indian mark 2
JF-Expert Member
- Jan 3, 2015
- 397
- 301
Habari za jion wakuu,
Kama nilivyoeleza hapo juu kiukweli nimejitahidi kufatilia hizi vuguvugu za uchaguzi kupitia vyama vyote vikiwemo vya upinzani na hata chama tawala nikakaa nikawaza nikasema hapana ngoja niandike kitu..
Jamani napenda kusema kwamba tusijidanganye kama CHADEMA wanaweza kukitoa chama tawala kilichoshikilia dola kwa staili hii wanayoenenda nayo, nasema tena nikujidanganya kwa kiwango cha barabara za mkulu.
Kwasababu moja ambayo nadhani wapinzani wanaijua au hawaijui kwanini nasema hivyo ni kutokana na huyo mkurugenzi mkuu wa tume ya uchaguzi ni kada tena kada kindakindaki
Mwaka 2015 aligombea jimbo la Ubungo kwa tiketi ya chama chake na hakufanikiwa kupata kura za kutosha na aliishia kupata nafasi ya 5 na baada ya hapo akaja kuteuliwa kuwa mkurugenzi Arusha na baada ya kugombana huko na mkuu wa wilaya huko ndiyo akaja kupewa hiko cheo alichonacho sasa hivi.
Sasa kwa mazingira kama hayo mnadhani hata ningekuwa mimi naanzaje kumkataa mtu ambaye amenipa ugali hahahahaha tuendelee kujichekesha maana safari bado kubwa sana.
Na kwa jinsi ninavyowaona CHADEMA wanavyofanya hizo kampeni zao ni kama hawakujiandaa kabisa tuwe tu wakweli kulidondosha jiwe kunahitaji support kubwa sana na mbinu lukuki za kampeni kwa staili yoyote ile.
Niwatakie kazi njema katika kulitumikia taifa na tuwe wazalendo wa kweli katika kuisogeza nchi yetu mahali panapostahili.