Kujadiliwa kwa hoja za CHADEMA zaidi ya hoja za Bungeni ni Jambo linalotafakarisha

Kujadiliwa kwa hoja za CHADEMA zaidi ya hoja za Bungeni ni Jambo linalotafakarisha

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
Toka CHADEMA ianze ziara zake nchini, Hoja zake imekuwa zikijadikiwa zaidi kuliko za Bunge.

Suala la kataiba Mpya ambalo lilichagizwa na BAVICHA pale Baracuda limepelekea kuzua mijadala mizito kila kona nchi. Limewaibua mpaka Waziri Kabudi kutoka mafichoni, Kabudi toka ameteuliwa kuwa waziri wa katiba hajawahi ongea na vyombo vya habari mpaka hapo juzi alipojitokeza kuzungumzia hoja hii.

Bunge limekosa mvuto hali inayopelekea hoja zake kuwa hazina mashiko kwa jamii, imefikia mahali Mdude CHADEMA anazungumziwa zaidi kuliko hoja ya kodi ya miamala ya simu Ilipitishwa na Bunge.

Ukiwauliza watu wengi sasa hivi Je Bunge linaendelea? Jibu utakalolisikia kwa wengi hawajui chochote. Hii ni hatari bunge lipo kwenye Bunge muhimu sana wananchi walipaswa kufuatlia na kujua mstalabali wa nchi yao.

Ni watake CHADEMA "shikilia hapo hapo usiachie"
 
Utamu wa kubeba mtoto, asikukojolee, akikukojolea tu, hiyo ndiyo itakuwa agenda ya siku nyingi, kila ukimbeba utahisi utakojolewa tena.

Chadema hamna agenda zaidi ya kufanya ukikojozi kwenye kitanda.

Kwa akili yako unataka tuache kuongelea namna ya kuwasaidia ili msikojoe tena?
 
Bunge limekosa mvuto hali inayopelekea hoja zake kuwa hazina mashiko kwa jamii, imefikia mahali Mdude CHADEMA anazungumziwa zaidi kuliko hoja ya kodi ya miamala ya simu Ilipitishwa na Bunge.
Ha ha haa ha, mkuu umenichekesha sana hapo eti Mdude Chadema anazungumziwa zaidi kuliko HOJA ya miamala ya simu. Haa haha, kwamba watu hawana time kinacho endelea Dodoma, very funny
 
Utamu wa kubeba mtoto, asikukojolee, akikukojolea tu, hiyo ndiyo itakuwa agenda ya siku nyingi, kila ukimbeba utahisi utakojolewa tena.

Chadema hamna agenda zaidi ya kufanya ukikojozi kwenye kitanda.

Kwa akili yako unataka tuache kuongelea namna ya kuwasaidia ili msikojoe tena?
Siku hizi hukojoi kitandani?
 
Nina maoni yafuatayo.

Kwanza Kabudi apuuzwe yeye na alichokiongea. Mtu wa jalalani wa kaliba yake si wa kumzingatia hata kidogo.

Pili, bunge halina tofauti na party caucus ya ccm. Kwahiyo watu hawasikilizi kwasabb wanaona kama ni kikao cha CCM.

Tatu, chadema na watu wake ama ajenda zake kujadiliwa ni sawa kwasabb ndiyo chama kinachobeba ajenda za watu. Ndiyo chama kinachowasemea watu. Ndiyo chama kinachopendwa na watu. Na ni chama cha watu.

CCM imejaa wanafiki na wasakatonge.
 
Back
Top Bottom