Kuishi na mke kunataka uvumilivu wa chuma

Kuishi na mke kunataka uvumilivu wa chuma

Mkuu sema umeoa mwanamke asiesoma bila shaka...
 
hebu mtupishe, kuna watu wanavumilia kwenye ndoa kama wanawake? tena sio kumvumilia mume tu, unamvumilia mume, wakwe, mawifi na mashemji, tatizo lenu wanaume mnapenda kuabudiwa na hizo zama za mama zetu na bibi zetu zilishapita na wao walikuwa na haki ya kuwanyeyekea sababu walikuwa wanakaa tu nyumbani kazi kuu ni kuzaa na kulea na kumuhudumia mume, sasahv nimwendo wa sawa kwa sawa, haiwezekani wote tunatoka asubuhi kila siku tunarudi wote jioni mwisho wa mwenzi wote tunaleta mezani mishahara, alafu utake kujifanya mfalme wa nyumba. Maisha ya sasa ni kusikilizana na kuelewana kiustaarabu tu nyumba itaenda ila ukileta ubabe kweli ndoa utaiona chungu
Duh !
 
WAPALESTINA ni mwisho wa RELI. Kuna jirani yangu anakula mkong'oto balaa siku majiran kwenda kuulizia tulipatwa na aibu maana jamaa alijificha chumbani
 
Na wanawake walioolewa wanajisahau saana! Anadhani akishavaa shela ndo kazi imeisha! Walegee tu sie tuendelee kuwaibia waume zao [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji85]
Hongera,, .
 
Hivi hakunaga testimony nzuri ya ndoa....kila siku negative tu....[HASHTAG]#SIOI[/HASHTAG] ngoja nsake tu mtoto wa pili na mtu fulani.......ika we sasa huu uboya...unaamia ufue wewe...kweli hujawa kichwa bado kukanyagwa.....house girl anafanya usafi chumbani....wife nadhani bado ana akili za kitoto...au kajisahau....endelea kuzifua tu..
 
hebu mtupishe, kuna watu wanavumilia kwenye ndoa kama wanawake? tena sio kumvumilia mume tu, unamvumilia mume, wakwe, mawifi na mashemji, tatizo lenu wanaume mnapenda kuabudiwa na hizo zama za mama zetu na bibi zetu zilishapita na wao walikuwa na haki ya kuwanyeyekea sababu walikuwa wanakaa tu nyumbani kazi kuu ni kuzaa na kulea na kumuhudumia mume, sasahv nimwendo wa sawa kwa sawa, haiwezekani wote tunatoka asubuhi kila siku tunarudi wote jioni mwisho wa mwenzi wote tunaleta mezani mishahara, alafu utake kujifanya mfalme wa nyumba. Maisha ya sasa ni kusikilizana na kuelewana kiustaarabu tu nyumba itaenda ila ukileta ubabe kweli ndoa utaiona chungu
Kawe mwanaume tu sasa.
 
Najaribu kukusoma, wewe ni miongoni wa wake wenye maneno kama cherehani[emoji3]
Jamaa atakuwa anapata shida, ila wanawake wengi wenye maneno mengi hawadumu kwa ndoa[emoji12]
.
Hata hivyo dawa kubwa ya ndoa ni mwanaume kuwa na wake wawili au zaid,
facts
 
Kuna vitu vingi sana vinavyowezesha ndoa idumu, ila kwa uchache ni;
+Kumuogopa muumba ( for believers)
+Upendo
+Kuvumiliana
.....unapoingia ktk ndoa yapasa ujue kuwa watu mmeumbwa na tabia tofauti, na pia mmelelewa ktk mazingira tofauti, vyote hivi lazima au possibly vinaweza leta kutofautiana ktk ndoa yenu.
Pia utofauti wa elimu mlizonazo kunaweza leta misuguano, ukiwa mmoja umesoma sana mwingine hajasoma kivile au kafeli feli inaweza leta kitu "inferiority complex" ukadhani kila unalosema ndo sahihi na anatakiwa afuate tu, na yeye pia anaweza kuona ume overlook jambo akahofu kukueleza b'se unaamini yeye hawezi kuona kitu kwa usahihi, akikuacha mnapotea wote, na akikuambia unakua mkali.
Lakini pia anaweza kuwa kweli anakosea, ila kwakua anajua yeye hajasoma kuliko wewe anajenga fikra kua kila unapomrekebisha ni kwa sababu tu unajua ye hajasoma so unadharau kila anachofikiria, kumbe ktk hilo upo sahihi. Ukimuacha mnapotea wote
* cha msingi ktk hili ni kueleweshana kwa utaratibu, tena sehem ilotulia, sio mbele za watu au watoto.
Jua kua, ukiwa umesoma na mwingine hajasoma, uelewa wako unachangiwa na "a long and very complicated process of transformation" iloipitia shuleni, ambayo mwenzako hajaipitia, so tegemea kutofautiana, na wala usione "khaa yani haelewi hata hiki kitu kidogo tuu, au khaa yani hawezi kutumia akili ya kawaida tuu"..!, No, that's wrong, wewe unaweza kutumia hiyo akili b'se umeshapitia shule nyingi na uelewa wako ushakua sharpened.
Ni kama mtu aliyekulia familia bora af anataka kuwashangaa maskini kwanini hawawezi kufanikiwa!

All in all, kumuogopa muumba kutasaidia ktk kuepukana na vishawishi vya nje ya ndoa
Upendo utasaidia ktk kutoyaona makosa madogo madogo kama makuuuubwa sana (mtu ukimpenda hata akosee unaweza kupuuzia tu, utapenda kumsikiliza, utapenda kuwa nae ktk kila hali)
Kuvumiliana kutasaidia ktk hali ngumu za maisha, mitihani ya maisha, magonjwa, kuna zile tabia zisizoweza kubadilika kirahisi.

+++unaweza dhani watu flani hawaonekani kugombana ukafkiri ndoa yao ina amani sana, No!, nao wana yao mazito kabisa ambayo ukisimuliwa utakimbia na kuona bora yako.
Pia, waweza udhiwa na mumeo/mkeo hadi ukafkiria bora ya kumuacha ukaoa/olewa mwingine, No,! Unaweza angukia pua zaidi na kuona kumbe yule ulomfikiria ana nafuu, kumbe ilikua gia ya kukupata tuu, baada ya kumuoa/olewa nae, akawa ndo bora ya yule wa kwanza!

Nawasilisha[emoji120]
[emoji106]
 
Ni kuvumiliana tu, maisha ya kuishi na mtu mzima aliyelelewa huko na wewe kule yataka moyo Sana. Utamaliza dunia nzima tabia ni zile zile.
 
Yaani hawa huwa wanakuwa wazuri sana nyakati za mwanzo za uchumba na ndoa. Baada ya miaka3 na kuendelea ndio sasa utamtambua vizuri. Yaani utanyooshwa tu. Chezea wanawake wewe! Unarudi nyumbani ukifika getini unajiuliza niingie au nirudi nilikotoka?
 
Yaani hawa huwa wanakuwa wazuri sana nyakati za mwanzo za uchumba na ndoa. Baada ya miaka3 na kuendelea ndio sasa utamtambua vizuri. Yaani utanyooshwa tu. Chezea wanawake wewe! Unarudi nyumbani ukifika getini unajiuliza niingie au nirudi nilikotoka?
Pole. Lkn yawezekana ulianza wewe na yeye anamalizia sasa.
 
Maisha yako hayana tofauti sana na mimi Mkuu.
Ukisema ushindane na mwanamke ndani ya nyumba,ni sawasawa na kupigana na ukuta,kuna wanawake wengine tabia zao hazivumiliki wala hazizoeleki.Wanawake kama hao kama ulivyosema,inahitajika akili ya ziada na kujifanya mjinga.
Kitu kibaya ndani ya nyumba kuliko zote ni kushindana na mwanamke,ukishindana na mwanamke ndani ya nyumba,kila kitu kitadorora,majukumu ya kuikarabati nyumba yatapungua kwenu wote wawili,kuzungumza kwa maelewano kwa ajili ya kuijenga nyumba yatakuwa siyo mazuri,kuna hasara nyingi sana kushindana na mwanamke ndani ya nyumba.
Mi mrs wangu ni mlokole kindakindaki ila huwa nakuwa naye makini sana katika maamuzi na kauli zangu.

Kuna wakati huwa najiuliza kuwa huko kanisani wanasali nini. Naishi naye kwa furaha sana maana huwa napotezea mengi ilimradi maisha yasonge.

Kuna wakati najifanya mjinga mpaka wazazi wangu wanashindwa kunielewa wanadhani nimepewa limbwata.

Pamoja na mapungufu aliyonayo mrs, nimejiridhisha huwa hachepuki hivyo hiyo imenifaya nipate nguvu ya kumpotzea hayo mengine.

Kuna wakati siku za mwanzoni mwanzoni mwa ndoa tulikuwa hatujafahamiana vizuri tuliingia kwenye bifu kali lililotikisa ndoa yetu. Namshukuru Mungu tulimalizana wenyewe bila kusuluhishwa na mtu ila i nataka moyo sana.

Kuna wakati najifanya mjinga ili mambo yaende maana migogoro ya ndoa inarudisha sana maendeleo nyuma maana hakuna linalopangika.

Ndoa zinafundisha mengi sana wandugu ila aina ya mwenza umpatae anaweza kukujenga ama kukupoteza kabisa kutokana na kujitambua ama kutojitambua.

Kiujumlla hakuna kanuni maalum ila ni kumwomba Mungu kwa kila siku ianzapo.
 
Back
Top Bottom