The Icebreaker
JF-Expert Member
- Feb 11, 2018
- 22,278
- 65,817
Kwenye hili sakata la kuitia watu neno MWIZI, raia tunaonekana tuna makosa lakini makosa yapo kwa wanaotakiwa kuwajibisha adabu na si wengine ni vyombo vya usalama.Mimi ndugu yangu ilibaki nusu apigwe vibaya mbagala kisa Mama mmoja aligundua kuwa anatoka na Mwanae ambaye mwanafunzi akamkodia wahuni wachache wakamtarget njiani akiwa kabeba Flat screen yake akapigiwa kelele za mwizi dakika chache raia wakamzunguka kipindi kikaanza , ila bahati nzuri alifuatana na kijana mmoja akawa analia huku akipiga kelele wamuache sio mwizi hapo ndio ikawa salama yake japo aliumia kidogo.
Kingine kwa Sheria ya Uislamu kupiga mwizi na kuua ni makosa inatakiwa , inatakiwa kuwe na ushahidi wa wazi na afikishwe kwenye vyombo vya Sheria ikiwa.
Hivi ujasiri mtu anapata wapi wakufika na kushusha kipigoMwizi, Mwizi, Mwizi... Kusikia hii Yowe kwa watanzania wengi ni kibali cha kuanza kumfukuzia mlengwa na kujichukulia sheria kwa kumshushia kumpiga, kumponda mawe na hata kumchoma bila kumpa nafasi ya kujieleza,
Yani ile unaanza kujieleza tayari ushapigwa ngumi ya taya, umerukiwa kichwa, n.k. ukidondoka chini hesabia shughuli itaisha kwa kuondoka kwa kujikokota ukiwa kilema ama sehemu hio kuwa mahali utapofia, ponea yako labda defender ya polisi ipite utaokolewa lakini nao tayari wanakupa kesi ya wizi kwa ushahidi kwamba ulikuwa unapigwa kwa kuitwa mwizi.
Ndicho kilichotokea hata leo kwa Mandojo. Itakuwa kuna mtu alikuwa ana ugomvi nae akamuitia mwizi, labda ni yeye mwenyewe Mandojo aliibiwa lakini mwizi akamuwahi kumwitia mwizi, n.k. anayeitwa Mwizi ndio hupigwa, Hakuna maelezo !!
Binafsi nakumbuka nikiwa chuoni tuliwahi kumpoteza mwenzetu kwa huu ushamba, Alienda kumtembelea girlfriend wake, huko alipofikia waligombana kwa kupishana kauli, alipoanza safari ya kurudi akiwa mtaani ghafla girlfriend wake akaanza kumwita mwizi, kilichofuata wananchi wenye hasira kali bila kumhoji wakaanza kumshushia kipigo mpaka mauti, wananchi walitumika kutekeleza nia ovu ya huyo mwanamke.
MAONI YANGU:
Tujenge utamaduni wa kistarabu tuwe na utu, kabla ya kukurupuka kuchukua maamuzi ya kupiga, kuua, kutia vilema, kuchoma, n.k. kwa kusikia yowe za "Mwizi! Mwizi huyo !", ni vema tutumie akili zaidi.
"msikilizeni huyo mtuhumiwa kisha msikilizeni na anayedai kuibiwa."
Hata kama kweli mtu ni mwizi, kitendo cha kumpiga mpaka kumuua, kumkata mikono, kumpa kilema, kumchoma, n.k. sio ustarabu.
Kama imefika mbali sana kiasi cha kutoa adhabu mtaani. ingependeza iwe ni ya viboko endapo kuna ushahidi tosha mhusika kaiba, baada ya hapo kumpeleka kwenye vyombo vya sheria.
Inasikitisha sanaUkiona hivo ujue jamii hiyo ni masikini na ni wajinga wa kupindukia.Mtu mwenye akili timamu huwezi kushiriki kuua kisa tu umesikia mwizi.
Mi nlikua na mawazo kama yako mkuu lakini mwisho wa siku nikagundua hakuna kitu kinachodhidi thamani ya uhai. Kuna faida nyingi za kumuacha mtu akaishi kuliko kuyachukua maisha yake.Siku ukiibiwa utaona kuita mwizi ni option sahihi pia.
Siku yako ikifika hauwezi kuchomoka regardless ya sababu, sote ni wapita njia
Pointwakati mwingine uswazi kuna wazazi wanakumbatia watoto wao wezi.
aaah hizo zimefeli ndio maana wanapigania sharia yaani jino kwa jino.Huko pwani si mnawaroga na kuwasomea albadir, au mnadhani habari zenu hatuna?
Acha ujinga wewe, tatizo sio kuita mwizi, issue ni kupiga mpaka kuua bila ushahidi wowote zaidi ya kuita mwizi, angalia Kuna siku wewe au mtu wako wa karibu watawaita wezi kwa kukusingizia au bahati mbaya tuu ukaishia kupondwa na mawe mpaka ufe, hii tabia lazima ikomeshwe na iwekwe wazi Hilo ni kosa la jinai, polisi uanze kuelimisha watu na ni marufuku kuchukua Sheria mkononiSiku ukiibiwa utaona kuita mwizi ni option sahihi pia.
Siku yako ikifika hauwezi kuchomoka regardless ya sababu, sote ni wapita njia
Sikubaliani na kitendo cha kuuawa Mandojo, lakini hali ndio hiyo siku yake ilikuwa imefika.Mi nlikua na mawazo kama yako mkuu lakini mwisho wa siku nikagundua hakuna kitu kinachodhidi thamani ya uhai. Kuna faida nyingi za kumuacha mtu akaishi kuliko kuyachukua maisha yake.
Kwa kesi kama ya Mandojo utagundua angepewa adhabu ya viboko au kupelekwa polisi kusingekuwa na majuto kwa walioshiriki kuondoa uhai wa mtu asiye na hatia. He's gone na hakuwa mwizi kisa tu waliomuua walikuwa na mawazo haya "wewe hujawahi kuibiwa.".
Niwe mkweli tu nikisikia fulani kauwawa kwa kusingizia jambo huwa naumia na inaniharibia siku kabisa.
Njoo usome reply za huku mwishoni uone nilikuwa namaanisha nini na ujue mtazamo wangu.Acha ujinga wewe, tatizo sio kuita mwizi, issue ni kupiga mpaka kuua bila ushahidi wowote zaidi ya kuita mwizi, angalia Kuna siku wewe au mtu wako wa karibu watawaita wezi kwa kukusingizia au bahati mbaya tuu ukaishia kupondwa na mawe mpaka ufe, hii tabia lazima ikomeshwe na iwekwe wazi Hilo ni kosa la jinai, polisi uanze kuelimisha watu na ni marufuku kuchukua Sheria mkononi
Hapo mwenye hatia ni huyo aliye msingizia mwenzake wizi ...inatakiwa na yeye auliwe hadharaniMwizi, Mwizi, Mwizi... Kusikia hii Yowe kwa watanzania wengi ni kibali cha kuanza kumfukuzia mlengwa na kujichukulia sheria kwa kumshushia kumpiga, kumponda mawe na hata kumchoma bila kumpa nafasi ya kujieleza,
Yani ile unaanza kujieleza tayari ushapigwa ngumi ya taya, umerukiwa kichwa, n.k. ukidondoka chini hesabia shughuli itaisha kwa kuondoka kwa kujikokota ukiwa kilema ama sehemu hio kuwa mahali utapofia, ponea yako labda defender ya polisi ipite utaokolewa lakini nao tayari wanakupa kesi ya wizi kwa ushahidi kwamba ulikuwa unapigwa kwa kuitwa mwizi.
Ndicho kilichotokea hata leo kwa Mandojo. Itakuwa kuna mtu alikuwa ana ugomvi nae akamuitia mwizi, labda ni yeye mwenyewe Mandojo aliibiwa lakini mwizi akamuwahi kumwitia mwizi, n.k. anayeitwa Mwizi ndio hupigwa, Hakuna maelezo !!
Binafsi nakumbuka nikiwa chuoni tuliwahi kumpoteza mwenzetu kwa huu ushamba, Alienda kumtembelea girlfriend wake, huko alipofikia waligombana kwa kupishana kauli, alipoanza safari ya kurudi akiwa mtaani ghafla girlfriend wake akaanza kumwita mwizi, kilichofuata wananchi wenye hasira kali bila kumhoji wakaanza kumshushia kipigo mpaka mauti, wananchi walitumika kutekeleza nia ovu ya huyo mwanamke.
MAONI YANGU:
Tujenge utamaduni wa kistarabu tuwe na utu, kabla ya kukurupuka kuchukua maamuzi ya kupiga, kuua, kutia vilema, kuchoma, n.k. kwa kusikia yowe za "Mwizi! Mwizi huyo !", ni vema tutumie akili zaidi.
"msikilizeni huyo mtuhumiwa kisha msikilizeni na anayedai kuibiwa."
Hata kama kweli mtu ni mwizi, kitendo cha kumpiga mpaka kumuua, kumkata mikono, kumpa kilema, kumchoma, n.k. sio ustarabu.
Kama imefika mbali sana kiasi cha kutoa adhabu mtaani. ingependeza iwe ni ya viboko endapo kuna ushahidi tosha mhusika kaiba, baada ya hapo kumpeleka kwenye vyombo vya sheria.
Na hivi umaarufu ulishapotea kizazi cha kuanzia 95 hawamfahamu. i hope hakua anajihusisha na mambo hayo. Sijui story yake imekaaje kiuhalisia, alikua anatoka wapi kwenda wapi anafanya nini eneo gani ikawaje!!RIP mandojo, ila ukiitiwa mwizi kuchomoka ni ngumu aisee asilimia 90 lazima ufe, omba yasikukute.
Mwizi, Mwizi, Mwizi... Kusikia hii Yowe kwa watanzania wengi ni kibali cha kuanza kumfukuzia mlengwa na kujichukulia sheria kwa kumshushia kumpiga, kumponda mawe na hata kumchoma bila kumpa nafasi ya kujieleza,
Yani ile unaanza kujieleza tayari ushapigwa ngumi ya taya, umerukiwa kichwa, n.k. ukidondoka chini hesabia shughuli itaisha kwa kuondoka kwa kujikokota ukiwa kilema ama sehemu hio kuwa mahali utapofia, ponea yako labda defender ya polisi ipite utaokolewa lakini nao tayari wanakupa kesi ya wizi kwa ushahidi kwamba ulikuwa unapigwa kwa kuitwa mwizi.
Ndicho kilichotokea hata leo kwa Mandojo. Itakuwa kuna mtu alikuwa ana ugomvi nae akamuitia mwizi, labda ni yeye mwenyewe Mandojo aliibiwa lakini mwizi akamuwahi kumwitia mwizi, n.k. anayeitwa Mwizi ndio hupigwa, Hakuna maelezo !!
Yowe ya "Mwizi" inatumika kama silaha rahisi ya watu wenye nia ovu kuwatumia watu wengine kuumiza, kutia vilema na hata kuua watu wengine wasio na hatia. Hata ikitokea polisi ikawatia nguvuni watu waliojichukulia sheria mikononi, Huyo alieita mwizi anabaki salama.
Visa ni vingi sana, nikiwa chuoni tuliwahi kumpoteza mwenzetu kwa huu ushamba, Alienda kumtembelea girlfriend wake, huko alipofikia waligombana kwa kupishana kauli, alipoanza safari ya kurudi akiwa mtaani ghafla girlfriend wake akaanza kupiga yowe za kumsingizia ni mwizi, kilichofuata wananchi wenye hasira kali bila kumhoji walimshushia kipigo kikali sana hadi mauti, kisa kingine kipo mwisho wa hii post ni fundi aliekuwa anawahi kazini alfajiri ghafla anaitwa mwizi, hapewi nafasi ya kujitetea wala hakuna ushahidi, wakaanza kumpiga.
MAONI YANGU:
Tujenge utamaduni wa kistarabu tuwe na utu, kabla ya kukurupuka kuchukua maamuzi ya kupiga, kuua, kutia vilema, kuchoma, n.k. kwa kusikia yowe za "Mwizi! Mwizi huyo !", ni vema tutumie akili zaidi.
"msikilizeni huyo mtuhumiwa kisha msikilizeni na anayedai kuibiwa."
Hata kama kweli mtu ni mwizi, kitendo cha kumpiga mpaka kumuua, kumkata mikono, kumpa kilema, kumchoma, n.k. sio ustarabu.
Kama imefika mbali sana kiasi cha kutoa adhabu mtaani. ingependeza iwe ni ya viboko endapo kuna ushahidi tosha mhusika kaiba, baada ya hapo kumpeleka kwenye vyombo vya sheria.
Kwa kesi kama ya Mandojo utagundua kwamba kama angesikilizwa pamoja na aliemuitia mwizi, na hata kama wangefika mbali kumpa adhabu ya viboko au / na kumpeleka polisi, ingekuwa ni afadhali zaidi kuliko kilichotokea.
Mwezi uliopita majira ya saa 9 usiku zilisikika kelele kutoka kwa majirani wakisema "mwizi, mwizi"
Japokua nilisikia hizo kelele lakini sikutaka kutoka nje moja kwa moja kwasababu ni risk sometimes na hii nimejifunza baada ya tukio baya lililomtokea ndugu yangu.
Wakati niko ndani nikasikia sauti nje ikitokea kwenye ile nyumba iliyokua ikipiga kelele za kuita mwizi kuwa "aah wana bahati wamekimbia siku nyingine watakuja kufa kijinga"
baadhi ya majirani waliamshwa na ile sauti na ikabidi kuwauliza waliokua wanaita mwizi nini kimetokea. "Kuna wezi walikua dirishani wanataka kuiba na ndio maana tumeita mwizi"
Basi mimi niliposikia hivyo nikaona haina sababu ya mimi kutoka nje kama mwizi kasepa na hakuna alichoiba so ikanibidi niuchape usingizi tu.
Kesho yake tena majira ya saa 10 na robo usiku nyumba ile ile tena nikasikia kelele za kuita mwizi. Round hii nikachomoka na kinondo flani hivi huwa nakiweka nyuma ya mlango nikafungua geti ili niweze kukabiliana na huyo mwizi.
Katika hali isiyo ya kutarajia nikaona yule aliyeitwa mwizi anakuja kwangu na wakati huo mimi nipo getini bado sijafunga hata geti.
Huyo aliyekuwa akiitwa mwizi alikimbia na kuingia getini kwangu huku mimi nikiwa nimeduwaa. Kivipi mwizi akimbilie ndani mwangu wakati humu si sehemu salama kwake yeye wakati akijua kua itawarahisishia wananchi kumpiga kwa uraisi kwa sababu hatakua na sehemu ya kukimbilia.
Ikabidi nimfuate lakini nilishtushwa na sauti yake "Scars wananiua bure mi sio mwizi"
Nikataharuki kwa mshangao mkubwa kwasababu sauti hiyo ilikuwa si ngeni masikioni mwangu. Hapo ndipo nilipomsogelea kwa ukaribu na nikapata kujua kuwa yule ni mshkaji wangu wa kitaani.
Wakati huo alikuwa amelala chini huku damu zikimvuja kama maji, aah nilidata nikajikuta namuuliza maswali ambayo yalikuwa yananitatiza "daah mwanangu imekuaje umekuwa mwizi na mtaani wote wanakujua kuwa wewe ni fundi"?
Jamaa alijibu kwa shida sana maneno yake yalisikika kwa mbali kama mtu anayeweweseka, "Scars nilipigiwa simu kuwa kuna kazi inabidi nikaifanye na ndo maana nimejihimu asubuhi ili kuepukana na foleni maana kazi naenda kufanyia mbali. Lakini nilipofika hapa nashangaa wamenivamia na kunichoma visu kuwa mimi ni mwizi japokuwa niliwaambia kuwa mimi ni kijana wa mtaa huu huu"
Hapo nikaona niwaite vijana makamo yangu tusaidiane kumbeba mshkaji kumpeleka hospitali
Tulivyokua tunamnyanyua pale chini ndipo tulipobaini kuwa jamaa kashambuliwa vibaya sana. Shingoni kulikuwa na kitobo ambacho kilikuwa kinavuja damu ambazo zilimfanya akose nguvu ya kusimama peke yake.
Tukamchukua mpaka dispensary ya mtaani hapa ili aweze kupata matibabu ya huduma ya kwanza lakini wauguzi hawa hawakumhudumia chochote ndugu yetu wakatuambia tumpeleke Amana huku tukifuatilia PF3.
Tukakodi bajaji fasta fasta tukampakia huku akiongozana na kaka yake kuelekea hospitali ya Amana. Huku mimi nikirudi home kusafisha mazingira ya pale maana damu ilitapakaa ndani kiasi cha kufanya paonekane kama ni Vingunguti.
Majira ya saa 4 asubuhi tuliletewa taarifa kua jamaa kashafariki na ukweli halisi ni kwamba jamaa kauliwa kimakosa. Waliyemdhania kuwa ni mwizi alikimbia na walipotoka kumkimbiza wakakutana na huyu mshkaji wetu ambaye alikuwa mpita njia tu asiye na hatia akielekea kazini. Aisee nilihuzunika sana siku hiyo.
Hata kama angekua mwizi kweli Japokuwa wanasema huwezi kuthubutu kumpiga mwizi kama hukuwahi kuibiwa. Lakini hapana sio kwa kiwango cha kufikia kumpiga visu vya shingoni binadamu mwenzako bila huruma.
Halafu bora hata wagemkuta anavidhibiti kuwa ni yeye kafanya, maskini hata yule mwizi halisi aliyekimbia naye hakufanikisha kuiba chochote.
Wapumbavu wachache walikuwa wakisema siku yake ilifika
Source: Tukio lililotokea mwezi uliopita linanithibitishia kuwa "binadamu wote ni sawa ila hatupo sawasawa"