Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimeiona ni mkatoliki, na ana foleni ndefu ya wagonjwa!Ameibuka mama anaetoa tiba ya kikombe huko Tabora kwa gharama ya TSH 500, ni muumini wa kikristo {haikutajwa kanisa gani} anatoa maombi kabla ya kikombe. Watu wengi wameonekana kwenye foleni wakisubiri tiba. Source ITV Hapa na Pale leo.
Je, hii inaashiria nini? WaTZ wengi tuna magonjwa sugu yaliyoshindikana hosptalini?, Wa TZ tumepoteza imani na tiba za Hospitali zetu, au .....?
Mkuu!Ameibuka mama anaetoa tiba ya kikombe huko Tabora kwa gharama ya TSH 500, ni muumini wa kikristo {haikutajwa kanisa gani} anatoa maombi kabla ya kikombe. Watu wengi wameonekana kwenye foleni wakisubiri tiba. Source ITV Hapa na Pale leo.
Je, hii inaashiria nini? WaTZ wengi tuna magonjwa sugu yaliyoshindikana hosptalini?, Wa TZ tumepoteza imani na tiba za Hospitali zetu, au .....?
Njaa zimejaa makanisani. Ndo maana kuna utitiri wa makanisa ambayo ndani hakuna waumini. Lengo kuganga njaa. Matokeo ni :-DECI, WANAOJIDAI KUPONYA, BABU LOLIONDo, BIBI WA TABORA, WA ROMBO, MBEYA. Yote matunda ya utapeli makanisani.
Thanks to God Hollyspirit is alive so acha wajichore kwanza, maana tumeongea mpaka sauti zimekauka kwamba hakuna tiba nje ya jina la Yesu kwa nguvu ya roho mtakatifu watu waka m ignore roho anayeishi ndani yao nakuamini ukuu wa kikombe kwa jina la yesu wa kuchongwa! Hata kama imani inakuwa ngumu kuipata thru neno basi science itusaidie maana yenyewe tumepewa kusolve carnal problems!
Ukiona mtu anakimbia huku na kule eti akidai ni imani basi ujue hata hiyo imani hajaijua bado. Kama unaamini nivipi ushindwe kuamini roho aliye ndani yako na kuamini roho iliyo ndani ya mtu mwingine? Kwenye old testament tunasoma Mungu akisema siku zile sintaandika sheria yangu katika mbao bali katika mioyo yao...inasikitisha hata baada ya Yesu kuileta sheria hiyo ndani ya mioyo bado watu wanataka kutumia sheria inferior ya mbao ambazo zilivunjika enzi hizo Musa alipozitupa chini baada ya kukasirishwa na wana wa isarael kwa ibaada zao za sanamu.
Tulieni katika uwepo wa mungu ambaye Yesu ametuambia tumwabudu katika roho na kweli. Ni bora tufe kwa magonjwa ya mwili kuliko kufa kiroho na kurushwa rushwa kama makapi na imani za dunia hii ambazo ziko kumdhalilisha mwanadamu. Mungu anapata utukufu gani pale Loliondo? Nature inaharibiwa, watu wanakufa kila leo na bado kukaa masaa yote bila kula wala kunywa for something which you can easly get in you bila hata kumsujudia mtu. Hivi hamuoni kuwa mnamsujudia Babu kwa kufuata masharti yake magumu ya yy pekee kugawa kikombe? Dont you see he is maqking himself a god? Is he not an idol?
something to do with 21- 05- 2011???!Mkuu nami pia nimeiona hiyo story(kupitia TBC1)! Yaani sielewi matukio haya mwisho wake utakuaje! Ni kweli ni miujiza ya Mungu yule tunaemwabudu na kumwamini au kuna something else?
Duh, jamani kuna mwanamke tabora naye anatoa tiba kwa mtindo wa babu wa loliondo kwa chaji ile ile ya sh. 500 na watu kibao wanakunywa.
Source: Itv
Watanzania tumepoteza matumaini kwa kiasi kikubwa.Mbaya zaidi na Serikali inayabariki haya.