SoC04 Kuifikia Tanzania Tuitakayo: Matatu ya Kuweka Kipaumbele kwa kuelekea Tanzania Yenye afya njema

SoC04 Kuifikia Tanzania Tuitakayo: Matatu ya Kuweka Kipaumbele kwa kuelekea Tanzania Yenye afya njema

Tanzania Tuitakayo competition threads

josee israel

Member
Joined
Jun 2, 2024
Posts
6
Reaction score
1
Kumekuwa na kasi ya ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kulingana na tafiti za shirika la afya duniani (WHO) takriban asilimia 74 ya vifo vyote duniani vinasababishwa na magonjwa yasiyoambukiza nah uku magonjwa kama vile kisukari,shinikizo la damu,magonjwa ya figo na magonjwa ya moyo yakiongoza kusababisha vifo vya watu wengi zaidi.

Jambo linalosikitisha zaidi ni kwamba magonjwa kama vile kisukari na magonjwa ya figo ambayo yalikuwa yanachukuliwa kama ni magonjwa ya watu wenye umri mkubwa zaidi yamekuwa yakiwapata hadi Watoto na vijana wenye umri chini ya miaka 40 wamekuwa wakisumbuliwa na magonjwa haya nini kifanyike sasa? Ni swali ambalo kila mmoja anapaswa kulitafakari katika Makala hii ili kuifikia TANZANIA TUITAKAYO ile Tanzania ambayo ipo huru kiafya ,ambayo wananchi hawasumbuliwi na magonjwa ambayo kiukweli yanaweza kuepukika ,yanaepukika pale tu ambapo tutabadilisha mitindo ya kimaisha na kufuata mitindo mizuri ya kiafya matatu yafuatayo yanabidi kuzingatiwa ili kuifikia TANZANIA TUITAKAYO yafuatayo yazingatiwe na kila mtanzania

Ushughulishe mwili wako
Mifumo ya sasa ya kimaisha imekuwa chanzo kikubwa cha ukosefu wa shughuli za mwili. Aina za kazi zimebadilika, kazi ngumu za mikono zimebadilishwa na kukaa kwa muda mrefu kwenye ofisi. Ratiba ngumu za kazi na kutegemea usafiri wa magari kwenda kazini na kurudi nyumbani kunapunguza zaidi nafasi za kufanya mazoezi. Hata burudani mbalimbali ikiwemo televisheni, kompyuta, na michezo ya video - vyote vikitufanya tuketi tu kwenye sofa. Mabadiliko haya yote ya mtindo wa maisha wa kutofanya mazoezi yana athari mbaya kwa afya yetu, ikihusishwa na kuongezeka uzito, magonjwa sugu, na hata kuathiri ustawi wa akili. Hata hivyo, vita dhidi ya ukosefu wa shughuli za mwili bado inaweza kushinda. Kwa kufanya mabadiliko madogo, tunaweza kuwa watu wenye shughuli nyingi zaidi. Chukua matembezi mafupi wakati wa mapumziko kazini, punguza muda wa kutumia simu na badala yake fanya mambo yanayohitaji shughuli za mwili kama burudani, na ujitahidi kufanya shughuli ndogondogo kama vile kuegesha gari mbali zaidi, kutumia ngazi badala ya lifti, au kutumia nguvu zaidi katika kazi za nyumbani. Muhimu zaidi, tafuta aina ya mazoezi unayofurahia, iwe ni michezo ya timu, kucheza, au mazoezi ya mtu mmoja. Kwa kufanya mabadiliko haya katika mazingira yetu ya kazi na utaratibu wa kila siku, sote tunaweza kuwa watu wenye shughuli nyingi zaidi na kujenga msingi wa maisha yenye afya na furaha.Na tutaifikia TANZANIA TUITAKAYO

Ongeza mbogamboga na matunda katika mlo wako
Kumbuka kwamba unachokula kinaweza kuwa dawa kwa mwili wako au unajilisha sumu mwilini mwako naweza kusema wewe ni kile unachokula ilikuwa rahisi kwa babu na bibi zetu kuwa wenye afya na wenye nguvu inashangaza zaidi kwamba hata magonjwa haya hayakuwepo kwa kiasi kikubwa kwani walikula vyakula sahihi na vyenye manufaa makubwa kwa mwili lakini kwa kipindi tunachoishi mambo yamebadilika sana inakuitaji bidi kula chakula bora na kuwa mwenye afya kwa ujumla kwani tumezungukwa na vyakula ambavyo vina kiwango kidogo cha virutubisho “tunashiba lakini bado tuna njaa kali”

Duniani yetu ya kisasa inatoa kipaumbele kwa starehe kuliko afya, na hivyo kusababisha mabadiliko makubwa katika vyakula tunavyokula. Vyakula vilivyosindikwa, vinywaji vyenye sukari nyingi, na milo mikubwa sasa ni kawaida, na hivyo kuchangia mafuta yasiyo na afya, sukari iliyoongezwa, na kalori nyingi.tunakula lakini tuna njaa inashangaza lakini ni ukweli mtupu tunakula lakini tunavyokula havina virutubisho tuna njaa njaa ya virutubisho , Mtindo huu wa maisha wa "chakula cha haraka" unachangia ongezeko la watu duniani kote kuwa wanene kupindukia na kuongeza hatari ya magonjwa sugu. Lakini mabadiliko yanawezekana! Kwa kutoa kipaumbele kwa vyakula halisi kama vile matunda, mboga mboga, na nafaka nzima, tunaweza kupunguza vyakula vilivyosindikwa. Kupika nyumbani, kupanga milo, na kusoma lebo za chakula vyote ni silaha katika vita vyetu vya kupata mlo wenye afya. Hatua ndogo kama vile kubadilisha vinywaji vyenye sukari na maji na kutumia sahani ndogo zinaweza kuleta mabadiliko makubwa. Kumbuka, mlo wenye afya ni msingi wa wewe kuwa na afya njema!
Mazingira tunayoishi watu wamepuzia umuhimu wa mbogamboga ,matunda hayaliwi tumekuwa walaji wazuri wa vyakula kama vile chipsi ambavyo kiukweli faida zake ni ndogo sana kwa mwili

Pia unywaji wa maji watu wengi wanasahau umuhimu wa maji kunywa maji ni muhimu kwa mwili hasa katika kusaidia ufanyaji kazi wa viungo kama vile figo inashangaza watu wanakula vyakula kama vile chipsi chumvi nyingi alafu hawanywi maji ya kutosha ,badala ya kunywa maji soda na “energy drinks” zimekuwa mbadala kwa vijana wengi na huenda hii pia ni moja ya sababu katika hospitali zetu kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa figo “hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imetangaza kuwa inapokea wagonjwa wapya wanne mpaka tisa kila wiki wenye umri kati ya miaka 24 mpaka 40“ takwimu toka katika gazeti


Turudi majumbani
Turudi tukapike vyakula vyetu wenyewe vyakula vyenye kiwango kidogo cha chumvi , vyakula halisi,vyakula vyenye kiwango sahihi cha sukari,vyakula vyenye virtubisho sahihi kwaajili ya miili yetu ,tukirudi nyumbani tutapunguza ulaji wa vyakula vya viwandani tutakula vyakula halisi ,kutapunguza hata matumizi ya pombe kwa kiasi Fulani

Ukweli ni kwamba Kurudi nyumbani mapema baada ya shughuli za kila siku kunaweza kuifanya nyumba yako kuwa kimbilio la afya kwa familia. Kuachana na msongo wa mawazo kazini na shuleni kunawaruhusu wote kupumzika, na hivyo kusaidiausingizi mzuri kwa kupunguza wasiwasi. Usingizi huu bora ni muhimu kwa ustawi wa kimwili na akili wa wazazi na watoto. Aidha, kupika chakula nyumbani huwapatia familia uwezo wa kudhibiti viungo wanavyovitumia katika chakula . Hii inawawezesha kuchagua vyakula vipya, vyenye lishe bora kwa kila mtu, tofauti na matumizi ya vyakula vilivyosindikwa au milo isiyo na afya ya migahawa au viwandani ambavyo hujui vimetengenezwaje. Mwishowe, kuanzisha utaratibu wa kupumzika kabla ya kulala, kama vile kusoma au kuoga, sio tu huboresha ubora wa usingizi bali pia huunda nafasi ya kuwasiliana na watoto. Hii inakuza mawasiliano mazuri na kuimarisha uhusiano wa kifamilia, na hivyo kuweka msingi wa tabia njema za kiafya kwa kila mtu katika maisha yao yote.

Kuifikia TANZANIA TUITAKAYO ni muhimu kujua kwamba afya ni hazina kubwa tunayoihitaji kama taifa ili kufikia maendeleo kwa kuzingatia mambo matatu yaliyoelezwa katika andiko hili
 
Upvote 0
Back
Top Bottom