Kuhusu Wabunge 19 wa Viti Maalum wakiongozwa na Halima Mdee: Mambo yako wazi ila wahusika wako kimya

KABISA,ALIYEKUA KAKA MKUU WA SHULE AKFUKUZWA,SHULE HAWEZI KUA KAKA MKUU TENA,NAFASI INAKOMA
 
Ukiwaeleza wewe kama hivi watakuelewa. Wamekuwa wakitetea ukanyagwaji wa katiba kwa sababu tu hilo lilikua linaonekana lina mkono wa Jiwe. Sasa hayupo, kama ilikua hofu ya kumuogopa Jiwe, tubadilike tuangalie ukweli. johnthebaptist unaonekana umeamua kusimamia ukweli, no matter what. Hivi watu wanashindwa hata kuangalia huo mfano wa huyo wa kutoka gerezani Singida akasafirishwa usiku kwa usiku kuelekea Dodoma kwenda kuwahi uapisho?? Uapisho wenyewe ulikua wa haraka haraka. Watavuta muda lakini ukweli unakuja na itakua aibu zaidi. CHADEMA wakikutana na Rais mambo yatakaa vizuri zaidi.
 
Mkuu, ipelekwe mara ya tatu? Ya kwanza ilipelekwa kwa dispatch na ya pili ilipelekwa kwa DHL, Zote ni December 2020.
 
Ofisi ya Spika inafanya uhuni kwenye jambo hili.. ni mbaya sana kuchezea katiba ya nchi namna hii.
 
Kwa mantiki ya uzi huu, Bunge lina wabunge wasio halali kisheria, je mambo wanayopitisha Bungeni yana uhalali gani kisheria?
Wanasheria tusaidieni katika hili!
 
Barua hiyo imepokelewa na Spika na ushahidi ni despatch.

Unataka nini tena zaidi ya hivyo??
 
Upuuzi mtupu, nilikuwa nakuamini ila sasa basi, sitakaa nikuamini tena.

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
No wonder kawe walikunyima kura
 
Petro E. Mselewa ,

..Ndugai na Tulia wanaweza kusingizia kuwa Ofisi zao hazina taarifa ya Mdee na wenzake kutimuliwa ktk chama chao.

..sasa Mdee na wenzake wamekata rufaa ya kufukuzwa uanachama. Maana yake tayari wanajua hawana SIFA za kuwa wabunge.

..kwa msingi huo, Mdee na wenzake wanatakiwa waulizwe kwanini wanakwenda bungeni wakati wanajua wao sio wanachama wa chama cha siasa?

..mimi sio mwanasheria, lakini nadhani Mdee na wenzake wanatenda makosa ya MAKUSUDI kwa kuendelea kuhudhuria vikao vya bunge.
 
Hayani uyu ndugai job karne anavunja katiba .kweli tugai ametuoa watz wote.
 

Hiki ndicho kisemwacho mara kwa mara mtaani kuwa "..politics is a dirty game...!!"

Uongozi wa Bunge, unacheza huu mchezo "kwa ujinga" mkubwa huku wakidhani na watu (watanzania) wote ni wajinga vilevile...

Funny enough, Spika Ndugai akaenda mbele zaidi akijaribu kujigeuza kuwa ni Mahakama na Hakimu kwa wakati mmoja huku akijaribu kuwavuta CHADEMA waingie ktk mtego wake huku akijua kabisa kuwa hataweza kupata anachokitafuta kutoka kwao...!

Jambo rahisi kabisa wanaloweza kulifanya hawa kina mama 19 kama wanadhani wameonewa na chama chao, ni kukimbilia mahakamani na kuomba mambo mawili au matatu tu;

1. Wanaweza kufungua shauri kuiomba mahakama ipitie maamuzi ya CHADEMA kama yalizingatia sheria na kanuni cha chama na haki za kikatiba za kila mtu

2. Ama wanaweza kuiomba mahakama iishinikize CHADEMA kuitisha kikao cha chombo cha rufaa (mkutano mkuu) ili kisikilize na kuamua shauri lao..

3. Kwa kuzingatia hoja #1, wanaweza pia kuiomba Mahakama isimamishe uamuzi wa CHADEMA wa kuwafutia uanachama wao mpaka shauri lao lisikilizwe na mahakama...

NADHANI, hiki ndicho ambacho Spika Ndugai angeweza kuwashauri hawa kina mama 19 iwapo Bunge lake linawajitaji sana ili kutekeleza wajibu wake wa kikatiba kiasi ambacho labda linadhani bila wao Bunge haliwezi kufanya lolote...

Lakini akifanyacho Spika Ndugai kwa sasa is just worthless drama...
 
Nakubaliana na maoni yako kabisa kuhusu uachama wa hao 'wabunge' 19 wa viti maalum na kwamba 'wahusika wako kimya'. Ninavyoelewa mimi, mgogoro unapojitokeza kwenye chama au sehemu ya kazi na uamuzi ukatolewa - uwe uamuzi wa haki au usiwe wa haki, uwe umefuata mchakato au haukufuata mchakato sahihi - inabidi uheshimiwe na mwathiriwa atakayeona haki haikutendeka, basi ana haki ya kukata rufaa kwa ngazi za juu.

Ndiyo maana hata katika idara mbalimbali za serikali tunasikia 'waziri kamsimamisha x kupisha uchunguzi na y kwa sasa ndiye anayekaimu nafasi ya x'. Ina maana kwamba baada ya uchunguzi, kama x atakutwa hana hatia, badala yake mwenye hatia ni z, basi x atarejeshwa kazini na kulipwa stahiki zake alizopoteza wakati alipopisha uchunguzi. Spika kuwabeba hao wabunge wa viti maalumu 19, kwa upande wangu ndiye ninayeona kama hafuati utaratibu. Sina namna nyingine ya kuliweka hili na napenda Bunge litimize wajibu wake, chama kitimize wajibu wake na wabunge wa viti maalumu 19 nao watendewe haki na haya mambo matatu yakifanyika kila party itakuwa imetimiza wajibu wake. Njia mojawapo ya kutatua tatizo ni kuliita kwa jina lake (one of the ways to solve a problem is to name it).
 

Yaani hii drama iko wazi na kama ni kesi basi hata mgambo wa jiji anaweza kuiamua kwa haki ya 100% within a minute
 
Hivi kwani Chadema wakiteua wabunge na kuwapeleka Bungeni badala ya waliopo kuna tatizo gani?
Je ni lazima kina Halima na kundi lake ndio lazima wawe wao tu ?
Ina maana kina Halima na kundi lake ni wakubwa kuliko Katiba ya Chadema?
Ina maana kanuni,taratibu za Bunge pamoja na katiba za vyama vya siasa ni kubwa /muhimu kuliko Katiba ya nchi?
 
Brother Paskal hili konde ulilowapatia huyu anaejiita wakili na timu yao kwa ujumla hawasimami,

Kaka nakuvulia kofia umeiva kwenye hii tasnia ,habari umeipanga ikapangika, huyo Petro lazima ajione choo .ni muoga ,anaogopa kutukanwa kwa kuogopa kusema ukweli ,ni wakili tapeli tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…