Uchaguzi 2020 Kuichagua CCM ni kuchagua mateso makubwa

Uchaguzi 2020 Kuichagua CCM ni kuchagua mateso makubwa

Fundi Madirisha

Senior Member
Joined
Jun 30, 2020
Posts
184
Reaction score
988
Kuchagua CCM ni kuwafungia zigo la mateso makubwa Wananchi. Ni kuchagua maumivu makubwa kwa Watanzania ni lazima tuwe makini zaidi.

1. Kuchagua CCM ni kuchagua watu kuendelea kupotea bila kujua walipo, ni kuchagua watu kuendelea kupigwa risasi na wasiojulikana bila kuwajua ni kina nani.

2. Kuichagua CCM nikuchagua kutumia pesa za miradi mingi kutumika bila kupitishwa na bunge. Hapa ni kuchagua pesa zetu kutumika hivyo huku tukidanganywa eti wanawajali wanyonge.

3. Kuichagua CCM ni kuchagua kuibadili katiba ili Magufuli aendelee kutawala zaidi ya miaka 10, Ndungai na Ally Kesy wanalijua hili.

4. Kuchagua CCM ni kuchagua vyombo vya habari kunyimwa uhuru wa kusema. Ni kuchagua kunyima sauti za wananchi.

5. Kuichagua CCM ni kuchagua Mateso makubwa kwa watumishi wa umma kutoongezewa mishahara na malimbikizo yao.

6. Kuichagua CCM ni kuchagua kilio kwa wanafunzi elimu ya juu makato makubwa 15% na ubaguzi mkubwa kwenye utoaji mikopo.

7. Kuichagua CCM ni kuwaumiza Wastaafu kutopata nafasi yao mapema na kuchagua kukosa fao la kujitoa.

8. Kuichagua CCM ni kuchagua Mama zetu kujifungua kwa gharama kubwa mahospitalini.

9. Kuichagua CCM ni kuchagua mifumo mibovu ya biashara na kuendelea kuzorota kwa biashara na pesa kuwa ngumu.

10. Kuchagua CCM ni kuchagua kuzorotesha bei za mazao yetu kama vile Korosho, Kahawa, Pamba ni.

MTANZANIA ZINDUKA ACHANA NA CHAMA KILICHOCHOKA HAKINA MSAADA KWAKO. ACHANA NA MAUMIVU HAYA.
 
Actually inawezekana CCM kama CCM Institution, haina shida kubwa kihivyo, Hapa kuna mtu mmoja Magufuli. Kuchagua Magufuli ni kuchagua KIFO na MAUTI. Hapa kuna mtu mmoja authoritarian anavuruga kila kitu na wapambe wake.
 
Kufuatia Kauli ya Tundu Lissu.

Yemwe yemweeeee

IMG_20200914_064018_704.jpg
 
Umeongea ukweli mkubwa sana ndugu!!! Hivi naachaje kumchagua Lissu wakati ana Sera ya kumsomesha hata mwanangu ambaye nimemsomesha private?

Hivi naachaje kumchagua Lissu ambae anarudisha makato ya mikopo ya bodi ya mikopo kutoka asilimia 15 ya magufuli hadi asilimia 6???

Hivi naachaje kumchagua Lissu ambaye ametoa Sera ya kunijali mimi mlipa kodi na mfanyabiashara kwa kuniwekea mswada wa kunilinda mimi mlipa kodi ili TRA wasininyanyase?

Hivi naachaje kumchagua Tundu Lissu ambaye hataniwekea mipaka kwenye masoko ya kuuza mazao yangu niliyoyalima kwa jasho kubwa?

Hivi naachaje kumchagua Tundu Lissu mwenye Sera ya kurudisha katiba mpya ya warioba itakayoweka misingi ya utawala bora na kuondoa matumizi mabaya ya madaraka?
 
Wanaume tumeumbwa kwa ajili mateso, imeandikwa hata kwenye vitabu vya dini. Hivyo wanaume yatupasa tuipigie kura ili hayo maneno yatimie
 
Hivi hao wanaomtetea magufuli wana sababuz zipi yaani. Nimeamini tunaishi na mashetani nchi hii.
Katiba imetupa uhuru wa kumchagua mgombea yeyote kadri inavyotupendeza. Tumeamua kumchagua Magufuli
 
Ilo liko wazi kabisa kwa mtu mwenye akili timamu.Ndo maana ukiona wanaokishabikia hicho chama jua wana matatizo haya yafuatayo,aidha ni waoga wa mabadiliko, au ni wanufaika wa mfumo mbovu uliopo,au uwezo wao wakufikiri nakuchanganua mambo ni mdogo kwahiyo wanasubiri kuambiwa kila kitu bila kushirikisha akili zao kwahiyo wamekariri maisha,au jua kwao wao mambo mabaya,shida,umaskini na mateso ndio furaha yao.

Na bora awe ni mtu kuanzia miaka 50 kwenda mbele unaweza kusema kuna vitu vya msingi alikosa lakini ikiwa ni kijana unaona kabisa wengi wana hayo matatizo hapo juu.
 
Back
Top Bottom