Kuishi bila ya kuwa na Mtoto ni uamuzi mzuri pia

Mjanja M1

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2018
Posts
4,058
Reaction score
14,382
Kuna baadhi ya watu wameamua kutokuwa na watoto na wana sababu zao za msingi,

Sababu zao,
  • Hawataki kujipa kazi ya kulea kwasababu kulea ni kazi kama kazi nyengine uzijuazo.
  • Hawataki matatizo endapo mtoto akiwa pasua kichwa mbeleni
  • Hawaamini kuwa wanaweza kuwa wazazi bora kwa mtoto n.k

EWE KAPUKU! UNAPOONA MTU HANA MTOTO USIJIPE UMUHIMU WA KUMSEMA MAANA HUJUI SABABU YA YEYE KUCHAGUA MAISHA HAYO.

Note: Mjanja M1 kwasasa napatikana Paris nchini Ufaransa 🇫🇷
 
🤣🤣🤣🤣 upo sahihi shida wabongo kuopangiana maisha na umaskini umekithiri haadi umeathiri ubongo, kuna watu Wana watoto watano wamepanga chumba na sebule, jiulze hapo wanaishije tena watoto jinsia tofauti
 
Kuna umri ukifika hata kichaa anatamani kupata mtoto. Ni majaaliwa ya Mungu tuu kupata au kukosa, lkn ukisema eti mtu anapenda mpaka kufa eti asipate mtoto ni urongo mkubwa.
Kwa nini unataka kumsema mtu mwingine?

Mtu akisema hataki mtoto, wewe ni nani mpaka useme huyo mtu ni muongo?

Unajuaje hisia za mtu mwingine zikoje?
 
Kwa nini unataka kumsema mtu mwingine?

Mtu akisema hataki mtoto, wewe ni nani mpaka useme huyo mtu ni muongo?

Unajuaje hisia za mtu mwingine zikoje?
Nimesoma utafiti. Wengi wanamatizo, wanajificha kwenye kichaka cha eti tumeamua kutokuzaa. Ni urongo mkubwa
 
Kusudi lako la kuja duniani ni lipi hasa......
 
Watu wa Morogoro mnapenda kutoa kafara kizazi ili mpate pesa.
Achaneni na hizo tabia shwaini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…