Hivi huu mtindo wa kuita watu kwa kutanguliza neno "mzee" ni umetokana na nini?
Halafu kwa nini ni wanasiasa tu wanaitwa wazee? Utasikia mzee Kikwete, mzee Mbowe, mzee Kinana, mzee Warioba, Mzee Slaa, Mzee Wasira n.k ila huwezi kusikia mzee Bakheresa, Mzee Janabi, Mzee Rostam!
Kwa nini mzee inatumika kwa wanaume tu? Kwa nini hakuna mzee mama Mongela, mzee mama Nyerere, mzee mama Makinda n.k?