Mkuu;
Mara hii umeishasahau ''mafuriko ya Lowassa''!
Hoja sio kujaza watu bali hao watu uliojaza wamekubaliana na ulichokisema na pia wamekifanyia kazi!
Kumbuka kwa wengine mikutano kama hii ni sehemu ya kwenda kupitishia siku baada ya kazi!
Baada ya uchaguzi mnakuja na kelele mkisema wameiba kura!
Ni hoja kubwa sana hii, acha kujidanganya ngosha Ng'wamapalala na kutoa utetezi dhaifu kama huu, eti wanatumia mikutano kama hii kupoteza muda. Really?
Kwa hiyo hata wanaomsubiri Magufuli barabarani (japo mahali pengine tunaambiwa huwa wanalazimishwa tu na maDCs na WEOs kama ilivyofanyika juzi kwenye kuandikisha wapiga kura wa uchaguzi wa serikali za mitaa) kumbe huwa wanakwenda kupoteza muda na kushangaa maVX na askari wenye mitutu ya bunduki???
Kualika watu kwenywe sherehe yako na wakaja kula na kufurahi nawe, ni ishara ya kukubalika kwako na watu wanakuwa tayari kushiriki nawe shughuli yoyote ile.....
Ukiona watu wanakususia au unatumia vitisho na mapolisi kulazimisha watu wahudhurie shughuli yako ya sherehe, msiba, harusi ama mkutano wa siasa kama huu ujue una tatizo au kasoro wewe.......!!
Kama jamaa hawakubaliki, wala watu wasingekuwa na taimu kwenda kwenywe mkutano....
Na kumbuka hapo Zito Kabwe hana hata Msanii mmoja wa kutoa "show" ya bureee....
Na kumbuka kuwa, mshindi katika chaguzi za Tanzania kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi SI YULE MWENYE SERA BORA na ANAYEKUBALIKA NA WAPIGA KURA bali ni yule anayetangazwa na tume ama msimamizi wa uchaguzi, mchezo unakuwa umeishia hapo.....
Rejea agizo la Rais John Pombe Magufuli kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, miji na manispaa wakipewa "OLE" iwapo watamtangaza mgombea asiye CCM kuwa mshindi huku akiwa amewapa fedha, gari la kutembelea na nyumba nzuri ya kuishi....!