Kuishiwa kwa damu

Kuishiwa kwa damu

twende-kazi

Member
Joined
Apr 7, 2011
Posts
82
Reaction score
102
Kwanza habari zenu wanajamvi wote Kwa ujumla.Mimi Nina tatizo la kuishiwa damu Kwa baba yangu yaani damu inamuisha tuu Na kila baada ya week Tatu au nne anabidi aongeweze damu. Tulikwenda kila hospitali hapa Dar es salaam Na akafanyiwa kila aina ya vipimo lakini hawakuwa Na uhakika Na kila wakisemacho kuhusu majibu yake . Bone marrow wamemfanyia zaidi ya Mara Tatu lakini hawakutoa majibu yanayo eleweka .

Nikaamua kumpeleka India ambapo alifanyiwa vipimo vyote Kwa Mara nyingine Tena Na hatimaye wakatoa jibu kuwa Ni ugonjwa wa LESHMINIASIS ambao unaambukizwa Na wale sandflies wakikuuma (Leishmaniasis, also spelled leishmaniosis, is a disease caused by protozoan parasites of the genus Leishmania and spread by the bite of certain types of sandflies.[2] The disease can present in three main ways: cutaneous, mucocutaneous, or visceral leishmaniasis.[2] The cutaneous form presents with skin ulcers, while the mucocutaneous form presents with ulcers of the skin, mouth, and nose, and the visceral form starts with skin ulcers and then later presents with fever, low red blood cells, and enlarged spleen and liver.[2][3]

Baada ya hapo mzee akapewa dawa ya kutumia ambayo Sijaipata hata nilipokuwa huko INDIA dawa yenyewe inaitwa MILTEFOSINE (tablet) nimejaribu kuitafuta kule INDIA (Mumbai) bila mafanikio, tukarudi Dar es salaam Na kuendelea kuitafuta, wakati huo damu bado inapungua tuu. Nikaona niwarudie wale Madaktari pale muhimbili wanisaidie kuitafuta hii dawa lakini nilipo fika pale wakaanza kuniambia kuwa mzee haumwi huo ugonjwa Na wao wanaupinga kabisa wakaanza kubishana wenyewe Kwa wenyewe (madaktari bingwa wa damu pale muhimbili majina nayaficha) mpaka sasa hawajakuja Na jibu lolote kuhusu tatizo la mzee wangu zaidi ya wao Kusema wa Nadhani mzee anaumwa hiki Na kile.

Sasa Nawaombeni wanajamvi wenzangu Kama kuna mtu anaweza kunisaidia mimi kupata hii dawa MILTEFOSINE (tab) 50mg brand name Ni mpavido au labda kuna Majina mwingine mnisaidie Na vile vile huu ugonjwa wa leshmaniasis unaambukizwa Na wale Jamii ya mbung'o pia mnisaidie kwa sababu nipo njia panda Kwa sasa , Kama pia kuna mtu anajua matibabu kwa njia nyingine naomba mnisaidie Mfano Kama kuna mtu anajua dawa zozote za kuniponya ugonjwa huu zaidi ya ile niliyo andikiwa Kule India .....Email yangu Ni
nicholasgordon30@yahoo.com
 
Back
Top Bottom