Kuitwa mwizi na wananchi kuanza kushusha kipigo bila kuhoji ni kukosa ustaarabu jamii za Tanzania Bara, Wengi wamesingiziwa na kuuawa / kupata vilema

Me naona ata kitendo cha kumpiga mwizi tu pia sio ustarabu
kwa nin usimpeleke kwenye vyombo vya sheria badala yake ujichukulie sheria mkononi kwa kumumiza binadam mwenzako ama kukatisha uhai wake kabisa?
Kujichukulia sheria mkononi kunatokana na udhaifu wa sheria zetu.

Ni ngumu sana mwizi wa kukurupushwa mtaani kupatikana na hatia isiyotia mashaka.

Ndipo wananchi wanaona kumpeleka kwenye vyombo vya sheria ni kupoteza muda tu ni heri kumalizana naye.

Na hata hivyo wanaomfukuza na kumuua mwizi 90% ni majizi watupu.

Hali hii sijui inatokana na nini, maana hata mzinzi akishika ugoni anaua bila ya kupepesa macho.
 
Tatizo hamuendi mahakamani kutosa ushahidi
 
Kwa akili za wa Tz Usiombe mwizi akakimbizwa akakata kona kwenye kichochoro unachotokea wewe alafu umevaa shati linalofanana na lake hapo inabidi ukimbie zaidi ya huyo mwizi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
2020 In zambia kuna jamaa niliznguana nae.nkampa kichapo ile na escape eneo la tukio akaanza kupiga yowe,"kabwalala kabwalala kabwalala ".ikabidi ni simamame ilikuwa amanaanisha "mwizi mwizi mwizi".

Ghafla raia wakajitokeza pande zote.most of them wananijua,wakauliza "iwe kabwalala Ali kwii" yani mwinzi yuko wapi" jamaa akani point 👉 mimi.

Hata hawakuliza amekuibia nini,wakaanza kumuwakia na kusema huyu mbongo hawezi kuwana tabia hizo mbona tunaishi nae vizuri labda kuna mengine.

Hapo nilipata nguvu ya kuongea sasa nilijiongeza hadi wakataka kumshushia kipigo nikaanza kumtetea.jamanii ishini na watu vizuri hasa ugenini.
 
Hatari sana mkuu,Mimi uliwahi Nikita Mbeya huko,sema Mungu ni mwema jamaa alikosea kusema nimeiba nguo ya mtumba mkononi sikuwa na kitu,yeye ndio alishushiwa kipigo!
Na wewe siku ukisingiziwa wizi ndo utajua umuhimu wa hoja iliyoletwa jukwaani.
Kuna siku mwizi alifukuzwa,akaingia uwa wa nyumba ya ghorofa,akajificha chini ya ngazi,waliofika mwanxo me uwani,wakamkuta aliyetangulia kufukuza mwizi,wakaanza kumpiga,bahati kwenye gjorofa kulikuwsko na mzee wa kihindi,akapiga kelele huku anashuka ngazi,kuwa huyo sio mwizi,akaulizwa meizi yuko wapi akasema hajui,lile genge la wauwaji wakatoka,akabaki yule mzee wa kihindi na wale vijana wawili,mpaka alipoona kuko vizuri,akawaruhusu wende zao,kumbe hata yule aliyejificha ngazini,amesingiziwa ki ugomvi tu,sio mwizi.
 
Ukipigiwa kelele za mwizi na kama sio mwizi na haujaiba basi usikimbie coz hata ukikimbia watakudaka tu na ndo utapigwa ufe... Just relax na waendee waliokuita wew mwizi mkamalizane tena ni kwa ugomvi kabisa.

Raia wakiona watu mnapigana hiyo ndo pona pona yako coz lazima waje waulize kuna nin kinaendelea, so hapo ndo utaanza kujielezea ila ukikimbia kwa kuitwa mwizi asee haufiki mbali na watu wakikudaka hawaulizi.

Hii iliwai kutokea kwa shemeji yangu tena anakwambia alizusha ugomvi haswa na alipiga wale wajinga mpaka watu wakaingilia kati but hakukimbia kwanza bali yeye alisimama na ku deal nao.
 
"Yani ile unaanza kujieleza tayari ushapigwa ngumi ya taya, umerukiwa kichwa, n.k. ukidondoka chini hesabia shughuli itaisha"*

Duh!😳
 
Me naona ata kitendo cha kumpiga mwizi tu pia sio ustarabu
kwa nin usimpeleke kwenye vyombo vya sheria badala yake ujichukulie sheria mkononi kwa kumumiza binadam mwenzako ama kukatisha uhai wake kabisa?
Uko sawa kabisa,ila vipi wezi wanaokuvamia na kuwakata mapanga kisa huna pesa waliyotegemea!!!????
 
Uko sawa kabisa,ila vipi wezi wanaokuvamia na kuwakata mapanga kisa huna pesa waliyotegemea!!!????
Ukivamiwa na wenye mapanga una haki ya kujihami na ww ila sio mtu hajashika hata pini mkononi unaenda kumsabulia na tofali la kichwa hii haija sawa ata kdg
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…