Dr Adinan
Member
- Jul 11, 2021
- 14
- 22
Utakumbuka wakati ule ametangazwa mgonjwa wa kwanza wa COVID-19 Tanzania, watu wengi walianza kuchukua tahadhari. Lakini kirusi alishaingia Tanzania. Watu baadhi wakaumwa. Kwakuwa tahadhari ilikuwa juu, idadi ya waliokuwa wanaumwa ikaanza kupungua. Virusi hawakuwa wameisha! Walikuwa wachache. Na walizunguka kwa watu wachache.
Virusi wakaendelea kusambaa kwa watu kidogo kidogo. Mwisho walioambukizwa wakawa wengi! Nao wengi walioambukizwa virusi wakaweza kuwaambukiza wengi. Idadi ikawa kubwa tena! Ikawa kama wimbi la maji: lilipanda, likashuka, likapanda tena.
Wimbi linamaanisha kuongezeka kwa idadi ya watu wagonjwa, na kisha kupungua. Neno “wimbi” linamaanisha muundo wa asili wa vilele na mabonde. Maana yake ni kwamba wakati wa mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza, hata kama maambukizi yamepungua, milipuko ya baadaye ya magonjwa inawezekana.
Ndiyo maana nasema, uchaguzi uko kwetu! Kuingia au kutokuingia kwa wimbi hili.