Kuibiwa kusikie tu

Busta ndio nini? Au ulimaanisha Boxer?

Na hiyo BOSSA? We jamaa mbona unatutafutia dhambi za bure πŸ˜‚
 
Pole sana mkuu, ila nyie wanaume mnapenda kuweka pesa mfuko wa suruali na unakua umetuna hivi, nashauri kama ukiweka kwenye wallet aisee ishikilie mkononi tu,ikiwa utapanda daladala
 
Siku ya jana niliibiwa pesa ndani ya daladala kiasi cha 350000 yani usiku mzima nimekosa usingizi. Hapa nilipo kichwa kinauma hatari 😭😭
Pole bothi na karibu mjini. siku ingine usitembee na mabunda ya ela keshi kwenye daladala. kuna watu wametumwa ela umu mijini wangekunyonya macho...shauri yako. shukuru haujakabwa.
 
Pole sana mkuu, ukiwa unahela nyingi mfukoni, usipende kusimama kwenye daladala( tafuta siti ukae)
Pia awe anaweka mfuko wa mbele na uwe mrefu, unaobana.

Hela ya nauli aitenge na hela nyingine kubwa, aweke kwenye mfuko mwingine, hii itamsaidia kuepuka kuvuruga hela ambazo amezitunza, kumbuka anaweza kuingiza mkono ili atoe hela kidogo ikasabisha kutoa au kuziweka karibu na kuwa rahisi kuchomolewa na mwizi
 
Asante sana kaka na nimejifunza pakubwa mkuu
Katika ulimwengu huu ambapo huduma za benki na mawakala wako kila kona kiukweli sijawahi kutembea na zaidi ya 50,000 kwa Wallet, kwanza inatuna na kuumiza ukikaa. Malipo mengi natumia lipa namba,na kiukweli faida ni nyingi ukilinganisha na makato ya kutoa hizo fedha. Pole sana ila tubadilike..
 
Nimekumis pia..ulikua wapi?.sikuoni
Nilikua hapa namsikitikia ndugu Antonio...
Heri ya mwaka mpya mtani wangu
Nikiona I'd yako nasikia raha japo ninaumia kuona simba wanatoboa ligi ya mabingwa na ligi kuu πŸ˜”πŸ˜”πŸ˜”

Anyway usiku mwema mtani πŸ€—β€οΈ
 
Yeah, kuweka hela sehemu moja inaweza kuleta shida kubwa sana, hasa hapa mjini.. ( kulala njaa, kutembea route ndefu kwa sababu ya kuibiwa nauli na n.k)

Ukifeli sana ni bora uweke hela kwenye soksi miguuni 😁, Alafu Yale makadirio ya nauli unaweka mfuko wa kawaida.
 
Hivi Mnaibiwaje...
Au huwa mnaonekana Washamba..!?

Mimi sijawahi na Siji Ibiwa. Neverrr...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…