Uchaguzi 2020 Kuiamini Tume ya Uchaguzi ni muhimu kwa Uchaguzi wa Amani

Uchaguzi 2020 Kuiamini Tume ya Uchaguzi ni muhimu kwa Uchaguzi wa Amani

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana heshima kwenu.

Kuaminika kwa mamlaka zote zinazohusika kwenye mchakato huu wa uchaguzi ilikuwa jambo la muhimu sana kwa amani yetu. Yote ni tisa, kumi ni kuaminika kwa tume ya uchaguzi ambayo haswa ndiyo yenye hii shughuli.

Ilikuwa ni jukumu la tume kuwahakikishia wadau wote kuwa inaaminika na kwamba haipendelei upande wowote katika kipindi chote cha huu mchakato.

Maonyo kwa washiriki na hata adhabu kuwa zinawahusu upande fulani tu kwa tunayoyashuhudia sote kwenye kampeni hizi kunaitia tume doa lisilopaswa kuachwa kama lilivyo.

Kwamba hata kuwa kuna tashwishi na malalamiko kuhusiana na integrity ya kura zenyewe kwenye mchakato wote hadi kutangazwa kwa matokeo? Inamaanisha hatua zilizopo hazijitoshelezi.

Yapo mengi ambayo kuyaacha hivi hivi ni kukaribisha matatizo yasiyokuwa ya ulazima hata kidogo.

Tujenge imani ya kutosha kuwa ni wapiga kura pekee ndiyo watakaoamua hatima ya uongozi hapa nchini come Oct 28.

Anasema Odinga "ati, hiyo ndiyo demokrasia."
 
Tume ya uchaguzi haiaminiki hata kidogo, itabidi tutumie nguvu nyingi sana ili haki itendeke.

Wangekuwa na nia njema, wangewashirikisha vyama upinzani hata kwa ushauri nao wakajiridhisha kuwa pana uwazi.

Kura za wazi kwa akina paskali, kina bashite na kina katawi kama ilivyokuwa ziliepusha mno marumbano ya kuibiwa kura japo bashite alilikosa sanduku moja la kura 😂😂😂.
 
Hii ni tume ya CCM

Walikuwa na nafasi ya kujivua huo u CCM kwa kumaliza ngwe iliyobakia kwa uhuru, uwazi na haki kutamalaki.

Tatizo sikio la kufa na domo chafu kama la bwana manoti. Ataacha vipi kujipendekeza kwa ajili ya teuzi zaidi.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Walikuwa na nafasi ya kujivua huo u CCM kwa kumaliza ngwe iliyobakia kwa uhuru, uwazi na haki kutamalaki.

Tatizo sikio la kufa na domo chafu kama la bwana manoti. Ataacha vipi kujipendekeza kwa ajili ya teuzi zaidi.
Wanapewa maelekezo na mzee kipara
 
Tume kutenda haki ni muhimu kwa uchaguzi wa amani
 
Upinzani ulimwekea pingamizi mgombea wa CCM kuhusu ujazaji wa form. Ni tume iliojibu badala ya mgombea. Mikutano na misafara ya kampeni ya wapinzani imejaa kamera za vyombo vya dola. Ahadi hewa za chama tawala si uvunjifu wa amani. Tume sio huru, hata mpumbavu analijua hili na ndio itakayo leta vurugu za uchaguzi
 
Kilele cha vurugu kitakuwa kwenye integrity ya kura usalama na uhalali wa matokeo.

Kama wanaitakia mema nchi hii na wakawahusishe upinzani kukubaliana kwenye uwazi, uhuru, na uhalali wa uchaguzi huu japo kwa sehemu iliyobakia.
 
Tume kutenda haki ni muhimu kwa uchaguzi wa amani
Kamwe tume haiwezi kutenda haki. Ndio chombo cha kusimamia na kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo. Umeshuhudia wagombea walivo enguliwa mwanzoni.
 
Kamwe tume haiwezi kutenda haki. Ndio chombo cha kusimamia na kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo. Umeshuhudia wagombea walivo enguliwa mwanzoni.

Tume wanayo sababu yote ya kuwekeza katika kuonyesha kuwa wanatenda haki kwa amani yetu. Kinyume cha hapo ni suala la muda tu.
 
Mkurugenzi wa tume alimpigia kampeni mgombea fulani ambaye ndio boss wake! So tume haijataka kuaminika so siiamini!
 
Mkurugenzi wa tume alimpigia kampeni mgombea fulani ambaye ndio boss wake! So tume haijataka kuaminika so siiamini!

Tume inaweza kujijengea imani kwa kuwaondosha watuhumiwa kama mkurugenzi huyu. Penye nia pana njia.
 
mpira wako, uwanja wako, referees wako, raise-men wako unashindwaje mechi. Kwa mazingira hayo timu pinzani itamuamini vipi referee?.
 
mpira wako, uwanja wako, referees wako, raise-men wako unashindwaje mechi. Kwa mazingira hayo timu pinzani itamuamini vipi referee?.

Tume isipojitathmini sawa sawa hapa tulipo tunaelekea kwenye maamuzi magumu.
 
Kamwe tume haiwezi kutenda haki. Ndio chombo cha kusimamia na kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo. Umeshuhudia wagombea walivo enguliwa mwanzoni.
kama haiwezi basi na amani haiwezekani
 
Tume hamuaminiki. Hili la kuzuia mawakala kuingia na simu ndiyo kabisa mnataka kujipalia makaa asubuhi asubuhi.
 
Back
Top Bottom