Huyu hapa
Julius S. Mtatiro
RAIS KIKWETE ANASEMA KUANZIA
MWAKA 2016 CCM ITATOA ELIMU YA
SEKONDARI BURE...
Kwa nini aanze kupanga sera za serikali
ijayo wakati yeye atakuwa Msoga, kijijini
kwake? Na kama yeye ni bingwa wa
mipango mbona mwaka huu peke yake
vijana zaidi ya 20,000 wamerudi
majumbani kwao kwa sababu wamekosa
mkopo wa elimu ya juu?
Wakati Rais anasema hayo nimejionea
jana wafanyakazi wa TAZARA wakianza
mgomo kwa sababu hawajalipwa
mishahara ya miezi mitano, wakati huohuo
nimeona walimu Kinondoni wakiandamana
kudai fedha zao.
Badala ya kuanza kufikiri kipropaganda
dhana ya kusomesha sekondari bure
mwaka kesho, kwa nini tusilipe ada za
watoto hawa masikini wa vyuo vikuu
ambao wanahitaji msaada sasa hivi ili
hayo ya mwaka kesho tuyapange wakati
wa kampeni mwezi oktoba 2015?
Vyama vya upinzani viliposema utoaji wa
elimu bure mwaka 2000, 2005 na 2010,
CCM ilisema vinaongopa na haiwezekani
na wananchi waliamini uongo wa CCM.
Hata hiyo elimu ya msingi tu CCM
imeshindwa kutoa bure, michango iliyopo
sasa inazidi ada ya zamani.
Kinachoonekana hapo ni propaganda za
kuanza kuwaweka sawa wananchi kwa
ajili ya uchaguzi wa mwaka.
Si ajabu kuwa, Kinana na Nape
watazunguka nchi nzima katika mikutano
yao ya mwaka huu, wakieleza sera hii ya
elimu ya sekondari ambayo kuitekeleza
hawawezi.
Na hapohapo wanasahau kuwa mambo
mengi yaliyoahidiwa na CCM mwaka 2010
hayajatekelezwa, Mahakama ya kadhi
siioni, waliahidi!
Ni jambo la ajabu mno kukuta kiongozi wa
nchi ambaye anamaliza muda wake
anaanza kupanga ahadi za serikali ijayo,
wakati uongozi wake umeacha majanga
mengi katika nchi huku ukishindwa
kutekeleza ahadi zake nyingi! Sijui
mnanielewa?
J. Mtatiro,
Dar Es Salaam,
11 Januari 2015.
2 hrs · Public