Kuitwa Mahakamani kutoa ushahidi na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa(TAKUKURU)

Suip

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2010
Posts
1,353
Reaction score
815
Wataalam humu JF Kwa kifupi kuna kesi ya ubadhirifu wa fedha za umma inayomhusu mkuu mmoja Idara ya umma ambayo Mimi nilikuwa member wa bodi yake japo sasa sio mjumbe tena, swali langu ni nani anayetakiwa kunilipia posho ya Safari na Malazi kwani Mara kwanza Takukuru waliniita kunihoji ofisini kwao lakini baada ya mahojiano waliniambia hawana fedha nikajigharimia ila sasa wananiita mahakamani kutoa ushahidi sasa hapa nilipo Sina fedha za kujigharimia.Je sio stahili yao TAKUKURU kunilipa posho ya Safari na Malazi kwani ni mahali pa kwenda kulala na kesho ndio uhudhurie mahakamani.
Naomba kuwasilisha
 
Takukuru fedha wanazo sasa!? Kama fedha za mafuta ni tatizo vituoni mwao, wataweza kukugharamia wewe!? Jaribu, labda utafanikiwa...
 
Wataalam humu JF Kwa kifupi kuna kesi ya ubadhirifu wa fedha za umma inayomhusu mkuu mmoja Idara ya umma ambayo Mimi nilikuwa member wa bodi yake japo sasa sio mjumbe tena, swali langu ni nani anayetakiwa kunilipia posho ya Safari na Malazi kwani Mara kwanza Takukuru waliniita kunihoji ofisini kwao lakini baada ya mahojiano waliniambia hawana fedha nikajigharimia ila sasa wananiita mahakamani kutoa ushahidi sasa hapa nilipo Sina fedha za kujigharimia.Je sio stahili yao TAKUKURU kunilipa posho ya Safari na Malazi kwani ni mahali pa kwenda kulala na kesho ndio uhudhurie mahakamani.
Naomba kuwasilisha

Upo umbali gani mkui??
 
mkuu kama TAKUKURU ndio wanahitaji ushahidi wako na wamekuita wenyewe, basi ni wajibu wao
kukugharamia kwa kipindi chote watachokuwa wana kutumia kama shahidi muhimu.

Wataalam humu JF Kwa kifupi kuna kesi ya ubadhirifu wa fedha za umma inayomhusu mkuu mmoja Idara ya umma ambayo Mimi nilikuwa member wa bodi yake japo sasa sio mjumbe tena, swali langu ni nani anayetakiwa kunilipia posho ya Safari na Malazi kwani Mara kwanza Takukuru waliniita kunihoji ofisini kwao lakini baada ya mahojiano waliniambia hawana fedha nikajigharimia ila sasa wananiita mahakamani kutoa ushahidi sasa hapa nilipo Sina fedha za kujigharimia.Je sio stahili yao TAKUKURU kunilipa posho ya Safari na Malazi kwani ni mahali pa kwenda kulala na kesho ndio uhudhurie mahakamani.
Naomba kuwasilisha
 
Nadhani Sheria ya ushahidi imetanabaisha kuwa shahidi anatakiwa kugharamiwa kufika na kurudishwa toka mahakamani kutoa ushahidi wake.
 
Nawashukuru kwa mchango wenu hivyo nitafuata na kuufanyia kazi ushauri.
 
Kijijini km40

Km 40 ni mbali sana TAKUKURU wanaowajib wa kukugharamia kila kitu
Angalau pangekua karib ungefanya kwa ajili ya umma maana rusha ni janga hapa nchini

ANGALIZO

hutakiwi kutoza pesa kwa ajili ya kutoa ushahidi
 
swala la kulipa shahidi mahakama ndiyo yenye jukum.la kulipa hati ya wito inatolewa na mahakama kutoa ushahid kama hao takukuru watakupa fedha hilo watakuwa wamefanya ubinadam tu lakin mahakama ndiyo inayolipa kwa kesi zote za jinai
 
Kama takukuru hawawezi kumgharamia shahidi afike mahakamani, basi siyo rahisi kuishinda rushwa.
Zaidi sana kwa hali hiyo, kuna uwezekano mkubwa wa kuungana na watoa au wapokea rushwa!
 
Shahidi mahakamani anaitwa na mahakama hivyo ni shahidi wa mahakamani bila kujali ni upande gani u me initiate aitwe. Mahakama inalo fungu maalumu kwa ajili ya kulipa mashahidi hivyo dai gharama mahakamani
 
Back
Top Bottom