Kuhusu wapi naweza kupima kipimo cha PCR jijini Dar?

Kuhusu wapi naweza kupima kipimo cha PCR jijini Dar?

Akotia

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2016
Posts
528
Reaction score
1,241
Ningependa kujua wapi naweza pata kupima pcr?majibu yanatoka kwa mda gani nikipima?na mwisho nataka kujua gharama zake?Nahitajika kujua kwa haraka ili niweze kusafiri kwenda Rwanda alhamisi.

asanteni sana
 
Akotia kwa uzoefu wangu hospitali ya Temeke pale wanafanya vipimo vya PCR, kuanzia asubuhi nadhani saa mbili mpaka saa nane mchana siku za kazi na majibu unapata siku ya pili baada ya kuchukuliwa kipimo tena baada ya saa tano mchana kwa SMS/ Email, gharama ni 1,15,000/- unaweza kulipia kwa kutumia wakala au mtandaoni.
Kuna wajuzi hapa watakupa maelezo mengine ya ziada kutokana na mahala ulipo kama utapataja.
 
Duh shukran sana,kwahiyo leo nishachelewa?je lazima ufanye appointment kabla?
 
Nami ningependa kujua kama zipo sehemu zinazopima PCR na kutoa majibu siku hiyo hiyo…

Tafadhalini sana 🙏
 
Fanya booking hapa...

Utaweka namba ya passport (sina uhakika wa vitambulisho vingine)

Utachagua kituo cha afya utapoenda chukuliwa sample/pimwa (chagua hospitali za serikali rahisi zaidi ni Muhimbili)
Tarehe ya safari n.k
Ukichagua hospitali/vituo binafsi vya afya utakuwa charged more (wana kitu wanaita consultation fee) ambayo ina range kati ya 60k to 80k, na majibu huchelewa kwa sababu wanatuma sample kwenda national lab

Baada ya hapo utapewa control number ile ya eGov, utalipia kwa simu, benki n.k, gharama ni 115,000 Tshs

Ukishakuwa na risiti (kama ni benki utakuwa na kile kikaratasi cha malipo au simu utakuwa na SMS inayoonesha umelipa), utasogea kituo ulichofanya booking kwa ajili ya kipimo...

Ukipima asubuhi, majibu hutoka kesho yake kuanzia saa 8 mchana, na utayaona kupitia link watayokutumia...
 
Nami ningependa kujua kama zipo sehemu zinazopima PCR na kutoa majibu siku hiyo hiyo…

Tafadhalini sana [emoji120]
Mloganzila unapata. Maana wanachukua sample na kupima hapo hapo ukiwa na hela ya chai unaondoka na majibu yako.
 
Ningependa kujua wapi naweza pata kupima pcr?majibu yanatoka kwa mda gani nikipima?na mwisho nataka kujua gharama zake?Nahitajika kujua kwa haraka ili niweze kusafiri kwenda Rwanda alhamisi.

asanteni sana
Ukitaka kupima Covid19 ni lazima kwanza uingie huu ukurasa:

Ukishajisajili utapewa Control number. Ukishawalipa fedha zao ambazo ni kama Tsh 120,000 utapewa taarifa kwamba unaweza kwenda kupima tayari Covid. Wakati unachagua hapo juu kwenye hiyo Link juu, utachagua sehemu unayotaka kuchukuliwa Sample.
Vipo vituo vingi vya Serikali na Private ambavyo utaweza kuchagua knachokufaa.

Kumbuka tu kuwa Private wanaongeza chao cha juu na hivyo gharama inaweza kuwa zaidi ya hiyo juu ila Hospitals za Serikali bei ni hiyo hapo juu. Kujaza iko rahisi sana. Wameweka maswali rahisi kujibu kwa msafiri. Kulipa waweza hata kwa simu kwa sasa.

Kuwa Mwangalifu usikosee kwani ukishaweka Passport number, utaweza kubook sehemu moja tu kwa siku hiyo. Hivyo ukishabook kwa mfano ILALA hospital, hutaweza kubadili tena uende Muhimbili. Itabidi ubook siku moja mbele au nyuma.

Hizo sehemu zote, WANACHUKUA SAMPLE tu na hawapimi. Samples zote zinachukuliwa na kupelekewa LABOLATORY ya Taifa pale External Ubungo na hapo ndipo wanapima. Pale Ubungo, HAWACHUKUI SAMPLE.
 
Ok.
Ila maabara zote hapa mjini Dar hakuna hata moja inayofanya rapid PCR testing!!!
Bado sana.

Sina uhakika...

Kwa sasa ni kama wanalizimishwa samples zote ziende maabara kuu ya Taifa...(itakuwa ni kwa sababu za kitakwimu na kucontrol maambukizi au sababu nyingine wazijuazo wao serikali)
 
Ok.

Ila maabara zote hapa mjini Dar hakuna hata moja inayofanya rapid PCR testing!!!

Bado sana.
Sina uhakika kama Agha Khan sasa wanafanya wao. Inabidi kujua kama kuna sehemu wanafanya wao Direct. Hata Muhimbili wanafanyia Lab ya Taifa. Nimefanya wiki mbili zilizopita na majibu yalitoka saa tano asubuhi siku iliyofuata.

Airport waliweka mitambo ya kupima PCR Test kwa ajili ya wasafiri wanaosafiri na EMIRATES. Hawa walikuwa wanaambia waje masaa 7 kabla na kupimiwa hapohapo kwa mara ya pili. Sijui kwa sasa wamepeleka wapi mitambo baada ya Emirates kutuondoa kwenye RED LIST.
Wapigie watu wa Lab kama wataweza kukupa majibu zaidi.

TEL: 0734677337 au 0734677338
 
Sina uhakika...

Kwa sasa ni kama wanalizimishwa samples zote ziende maabara kuu ya Taifa...(itakuwa ni kwa sababu za kitakwimu na kucontrol maambukizi au sababu nyingine wazijuazo wao serikali)
Hapana, sample zinapimiwa pale zilipochukuliwa kwa hospitali kubwa kubwa kama Amana, Muhimbili, Mloganzila n.k

Mloganzila ukiwa na hela ya chai unayakuta majibu nyumbani siku hiyo hiyo. Naongea kwa experience.

Hata hospitali za mikoani siku hizi hawapeleki sample maabara kuu DSM!
 
Asanteni sana,nitawajuza kitachotokea.
asanteni
 
Sina uhakika kama Agha Khan sasa wanafanya wao. Inabidi kujua kama kuna sehemu wanafanya wao Direct. Hata Muhimbili wanafanyia Lab ya Taifa. Nimefanya wiki mbili zilizopita na majibu yalitoka saa tano asubuhi siku iliyofuata.

Agha Khan wanacollect tu sample na wanacharge 60k kama nakumbuka vizuri hiyo ni hela inaingia kwao, 115k unalipa serikalini...
 
Back
Top Bottom