Kuipunguza damu ni kuchangia tu au kuna njia nyengine?

Kuipunguza damu ni kuchangia tu au kuna njia nyengine?

Naxria abdalla

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2025
Posts
204
Reaction score
379
Rafiki zangu nimerudi tena nimeenda hosptal nimepima vipimo wakaniambia nina damu nyingi ambayo ni 17.1 amenambia ndio chanzo naumwa na kichwa pia najiskia vibaya,naomba ushauri kuipunguza damu ni kuchangia tu au kuna njia nyengine?
 
Mbinu hiyo ya kukutapeli damu yako wakauze. Na usikute una group adimu la damu
 
Naskia mbu pia wanapunguza damu, kwa wastani mbu mmoja anaweza kunyonya lita 70 kwenye uhai wake wote.
 
Rafiki zangu nimerudi tena nimeenda hosptal nimepima vipimo wakaniambia nina damu nyingi ambayo ni 17.1 amenambia ndio chanzo naumwa na kichwa pia najiskia vibaya,naomba ushauri kuipunguza damu ni kuchangia tu au kuna njia nyengine?

Kabla ya kuhangaika na kiasi cha damu kama tatizo la msingi, ni vyema:

1: Kuhakiki huo wingi, upate vipimo kwa maeneo tofauti/maabara na kujua ni kwa kiasi gani iko juu ya kiwango tarajiwa. Hii ni baada ya kunywa maji vyema(lita2-3 kwa siku).

2: Kuhakiki kama kichwa kuuma ni shida itokanayo na wingi wa damu tu kwa mhusika na si vinginevyo/hakuna kisababishi kingine. Kazi ya mhudumu wa afya.

3: Kwenda hatua nyingine, kujua sababu ya damu kuwa nyingi/juu kama ndivyo:
(a)Hali ya kawaida/physiolojia kama kwa watu wafanyao mazoezi/wanariadha

(b)Suala la umbali toka usawa wa bahari/ Environmental issue/attitude?

(c) hakuna magonjwa mengine ya kimfumo/ systemic disease?

(d)Tatizo kwenye sehemu zinazotengeneza damu kama mifupa/Bone marrow issue?

NB: Hapa kama uko sehemu inayofikika kwa wahudumu wa afya husika(daktari bingwa wa mfumo wa damu/ Haematologist anahusika kwa sana. Hii ni kama tatizo litabaki kuwa ni wingi wa damu ili kuweza kutanabaisha vyema ni nini tatizo na nini kifanyike.
 
Back
Top Bottom