Kujenda Frems Mkuranga

Gajungi

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2011
Posts
257
Reaction score
83
Wakuu habari za shughuli.

Ninaomba msaada wenu katika hili,

Nina mpango wa kujenga frems kadhaa maeneo ya mkuranga,ningependa kujua makisio ya kujenga frem kwa ajili ya biashara.

Heshima kwenu
 
Unajenga frem ngapi, zenye ukubwa gani? Location unayotegemea kujenga ni pale Mkuranga mjini au unaingia ndani kidogo? Fafanua kwanza mkuu.
 
achana na akili za kimaskini wa kibongo!wengi wana mawazo mgando kama yako.
ifikie wakati tutofautishe residential na commercial areas,nyie ndio msio fuata mipango miji
kama ni kwa ajili ya uwekezaji real estate industry returns unaanza kupata baaga ya miaka 8-10 baada ya ku break even!
nakushauri tu fanya biashara nyingine inayokuingizia kipato kwa haraka ili mtaji wako ukue
 
Unajenga frem ngapi, zenye ukubwa gani? Location unayotegemea kujenga ni pale Mkuranga mjini au unaingia ndani kidogo? Fafanua kwanza mkuu.

Nakushukuru kwa msaada wako mkuu,

Kusema kweli mimi si mtaalamu sana wa haya mambo,ninataka kujenga frems kwa ajili ya biashara ya maduka na saloons,kwa hiyo wenye utaalamu watajua ni za ukubwa gani,namba yake inaweza kufikia 10,na sehemu ipo kabla ya kufika mjini Mkuranga__Vikindu.
 
Vikindu napafahamu, nakushauri kwanza ufanye utafiti wa baadhi ya vitu. 1. Kodi za frem ni bei gani, 2. Ni frem za aina gani zinazopata wateja, maana ukijenga frem za gharma kubwa na kodi yake itabidi iwe kubwa. 3. Vipi kuhusu upatikanaji wa vifaa vya ujenzi, maana gharama za vifaa zikiwa chini itakusaidia kupumguza gharama za ujenzi. Pia ni muhimu kufanya maamuzi ya busara kuusu aina ya uwekezaji unaoufanya, kwa maana kwamba uwekezaji wa frem za biashara inakuchukua muda mrefu kurudisha mtaji ulio uweka lakini ni uwekezaji mzuri/endelevu. Kwa msaada zaidi watafute wataalamu wa masuala ya ujenzi.
 
I doubt if you are certified great thinker,tafuta namna nzuri ya kuwasiliana.
 
Mkuu asante sana kwa ushauri wako,sehemu ninapotaka kujenga ni karibu sana na campus mpya ya SAUT hapo kwa masista wa Vikindu,chuo kitaanza mwezi november mwaka huu. Mimi nafikiri sehemu ambapo kuna chuo soon or later frem zitahitajika au unaonaje mkuu?
 
Kwa hapo mkuu nakuunga mkono, anza kutekeleza mradi, pia tuwasiliane hata mimi naweza kupata frem hapo kama zitakuwa eneo zuri kibiashara.
 
Mkuu nimevutiwa na hilo eneo,kutakuwa na biashara in future hapo.Vipi maeneo yanapatikana bado huko?
 
Mkuu nimevutiwa na hilo eneo,kutakuwa na biashara in future hapo.Vipi maeneo yanapatikana bado huko?

Kuhusu kupatikana kwa maeneo sehemu hiyo sina uhakika maana mimi nipo mbali,lakini nitaulizia kama bado kuna maeneo.
 
Kuhusu kupatikana kwa maeneo sehemu hiyo sina uhakika maana mimi nipo mbali,lakini nitaulizia kama bado kuna maeneo.

Nitashukuru sana mkuu.i will be waiting for your feedback
 
Kwa hapo mkuu nakuunga mkono, anza kutekeleza mradi, pia tuwasiliane hata mimi naweza kupata frem hapo kama zitakuwa eneo zuri kibiashara.

Ok,tuwasiliane,in the near future planner ataenda site,nafikiri nitahitaji mdau wa kurent sehemu kwa ajili ya catering.
 
Samahani mkuu hikichuo kinachoanza November kipo maeneo gani pale vikindu coz vikindu ni kubwa
 
Kuhusu kupatikana kwa maeneo sehemu hiyo sina uhakika maana mimi nipo mbali,lakini nitaulizia kama bado kuna maeneo.

Samahani mkuu hikichuo kinachoanza November kipo maeneo gani pale vikindu coz vikindu ni kubwa
 
Vikindu ni mbele ya Mwandege sio mbali sana jenga inalipa ingekua kipalang'anda au jaribu nsingekushauri kujenga labda ujenge Kimanzichana pale Center.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…