Kuhusu Uzalendo na Hekima, Tundu Lissu hana wa kumlinganisha. Ni Mzalendo kweli kweli, ni Magufuli ndani ya Sura ya Lissu

Kuhusu Uzalendo na Hekima, Tundu Lissu hana wa kumlinganisha. Ni Mzalendo kweli kweli, ni Magufuli ndani ya Sura ya Lissu

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
24,831
Reaction score
45,154
Ktk hali ya kawaida, kwa wanasiasa wenye tamaa ya madaraka na uroho wa kutumia vibaya rasilimali za Wananchi sio rahisi mwanasiasa kusema bora tuache kwanza uchaguzi aliyepo aendelee ili apate muda wa kufanya maboresho tupate mifumo mizuri yenye Tija kwa Taifa.

Si jambo rahisi kwa mwanasiasa kuacha kwenda kwenye uchaguzi hata kama ni za kiini macho na akakubali kukosa fedha za Ruzuku.

Si jambo jepesi hata kidogo kuacha pride ya kugombea ubunge, udiwani na Urais ukatanguliza maslahi ya Taifa kwanza. Si jambo rahisi ndugu zangu

Wale walaghai wa kisiasa wao wanasema Twende hivyo hivyo, kwa sababu wao hawajali maslahi ya Taifa. Ni Buti Mbele kaza twende tukale maziwa na asali hata kama Kuna Utumwa.

Wasio wazalendo wanaona ni bora tuchaguane kimagumashi hivyo hivyo lakini tunywe mchuzi.

Wenye macho tunajua chaguzi za Tz hazina malengo wala maslahi kwa Wananchi wa hali ya chini.

Huu Ni Mwaka wa Kumjua Mzalendo kwa Vitendo na sio Bla bla za majukwaani.

We need New Tanzania, New Beginning.

Bonne Journée. À biontôt.
 
Kwa tunaojua historia ya hii nchi, Tundu Lissu ndo the smartest politician we have ever had so far. Kwa mbali anayeweza kuwa anamkaribia tena kwa mbali sana ni Oscar Kambona
Okay, kwa sisi tusiojua historia tunamjua Lissu na Magufuli tu
 
Back
Top Bottom