Mlachake
JF-Expert Member
- Oct 13, 2009
- 4,472
- 4,723
Wadau, kuna taarifa ambazo zimekuwa zikisikika kwamba baadhi ya wateja waliokuwa wanapitisha mizigo yao kupitia Bandari ya Dar es Salaam sasa wanaanza kutumia zaidi Bandari ya Tanga kutokana na sababu mbalimbali kama gharama, ucheleweshaji wa mizigo, congestion na urahisi wa huduma.
Je, taarifa hizi zina ukweli kiasi gani?
Kama ni kweli, mamlaka husika zinachukua hatua gani kuhakikisha Bandari ya Dar es Salaam inaendelea kuwa chaguo kuu la wafanyabiashara?
Pia, kama kuna changamoto au kero zinazowafanya baadhi ya wateja kutafuta alternatives, je hatupo kwenye hatari ya kupoteza wateja zaidi kwenda bandari za nchi jirani kama Mombasa au Beira?
Ningependa kusikia maoni, uzoefu au taarifa kutoka kwa wenye uelewa wa sekta ya Usafirishaji.