Mungu jalia katika kipindi cha uhai wangu nimepanga kutumia fursa ya kutembelea mikoa yote ya nchi ya Tanzania ili kuweza kuifahamu Tanzania vizurizaidi pamoja na watu wake wakazi wa mikoa hiyo.
Dhamira yangu ni kwamba kila mwaka wakati wa likizo ya mwaka kazini, basi nitumie siku chache za likizo nifanye safari katika mkoa mmoja au miwili na niweze kupata nafasi ya kujichanganya na watu wa eneo hilo kujua zaidi mkoa kwa mfano kutambua mazuri na mapungufu katika nyanja za utafutaji maisha, mila na desturi za wakazi wa mkoa, na mambo mengineyo.
Mpaka sasa, nimepata fursa ya kutembelea mikoa michache sana.
Mikoa hiyo ni Dar es Salaam (ndiyo makazi yangu), Pwani (nategemea kuhamia Pwani wakati wa kustaafu), Morogoro, Kilimanjaro, Bukoba, Dodoma, Arusha (zamani sana nilienda huko) na Songwe (Tunduma).
Mikoa ya Western na Southern Tanzania pamoja visiwani Zanzibar na Pemba ni maeneo ambayo sijapata muda au sababu ya kutembelea kipindi cha nyuma na hivyo nimeweka kipaumbele kutembelea mikoa hiyo kwa awamu. Mwaka huu mwezi September nimepanga kwenda Mtwara (Masasi na Mtwara mjini).
Kwa miaka mingine ijayo nitaendelea na mpango huu wa kutembelea mikoa mingine ili niweze kuifahamu Tanzania yote na ku-appreciate uzuri wa mikoa pamoja mazuri na changamoto zake.