Kuitwa Kazini VETA

Joined
Nov 17, 2011
Posts
62
Reaction score
13
Wanajamii, wiki mbili zilizopita niliona thread iliyokuwa inaongelea mada hii. Na wengi kati ya waliochangia walisema bado hawajaita kwa ajili ya kuanza kazi. (Nasikitika sijaiiona na sina uzoefu wa kutosha ku-search kwenye mtandao huu). Binafsi nilihudhuria interview na ilibidi wawasiliane nasi wiki iliyopita. Kwa waliohudhuria interview pale Delloit (trh 17 mwezi uliopita) , je wenzetu mmeshaitwa? Au ndo hizo fununu kuwa serikali haina hela?

Ningefurahi kupata majibu kutoka kwa kundi lililofanyiwa interview na delloit, maana kulikuwa na interview zingine ndogondogo mikoani ambazo hao walishaitwa.

Mchana mwema.
 
Bado mapema.

Asante ulimkafu, unasema bado mapema kutokana na uzoefu wako wa ajira za serikali? au specifically kwa issue hii?. NB: Deloit walisema wangeita baada ya wiki tatu ambazo zimeshavuka. Nashukuru kwa mrejesho!
 
ni kweli wiki tatu zimeshapita na zaidi wadau mlioitwa pale delloite wengine hebu tupeni taarifa tufahamu, kulikoni mpaka sasa, na mimi bw. Mdogo alienda hajapata jibu lolote hadi leo.jm tupe taarifa
 
...Nimekuwa nikifuatilia maana kuna nafasi niliomba, ila kuna jamaa ambaye yupo ndani ya Veta akaniambia kuajiri ni mpaka Januari au February mwakani maana bado hawajapewa fungu toka serikali kuu. Tuwe wavumilivu wakuu... Mungu wetu ni mwema na mwaminifu.
 
Kweli uvumilivu unahitajika namungu ni mwaminifu atajibu kwa wakati wake kwani yeye hachelewi wala hawahi
 

Oh, Umenitoa kwenye wasiwasi mkubwa Sarya! Basi tunahitajika kuomba maana I desperately need that job!
 
Issue kidogo complicated, ilibidi muitwe mapema b'se plan ilkuwa watu waazne kaz by december especially kwenye vyuo vipya, ss inaonekana kuna issue ya financial: ngoja nfuatilie, tutajuzana!!!
 
Issue kidogo complicated, ilibidi muitwe mapema b'se plan ilkuwa watu waazne kaz by december especially kwenye vyuo vipya, ss inaonekana kuna issue ya financial: ngoja nfuatilie, tutajuzana!!!

Asante kwa taarrifa Teacher; tunaomba usisahau kutupa taarifa jamani... tunaendelea kuvuta subira
 
Wapendwa, tunaomba kupata update ya hii kitu jamani!

Mr. Teacher, ulisema hii kitu ilikuwa complicated na kuwa ungetupa mrejesho, vipi hakuna taarifa yoyote mpaka sasa? Tujuzane jamani!
 
Wapendwa, tunaomba kupata update ya hii kitu jamani!

Mr. Teacher, ulisema hii kitu ilikuwa complicated na kuwa ungetupa mrejesho, vipi hakuna taarifa yoyote mpaka sasa? Tujuzane jamani!

We ulishatuma maombi na interview ukafanya basi tulia subiri matokeo huku ukiendelea kumwomba Mungu. Jua kuwa kufanya interview haimaanishi ndio lazima upate hiyo kazi. Je ikitokea umekosa hiyo kazi utapokeaje hiyo taarifa? Uwe tayari kwa lolote kupata au kukosa na yote ni majibu ya Mungu pia.
 
Huyo mungu wa herufi ndogo huwa hasikiiagi labda kama unamaanisha Mungu, huyo ndo najua hua anajibu haraka sana
ni kweli ndugu ulikuwa kwenye mawazo yangu nilijiuliza huyu mbona anaandika kwa herufi ndogo. miungu ndo wanaandikwa kwa herufi ndogo. ila nafikiri kidhamira aliidhamiria Mungu Mwenyezi, na sio miungu. tunawaombea wafanikiwe.
 
Sio siri cjui mm nipo dunia ya ngapi hata usaili wenyewe sijausikia nashangaa ss wana jf mnaongelea kuitwa kazini mmmmh haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…