Kuhusu Wabunge 19 wa Viti Maalum wakiongozwa na Halima Mdee: Mambo yako wazi ila wahusika wako kimya

Mkuu mbona kabla ya mwenda zake kwenda hukuwa unayazungumza haya?
 
Hizo hela kwa namna yoyote ile inatakiwa watu 19 wa jinsi ya kike wazipata, vinginevyo zitakaa pasipo stahili! waache hao wa-mama/dada wazifanyie matumizi kwa kadri watakavyoona inafaa!!
 
Asante sana Wakili Msomi Petro.
 
Mkuu CCM nimakafiri na kutenda dhambi ni jadi yao
 
 
😂😂😂😂
 
H
hitimisho lako linaukakasi.umeanza vzr lkn umemaliza vibaya.kwa nn huwashauri CDM wamwandike barua spika kuwa wabunge hao wamevuliwa uanachama.je spika anafanya kazi kwa kufuata vyombo vya habari au documents?acheni ushabiki humu kila mtu ana utashi wa kujua nn kinachoendelea.CDM wanajua kila kitu kuhusu sakata hili na wameamua kukaa kinywa.mwambieni Mbowe amwandikie barua spika tuone kama hajareact na kama unaamini kuwa kuna barua ameandikiwa spika hebu iwazi hapa janvini.
 
Mkuu, unaposoma mada za watu wenye upeo na wasomi usiwe unakurupuka. Hebu nisome tena kwa utulivu. Kwenye hilo unalolisema nimeuliza maswali na si kwamba nimehitimisha kwa hivi au vile. Kunywa maji halafu nisome tena...usiniweke kwenye kundi la mashabiki wa vyama...
 
HILI SUALA NI KWENDA MAHAKAMANI TU SIJUI KUNAKIGUGUMIZI GANI KWENDA MAHAKAMANI ILI MAHAKAMA SASA ITASFIRI SHERIA YA WAO KUWEPO BUNGENI AU KUTOKUWEPO BUNGENI NA WANAOGOPA NINI KWENDA MAHAKAMANI? KUN TATIZO CHADEMA KAMA HAKUNA SHIDA WANGEENDA MAHAKAMANI TU SUALA LIKAISHA
 
Chadema nao wana kosa katika hili, wanashindwaje kuitisha kikao cha baraza kuu ili kuamua hatima ya hao wasaliti wao?

Sasa wakifungua kesi mahakamani itasaidia nini wakati itaonekana wao wenyewe hawajafuata katiba yao?
 
Mkuu barua imeandikwa na Mnyika alishaitisha press kuelezea hilo na imepelekwa mara mbili.....

Funny enough mtu akilitukana bunge kupitia media huwa anaitwa na spika kupitia kamati ya bunge ya maadili ila wakitumia media kutangaza maazimio ya kikao mnadai bunge halifanyi kazi kupitia media

Hii nchi unafiki hauwezi kutusaidia, sophia simba alifukuzwa kwenye press ya Polepole hata nusu saa haikupita kiti kikatangaza Sophia Simba hana sifa ya kuwa mbunge!!

Kama Ndugai anaona kina Mnyika wanapotosha kuwa wamefukuza bila kuleta barua si awaite kwenye kamati ya maadili kwa kudhalilisha hadhi ya bunge??

Weird
 
Hao ni wabunge wasiyokuwa na chama
Bungeni,only in tiziii

Ova
 
kuwa mimi si mwanachama wala mshabiki wa chama chochote cha kisiasa hapa nchini au nje ya nchi hii.

Hivi hata hapo haukuwa na chama?
 
Mkuu Wakili Msomi Petro E. Mselewa , hapo ambapo hautaki kupazungumzia, ndipo mimi ninapoanzia. Vyama vya siasa Tanzania, sio mali ya viongozi, sio mali ya wanachama, ni public parties, ni mali ya umma, vinaendeshwa kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, haiwezekani, viongozi waitane na kukaa kama a kangaroo court na kujiamulia kuwatimua tuu wanachama wake kama wanavyojisikia!. No Way. Lazima wafuate katiba, sheria, taratibu na kanuni. Katiba ya Chadema iko wazi, ni an open document ambayo iko kwa mujibu wa sheria na taratibu za nidhamu ziko wazi kabisa, lakini siku zote, Chadema inawatimua wanachama wake kienyeji enyeji tuu, bila kufuata taratibu. Hivyo huko kufukuzwa kwa wanachama hao ni batili!. Hii sio mara ya kwanza kwa Chadema kufanya madudu haya, wewe ni wakili msomi unajua maana ya ubatili, Halima Mdee ni mwanasheria msomi anazijua haki zake.

Chadema ilipofanya uhuni huo kwa kina Shonza, akina sisi tukalipigia kelele humu, Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili Kuwatendea Haki Watanzania 2015!

Chadema ikaja kurudia madudu haya kwa Zitto, Kitila na Mwigamba, hawa jamaa wawili dhaifu wakakubali yaisha, Zitto akawagomea, mimi kama kawaida yangu, niliwashauri Chadema Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau, Jiandaeni kwa "Karma!"

Hivi hii timua timua Chadema imeizoea!. Mmezoea vya kunyonga hamviwezi vya kuchinja. Hongera sana Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji

Kwenye hili la wabunge 19 wa Chadema, CC ya Chadema, did the same same mistakes, Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu

Ikakaa as usual as a Kangaroo court, kama kilivyokuwa kinakaa huko nyuma na kutoa hukumu za ajabu ajabu ikiwemo timua timua, ambazo karma za hukumu hizo, zinakuja kuigharimu Chadema mbele ya safari, tatizo, wakati wa karma payback time unapofika, when karma strikes back, hakuna anayekumbuka kuwa ni hukumu ya matendo yake ya nyuma!. Tatizo la karma, unaweza kufanya kitu kidogo, tuu, kwako ukakiona ni kidogo, it's nothing and insignificant, lakini when karma takes its toll, mapigo ya karma yanayokushukia ni mapigo makubwa in three folds, kulinganisha na ulichotenda, hadi huwezi kukumbuka ulifanya nini kustahili, kinachokupata. Ila pia, anayehukumiwa pasipo haki, karma pia huwa ina mtake care, na kumu elevate machoni pa watesi wake!.

Mifano ya Matendo ya Chadema, na Matokeo ya Karma Zake.
  1. Chadema walipo establish a torture chamber pale makao makuu yake na kumshughulikia ipasavyo Mlinzi wa Dr. Slaa, Kagenzi, nilionya kuhusu karma. Kwa vile hii ilikuwa ni internal operation, na mimi sio inside man wa Chadema, naombeni ndugu zangu wa Chadema, jifanyieni tathmini, nani alifanya nini, the roles walizo play, then angalia kilichokuja kuwakuta the players, na sasa Kagenzi yuko wapi na ana hali gani!. Bodigadi wa zamani wa Dr. Slaa, Khalid Kagenzi akanusha kutaka kumuua Dr. Slaa, Ya mke wa Slaa na Mlinzi binafsi wa Dk. Slaa, Tena tazameni karma ilivyo, aliyetuhumiwa kumpa sumu Kagenzi ili amtilie Dr. Slaa, na yeye alikuja kutiliwa sumu na ikamwingia na kumdhuri, tena alikuwa ni almanusura!, asingewahishwa saa hizi tungekuwa tunazungumza mengine!.
  2. Chadema mlipokuwa kwenye kikao chenu cha ndani, CC Arusha, kukatokea mtu miongoni mwenu aliyekuwa akivujisha jf, kilichokuwa kinajadiliwa ndani, mlimuita msaliti, kwa kuvujisha info humu JF, jiulizeni ni nani alimdakua mtu huyo, na mlimfanya nini!, then jikumbumbusheni kilichompata huyo kamanda shupavu aliyemshughulikia msaliti!. Kinachoendelea CHADEMA Mitandaoni: Je, ni Ushujaa wa Mhe. Lema au ni Udhaifu wa "Kule Juu"?
  3. Chadema mlipomtimua Juliana Shonza na masalia kwenye kangaroo court yenu, nililizungumzia hili, sasa leo angalieni waliomshughulikia Shonza, nini kiliwakuta, leo wako wapi, na mlinganishe na Juliana Shonza alipo!. Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili Kuwatendea Haki Watanzania 2015!
  4. Mlipowatimua kina Kitila kwa hoja ya ule Waraka wa Mabadiliko, ambao nyinyi mliuita ni waraka wa mapinduzi, mimi nikawaambie ule ni waraka wa kui transform Chadema kutoka Chama cha kiharakati, kukigeuza Chama Tawala in waiting, hivyo waraka ule haukuwa wa mapinduzi, bali a "winning coalition" kuu revamp uongozi static na stagnant wa Chadema, na kuleta uongozi mpya vibrant na dynamic, angalieni makamanda wa timua timua hiyo nini kiliwakuta, linganisha na mahali alipo Prof. Kitila, tena anakuwa Waziri kwenye key ministry!. Ningekuwa CC ya CHADEMA ningemsamehe Kitila Mkumbo
  5. Mlipomtimua Zitto kwa kutumia CC kangaroo, niliwauliza humu, CC ya Chadema, inapata wapi mamlaka ya kumuadhibu NKM wakati mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu, hakuna aliyejibu, angalieni nini kiliwakuta waliomtimua Zitto, na angalieni Zitto ni nani, tena anakwenda kuteuliwa mbunge wa kuteuliwa kwenye zile nafasi 10 za uteuzi za JPM, linganisha makamanda waliosimamia kutimuliwa kwa Zitto!. https://www.jamiiforums.com/threads...ie-mkajisahau-jiandaeni-kwa-karma.822703/Hiyo ni mifano ya dhambi ya dhana ya usaliti inavyoendelea kuitafuna Chadema ndani kwa, ndani, hapo sijamtaja Dr. Slaa, hadi watu kumuita Dr. Mihogo!, leo angalia waliombeza Dr. Slaa wako wapi, ulinganishe na mahali Dr. Slaa alipo!, haiwezekani watu na makamanda wameipigania Chadema kwa kuigharimikia kwa Machozi, Jasho na Damu, halafu leo uje uwaite wasaliti na kuwatimua kama mbwa!, kamwe Karma haiwezi kuacha salama Chadema!.
hiyo Kangaroo court ya Chadema ilipokutana kumhukumu Halima na wenzake, ndani ya majina yale 19 ya wabunge wa viti maalum wa Chadema, walioapishwa, wabunge 5 ni 'vidumu' vya wajumbe wa CC ya Chadema ambao sio vile 'vidumu' vya 'mpango kando', no!, ni vidumu vya cohabitation, mnaishi nyumba moja, mnalala chumba kimoja, kitanda kimoja!, huku mkiishi katika dhana ya ndoa, na kila mtu anawatambua kama mke na mume!, haiwezekani mwenza wako, akaibukia kwenye majina ya viti maalum bila wewe kujua, kisha akaamkia Bungeni Dodoma kuapishwa bila wewe, kujua!, namhurumia sana KM. JJ. Nnyika ni mtu muadilifu sana, lakini hajui, the games people plays behind his back. Ningekuwa mimi ndio JJ. Mnyika, kabla sijakurupuka kufanya lolote, ningefanya kwanza a due diligence, hao wabunge wameteuliwa na nani?, hiyo barua ya uteuzi imeandikwa na nani, imesainiwa na nani, inapelekwa kwa despatch gani na nani, ndipo mambo mengine yangefuata.

Miaka mingi nyuma nililizungumzia Chadema kuwa na kirusi, CHADEMA Kuna Kirusi! Je, Unajua kirusi hiki ni Nani?! Na The Motive Behind?
Sasa miaka mingi imepita nikajua sasa Chadema ni safi, kumbe bado!, na sio kuna kirusi, Chadema ina virusi!. Kikulacho...ki nguoni mwako!.

Mungu Ibariki Chadema at least for once iweze kutenda haki, kuepuka adhabu ya karma, maana kiukweli Chadema hapo ilipo, ni almost dead kinachosubiri ni kukomelea tuu msumari wa mwisho kwenye naniliu la Chadema na kulishusha 6ft under!. The choice is theirs!

Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…