢𝐤𝐢𝐚 𝐥𝐞𝐨, 𝐃𝐮𝐧𝐢𝐚 𝐢𝐧𝐠𝐞𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐦𝐚𝐡𝐚𝐥𝐢 𝐬𝐚𝐥𝐚𝐦𝐚 𝐧𝐚 𝐩𝐚𝐤𝐮𝐟𝐮𝐫𝐚𝐡𝐢𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐤𝐢𝐥𝐚 𝐤𝐢𝐮𝐦𝐛𝐞!
 
WANAJIFANYA WAJAMAA WAKATI WANAISHI KIBEPARI...

ova
𝐇𝐚𝐩𝐚 𝐧𝐝𝐢𝐩𝐨 𝐭𝐚𝐭𝐢𝐳𝐨 𝐥𝐢𝐧𝐚𝐩𝐨𝐚𝐧𝐳𝐢𝐚.

𝐊𝐚𝐦𝐚 𝐰𝐚𝐧𝐠𝐞𝐚𝐦𝐮𝐚 𝐤𝐮𝐮𝐬𝐡𝐢 𝐮𝐣𝐚𝐦𝐚𝐚 "𝐬𝐨𝐜𝐢𝐚𝐥𝐢𝐬𝐦-𝐢𝐦𝐩𝐞𝐫𝐢𝐚𝐥𝐢𝐬𝐦" 𝐥𝐚𝐛𝐝𝐚 𝐥𝐞𝐨 𝐝𝐮𝐧𝐢𝐚 𝐢𝐬𝐢𝐧𝐠𝐞𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐮𝐰𝐚𝐧𝐣𝐚 𝐰𝐚 𝐯𝐮𝐫𝐮𝐠𝐮 𝐧𝐚 𝐭𝐚𝐦𝐚𝐚 𝐳𝐚 𝐤𝐢𝐦𝐚𝐟𝐢𝐬 𝐥𝐚𝐦𝐚 𝐢𝐯𝐲𝐨 𝐥𝐞𝐨!
 
KILA SIKU POLEPOLE ANAONGEA KUWA TANZANIA SIO YA KIJAMAA .....BALI WATU WAKE NI WAJAMAA.......ELEWA HILO ....THATS Y TANZANIA MTU UKIPATA AJALI .....WATU NDIO HUWA WA KWANZA KUKUSAIDIA ........BUT UKIENDA LETSAY USA ...UKIPATA AJALI HAKUNA ANAEKUJALI. ....BALI ITAPIGWA TU SIMU HOSPITALI
𝐔𝐬𝐢𝐩𝐞𝐧𝐝𝐞 𝐤𝐮𝐨𝐧𝐠𝐞𝐚 𝐮𝐬𝐢𝐲𝐨𝐲𝐚𝐣𝐮𝐚.

𝐔𝐥𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐟𝐢𝐤𝐚 𝐔𝐬 𝐮𝐤𝐚𝐬𝐡𝐮𝐡𝐮𝐝𝐢𝐚 𝐡𝐚𝐲𝐚 𝐮𝐬𝐞𝐦𝐚𝐲𝐨?

𝐍𝐢 𝐤𝐰𝐚 𝐭𝐚𝐚𝐫𝐢𝐟𝐚 𝐲𝐚𝐤𝐨 𝐭𝐮, 𝐡𝐚𝐨 𝐦𝐚𝐛𝐞𝐩𝐚𝐫𝐢 𝐰𝐚𝐧𝐚 𝐮𝐭𝐮 𝐰𝐚 𝐤𝐢𝐮𝐭𝐮 𝐤𝐮𝐥𝐢𝐤𝐨 𝐡𝐚𝐨 𝐰𝐚𝐣𝐚𝐦𝐚𝐚 𝐢𝐜𝐡𝐰𝐚𝐫𝐚 𝐰𝐚 𝐡𝐚𝐩𝐨 𝐮𝐥𝐢𝐩𝐨!
 
Ukipata ajali hapa Tanzania, watu wa kuanza kufika eneo la ajali watakuibia kila kitu. Haijarishi watu hao ni vijana, wazee, wanaume, wanawake, mapadri, masheikh, askari polisi nk.
Hili ni taifa la vibaka.
Haya ndio matunda ya miaka 44 ya CCM.
........ACHA HASIRA MKUU ....LABDA HUKO DAR ..NDO WANAFANYA HIVO ......EBU FIKIRIA ....CHADEMA WANGEONGOZA NCHI......TANZANIA TUNGEIZIDI CONGO, SUDAN SOMALIA ....KWA CIVIL WAR.....PROUD FOR CCM GOVERNMENT
 
𝐔𝐬𝐢𝐩𝐞𝐧𝐝𝐞 𝐤𝐮𝐨𝐧𝐠𝐞𝐚 𝐮𝐬𝐢𝐲𝐨𝐲𝐚𝐣𝐮𝐚.

𝐔𝐥𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐟𝐢𝐤𝐚 𝐔𝐬 𝐮𝐤𝐚𝐬𝐡𝐮𝐡𝐮𝐝𝐢𝐚 𝐡𝐚𝐲𝐚 𝐮𝐬𝐞𝐦𝐚𝐲𝐨?

𝐍𝐢 𝐤𝐰𝐚 𝐭𝐚𝐚𝐫𝐢𝐟𝐚 𝐲𝐚𝐤𝐨 𝐭𝐮, 𝐡𝐚𝐨 𝐦𝐚𝐛𝐞𝐩𝐚𝐫𝐢 𝐰𝐚𝐧𝐚 𝐮𝐭𝐮 𝐰𝐚 𝐤𝐢𝐮𝐭𝐮 𝐤𝐮𝐥𝐢𝐤𝐨 𝐡𝐚𝐨 𝐰𝐚𝐣𝐚𝐦𝐚𝐚 𝐢𝐜𝐡𝐰𝐚𝐫𝐚 𝐰𝐚 𝐡𝐚𝐩𝐨 𝐮𝐥𝐢𝐩𝐨!
.......mkuu kumbe hujui maana ya ubepari .....wale majamaa hawanaga time ya kudeal na ishi za mtu mwingine wenyew huwa wana consider time and money tu....... Nyie huko kwenu. MNAOMBANA CHUMVI, MOTO, PESA .......SIJUI ELIMU BURE .....WAZUNGU WANATUSHANGAA SANA
 
........ACHA HASIRA MKUU ....LABDA HUKO DAR ..NDO WANAFANYA HIVO ......EBU FIKIRIA ....CHADEMA WANGEONGOZA NCHI......TANZANIA TUNGEIZIDI CONGO, SUDAN SOMALIA ....KWA CIVIL WAR.....PROUD FOR CCM GOVERNMENT
Nyinyi ndio watu ambao mnachelewesha maendeleo ya nchi hii.. Kuwa na fikra potofu na za kitoto..

Tena na ww unaweza kukuta una watoto na unatoa ushauri kbsa...

Toa facts kwa hyo maneno yako, usilete maneno ya kijiwen
 
.......mkuu kumbe hujui maana ya ubepari .....wale majamaa hawanaga time ya kudeal na ishi za mtu mwingine wenyew huwa wana consider time and money tu....... Nyie huko kwenu. MNAOMBANA CHUMVI, MOTO, PESA .......SIJUI ELIMU BURE .....WAZUNGU WANATUSHANGAA SANA
𝐌𝐤𝐮𝐮 𝐮𝐧𝐚𝐨𝐧𝐠𝐞𝐥𝐞𝐚 𝐮𝐛𝐞𝐩𝐚𝐫𝐢/𝐮𝐣𝐚𝐦𝐚𝐚 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐥𝐞𝐯𝐞𝐥 𝐢𝐩𝐢?

𝐔𝐬𝐢𝐜𝐡𝐚𝐧𝐠𝐚𝐧𝐲𝐞 𝐂𝐮𝐥𝐭𝐮𝐫𝐚𝐥/𝐬𝐨𝐜𝐢𝐚𝐥 𝐩𝐫𝐚𝐜𝐭𝐢𝐜𝐞𝐬 𝐧𝐚 𝐈𝐝𝐞𝐨𝐥𝐨𝐠𝐲
 
Nyinyi ndio watu ambao mnachelewesha maendeleo ya nchi hii.. Kuwa na fikra potofu na za kitoto..

Tena na ww unaweza kukuta una watoto na unatoa ushauri kbsa...

Toa facts kwa hyo maneno yako, usilete maneno ya kijiwen
......FACT NI KUWA VYAMA VYA UPINZAN TANZANIA BADO HAVIKO STABLE KUONGOZA NCHI HII .....KWANZA WENYEW TU HAWAELEWAN REFER WABUNGE 19 WA CHADEMA .......PILI WANAPONDA HATA VITU VYA MANUFAA KWA NCHI.....TATU ..WANATUMIKA NA MABEBERU .....
 
𝐌𝐤𝐮𝐮 𝐮𝐧𝐚𝐨𝐧𝐠𝐞𝐥𝐞𝐚 𝐮𝐛𝐞𝐩𝐚𝐫𝐢/𝐮𝐣𝐚𝐦𝐚𝐚 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐥𝐞𝐯𝐞𝐥 𝐢𝐩𝐢?

𝐔𝐬𝐢𝐜𝐡𝐚𝐧𝐠𝐚𝐧𝐲𝐞 𝐂𝐮𝐥𝐭𝐮𝐫𝐚𝐥/𝐬𝐨𝐜𝐢𝐚𝐥 𝐩𝐫𝐚𝐜𝐭𝐢𝐜𝐞𝐬 𝐧𝐚 𝐈𝐝𝐞𝐨𝐥𝐨𝐠𝐲
. Tukisha sema mfumo wa kibepari ....tuna maanisha ...vyote vilivyomo ....social practices , ideology na vngne vinavyo relate na capitalism/ubepar
 
Ukipata ajali hapa Tanzania, watu wa kuanza kufika eneo la ajali watakuibia kila kitu. Haijarishi watu hao ni vijana, wazee, wanaume, wanawake, mapadri, masheikh, askari polisi nk.
Hili ni taifa la vibaka.
Haya ndio matunda ya miaka 44 ya CCM.
Hahahahahaha #taifaaaa la vibakaaa hahaha
 
Back
Top Bottom