Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
asigwa huwez kuamini school of pharmacy MUHAS wanafundisha haya, na hata Nelson Mandela university. unajua tatizo ni nini?? wanachoombea lesen wengi wao kaa umechunguza sio wanavyo uza, ni sawa na duka la Mangi atasema ni duka la vyakula lkn humo ndani atauza hadi sumu ya panya, mafuta ya taa na panadol.Nimekuelewa sana mkuu, na mimi kinachonitatiza ni vibali na vyeti vya uthibitisho walivyo navyo hawa watu kwani inaonesha wana vibali vyoote kutoka wizarani na hata Muhimbili kufanya shughuli zao, japo hata madawa waliyo nayo hawayajui yanaundwa na nini
Kwa kuwa inaonekana wanawasaidia watu japo kwa trial and error nadhani imefika wakati serikali ianzishe kabisa chuo cha tiba mbadala na wapewe elimu yao bila urasimu kwani hata hizo tafiti za NIMR ni gharama sana kuzifanyia kazi na dawa zao japo zinatumia hii hii mimea inayouzwa shillingi mia sokoni wao wanauza madawa kwa malaki sasa kwa nini watoto wa mjini wasi-take advantege hapo???
Ha ha ha nimeipenda hii ya supu(mchemsho)
Ni kweli Tanzania hatuna vyombo vya utafiti na hili ndilo tatizo, juzi nimepita pale ferry jamaa mmoja alikua anaelezea madhara ya kaloraiti wanayopaka kina mama usoni pamoja na griseline nikashangaa sana.
Jamaa kawakusanya watu kama mia kadhaa hivi wasiojua mambo ya chemistry wala chemical reactions, kachukua gazeti kalipaka calorite halafu juu yake kamwaga griceline kidogo halafu kachukua ile GV ya kusafishia vidonda alipoimwaga tu gazeti liawaka moto likateketea loote, watu wakabaki modomo wazi , Wakashindwa kuelewa ni kwa temperature gani hiyo chemical reaction na kwa level gani ya humidity na mgandamizo(atmospheric pressure) hayo hutokea.
Nilipomuuliza kuwa kwa kuwa unaamini kuwa maji yanachemka kwa 100 degree Centigrade je haamini kuwa maji hayo hayo tukiyapa pressure fulani yaweza kuchemka katika 20 dgree Centrigrade vile vile, akasema yeye hayo hayajui na hajui lolote kuhusu chemistry na shule hajakanyaga..Nilipomuuliza kuhusu contents za hivyo alivyochanganya vikatoa moto ni zipi hakujua vile vile.
Lakini cha ajabu ana majarida na ana vibali vyoote vya afya kuwa ni "certified professional"..hapa ndipo nikajua kuwa tatizo ni elimu tu hakuna jingine...
Japo hawa jamaa wanafanya kazi ya maana na wana facts ambazo kama hujapita level zile huwezi kuwabishia, lakini wanasaidia mengi na wanasaidia wengi vile vile
Ha ha ha mkuu naona unatafuta kupigwa mawe humu ndani na baadhi ya watu aisee....wengi wao ni wasabato kina ndodi
Lakini mkuu hii kitu ya tiba asili sio Tanzania tu ni dunia nzima..Na ilianza USA baada ya serikali yao kukuta wanatumia more than $1 trillion(dola trillion moja) kwenye mambo ya afya tu kwa mwaka, na katika kupunguza hili wakaja na suala zima la tiba mbadala...
Kimsingi tiba mbadala sio mbaya ila wafanya biashara wa kibongo ndio wanaoiharibu dhana hii kwa ujumla, kwani mataifa yoote duniani yamegundua kuwa inawezekana kupunguza bajeti za afya kwa kurudi katika asili na hasa vyakula na herbs..
Na wameweza sana, juzi nilikuwa nasoma classified document(reserach) fulani ya matibabu ya kansa kutoka marekani, inadai kuwa makampuni ya kutengeneza dawa za kansa hasa level one na two yamekuwa yakitumia matunda ya stafeli kutengeneza dawa zao na ili kukwepa kupunguza faida inayotokana na biashara ya dawa hizo wakaamua kuficha kuwa dawa hizo zinatengenezwa kwa 100% na mmea huo wakadai kuwa serikali kwa kuwa wametumia kiasi kikubwa sana cha fedha katika research hiyo na bado ugunduzi haujarudisha fedha iliyotumika hivyo basi jamii ifichwe mpaka muda muafaka utakapofika, lakini bahati mbaya zikavuja..
Tunaoweza kuwalaumu hapa ni wabongo kuchakachua taaluma hii kwani wao huamini kila kilichotoka kwenye mtandao wa internet ni sahihi, na serikali kutokuwekeza huko pia kwa maana ya vifaa na reseach ili kujua contents za hizo tiba mbadala chemically ni nini..
Ila kwa sasa dunia nzima inahamia katika tiba hizo na ni kitu kisichoweza kuepukika kwani medical science imeanza ku-fail kutoa majawabu kwa baadhi ya matatizo na magonjwa