Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 413
Sheria inasemaje inapotokea mwanaume ameishi na mwanamke kwa kipindi cha mwaka na wakazaa mtoto? Uhusiano wao hapo awali ulikuwa ni wa kirafiki zaidi kwani watu hawa hawakufunga ndoa ya aina yoyote. Baada ya mwaka huo mmoja uhusiano huo unavunjika na mwanamke anaondoka na kwenda kufungua kesi akidai kupata mgao wa mali iliyopatikana katika kipindi cha mwaka huo mmoja walioishi na mwanaume. Je, sheria inasemaje katika hili?
Kuna uwezekano wa mwanaume kuamua kufunga ndoa na mwanamke kwa mkataba wa kipindi maalumu kama vile miaka 5 au 10 na baadae ndoa hiyo kufikia kikomo baada ya muda uliokubaliwa kwisha?? Naomba wataalamu wa sheria mnipe darasa hapo.