Hello dear members. Jamani nina babangu anaumwa takriban miezi mitano sasa. Shida ni kwamba maji na hewa yamejaa kwenye mapafu hafu yanamsababisha kukohoa kwa sana na kushindwa kutembea, yaani akitembea anahema kwa shida sana. Tukampeleka hospitali wakamfanyia upasuji kuondoa maji na hewa lakini baada ya wiki mbili maji na hewa yalimjaa tena tukampeleka tena hospitalini ambako alifanyiwa tena surgery kuondoa hayo maji lakini hadi sasa hivi hayajaisha wanasema bado yapo kama 20percent. Jamani hili tatizo linasababishwa na nini na tiba yake nini ? Naombeni ushauri wenu wapendwa.