Kuishi uswahilini yataka uvumilivu

Kuishi uswahilini yataka uvumilivu

Desire Dizaya

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2015
Posts
6,476
Reaction score
11,659
Kama huna uvumilivu na busara utaishia kuzichapa kila siku..
Kuna watu hawajastaarabika kabisa
Hebu ona mfano una mihangaiko yako ya huku na kule unatoka asubuhi unarudi usiku huna hata mda wa kushinda nyumbani.. Siku uko free unaamua uamke asubuhi kufua nguo zako za kutokea ulizovaa mwezi mzima
Umeshazianika zinakaribia kukauka ghafla anatokea jirani na matakataka yake anayawasha.. Moshi unazivaa nguo zako mpaka uishe nguo zote zinanukaa
Halafu ni za ofisini.. Hivi unadeal vipi na hawa watu?
 
Ndiyo maana msanii mmoja alisema uswahilini kuna vituko. Kuzichapa na mambo mengine yasiyo ya kistaarab ndiyo maisha yenyewe ya uswahilini. Unaishi nyumba ya kupanga kama Dar hivi, nyumba ya vyumba sita, haina ceiling board na kila chumba familia moja, choo kimoja na ndio bafu hilohilo, wategemea nini hapa! Ndani joto ukisema utoke nje nako kuna vinyesi nk watoto wamejisaidia. Ndiyo huko tulikoanzia maisha. Kama hauko kwako vumilia kijana, iko siku utatoka
 
Sasa ukitoka hapo nguo zishanuka, nenda chooni ukaanze kuweka jiwe la msingi. Choo kimejaa maji balaa.Ile chubwii, uwe umepitia JKT ili kukwepa maji yanayoruka. Uswazi ni kwetu lakini...
 
Mj siku ya kwanza nlimwagia maji takataka zake.. Kurudi kakuta zimelowa.. Kuwaka tena haziwaki
kama mara 1 unamsamehe tu.. kama kila siku ukifua na yeye anawasha moto.. hapo unamchana liwalo na liwe
 
Hujawahi ishi uswahilini wewe
Uswahilini tunachoma moto takataka????

Sijawahi kuona.

Najua hua tunazifukia au unalitoa furushi kwako unaenda kulitupa nyumba ya pili au ya tatu.
 
Hahaaa
Sasa ukitoka hapo nguo zishanuka, nenda chooni ukaanze kuweka jiwe la msingi. Choo kimejaa maji balaa.Ile chubwii, uwe umepitia JKT ili kukwepa maji yanayoruka. Uswazi ni kwetu lakini...
 
Back
Top Bottom