Kuitwa msaliti, is a curse, inaondoa heshima na hadhi kisiasa!

Kuitwa msaliti, is a curse, inaondoa heshima na hadhi kisiasa!

Trable

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2023
Posts
1,781
Reaction score
3,288
Najua wengi mtatukana matusi mengi ila mkashindwa kukubaliana na ukweli!

Kokote kule, msaliti huchukiwa na kila mtu, awe mke ama mume akimsaliti mwenzake, huibuka chuki na pengine mgogoro mkubwa ndoa unaanzia hapo na hata kuvunjika kwa ndoa!

Watu wengi hawafikii katika hali ya kufunga ndoa na kuishia kwenye uchumba pekee, ni kwa sababu ya mmoja kumsaliti mwingine!

Na kwa hali hiyo, msaliti mmojawapo akimsaliti mwenzake na ikajulikana hivyo kwa wengine, hata kuolewa na ama kuoa kwake hatapata tena katika maeneo anayofahamika nayo, ni kwa sababu usaliti ni kama laana inayomfuatilia mtu!

Mwanasiasa yeyote hata kama akiwa maarufu kiasi gani akafahamika kuwa ni msaliti kwa nchi yake na kwa wananchi! Iwe kwa kutungiwa uwongo, na uwongo huo ukaenea kwa wananchi wake, mtu huyo hudharaulika na hadhi yake kisiasa hushuka mara!

Tunayo mifano mingi sana hapa nchini, mfano Prof Lipumba aliwasaliti wenzake kwenye chama Chake, tokea hapo, heshima ya Prof Lipumba ikoje sasa, Je kisiasa?

Mwangalieni mh Zitto, naamini wengi mtanibishia na mtaishia kutukana matusi bila kufikiri, Zitto wa 2010 unaweza kumilinganisha na wa sasa? Shida ni nini? Usaliti, kwa sababu ni mzuri pindi uufanyapi na utakupa manufaa kwa muda mfupi lakini lazima ukurudie!

Mapokezi na kiu ya wananchi kwa mh Lissu ingelikuwa haijafamika na wala kutaokuwa na kuenea masikioni mwa watu kwamba yeye ni msaliti, mapokezi yake na hata mikutano anayoifanya na atakayoifanya, itakuwa na ubishani mitandaoni tu lakini uhalisia wake ni mdogo kulikoni ilivyokuwa kabla ya kutwishwa jina la usaliti wa nchi!

Ukiniuliza kwamba, Lissu amesaliti nini katika nchi, stakuwa na jibu, ila ijulikane tu, mtu yeyote akiitwa msaliti, na ikafahamika hivyo, hata kama ni kwa uwongo, tayari ataanza kupoteza umaarufu na heshima yake kisiasa!
 
Magufuli alisema msaliti wa nchi hatakiwi kuishi na baada ya masaa machache nikapigwa risasi ~~~~~ Lisu.

Kumbe anajijua kabisa ni msaliti
 
Mkuu Hawa wanasiasa wengi wanatuchezea akili tu, it's survival for the fittest! Almost wote wapo kwa ajili ya maslahi Yao, wachache sana ndo Wana uchungu na sisi

Ujinga wa wananchi ni kusubiria tupambaniwe, haki haiombwi Mzee, never! Kila sehemu penye haki ujue Kuna watu walishapambana sana na wakaji sacrifice ndo heshima huja

Huwezi kudai haki kwa kuomba, Hawa wanasiasa wanapiga kelele tu hakuna watachoweza kutusaidia, nilibahatika kufika kwa lisu kipindi anakaa tegeta(sijui kama alishahama), to cut the story short the guy is filthy rich

Mababu walisema aliyeshiba hamjui mwenye njaa, THINK!!
 
Umeandika kwa uchungu sana mkuu
 
Back
Top Bottom