Kuishi na ndugu wa mume

Kuishi na ndugu wa mume

kuna mdogo wangu anamchumba wake ambae process zote za kuoana tayar japo jamaa kaomba hajajipanga kufunga ndoa sasa hv uchumi haujakaa sawa anaomba amchukue kwanza ndoa baadae

bint amepanga kwake mkoa tofauti na jamaa
Sasa jamaa kamuomba akae na mtoto wa Dada
Bint kamaliza form 4 mwaka huu. hataki kurudi kijijin hivyo akae kwa bint siku ya kuolewa ikifika wataenda pamoja kw a jamaa maana jamaa hawez kukaa na ndugu yake kwa sasa anataka kuchukua likizo hivyo akae kwa bidada mpaka akitaka kuolewa ndio atamchukua

Bint anasema kukaa nae sio shida Ila tabia zake ndio shid

Alishawahi kukaa nae anavitabia flan vinakera hana heshima wala uoga anaweza maliza kuoga akachukua nguo yako akavaa bila kuomba yaan anavitabia tu vya ajabu ajabu ukimgombeza kidogo anaanza kulia,,, alishakaa nae mwez 1 alihisi kuumwa sasa hv anataka aje akae mda wote mpaka atakapo pata maisha yake,,,,,

anashindwa amjibuje mchumba wake anaogopa kukataa ataonekana hapend ndugu bado mapema na akikubal anahisi changamoto kubwa bora angekua anakuja kusalimia tu kuliko kuishi nae siku zote
anaomba ushaur afanyeje au amjibu mini jamaa?
Kama kuna mtu kaelewa hii hekaya atakuwa genius
 
Wadada mna mentality mbaya sana khs ndugu wa mume, mbona sie tunakaa na ndg zenu hatuna noma wala nini
Sijui kwanini hii tabia inaibukia huenda kwa sababu na wanawake nao wanatumia tumia vimishahara vyao kununulia nyanya za familia.
 
Akatae, ila ajue akiingia kwenye hiyo ndoa huo ni msalaba wake wa kwanza kudili nao.

Kwa sasa achomoe, huyo dogo akaishi kwao.
 
Hayo ni mapungufu yake tu na nzuri zaidi anaijua vyema tabia ya huyo ndugu wa bwana yake. Yeye akubali kuishi naye tu, Ila matatzo yake yakizidi maji amweleza ndugu yake ili akanywe. Afikiria kama angekuwa mdogo wake yeye na ana hizo tabia au ndugu upande wao angemfukuza.
 
Kweli yani sijaweza kuelewa naona kama vitu vinajirudia rudia mpaka anashindwa kuelewa nani ni nani na kipi kinasemwa kumhusu nani
Ipo hivi (najaribu): Chalii una mchumba. Mdogo wako wa kike alomaliza form 4 unataka akakae kwa huyo mchumba maana dogo hataki kurudi kwao. Mdogo wako ni pasua kichwa na hata adabu hana. Mchumba hayupo tayari kwa hilo. Akwambie vipi uelewe bila kuwa na tafsiri kuwa hapendi ndugu zako?
 
Nakutigo pesa mda c mrefu una akil sana
 
Ipo hivi (najaribu): Chalii una mchumba. Mdogo wako wa kike alomaliza form 4 unataka akakae kwa huyo mchumba maana dogo hataki kurudi kwao. Mdogo wako ni pasua kichwa na hata adabu hana. Mchumba hayupo tayari kwa hilo. Akwambie vipi uelewe bila kuwa na tafsiri kuwa hapendi ndugu zako?
Ahaa kumbe hivyo tu? Mbona kaandika mambo mengi sana kiasi cha tutulevya akili zetu mida hii ya usiku?
 
Huyu shule kidogo ilimpita pembeni...inshort haueleweki
 
dawa ni moha tu amuueleze ukweli kuhusu tabia za huyo ndugu yake,kwani ni vama tatizo kulikabili uso kwa uso,asiogope kusema na akae na huyu ndugu wa mchumba baadae likitokea la kutokea ataambiwa kwanini hukusema,aseme sasa
 
Back
Top Bottom