Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unajenga frem ngapi, zenye ukubwa gani? Location unayotegemea kujenga ni pale Mkuranga mjini au unaingia ndani kidogo? Fafanua kwanza mkuu.
Nakushukuru kwa msaada wako mkuu,
Kusema kweli mimi si mtaalamu sana wa haya mambo,ninataka kujenga frems kwa ajili ya biashara ya maduka na saloons,kwa hiyo wenye utaalamu watajua ni za ukubwa gani,namba yake inaweza kufikia 10,na sehemu ipo kabla ya kufika mjini Mkuranga__Vikindu.
achana na akili za kimaskini wa kibongo!wengi wana mawazo mgando kama yako.
ifikie wakati tutofautishe residential na commercial areas,nyie ndio msio fuata mipango miji
kama ni kwa ajili ya uwekezaji real estate industry returns unaanza kupata baaga ya miaka 8-10 baada ya ku break even!
nakushauri tu fanya biashara nyingine inayokuingizia kipato kwa haraka ili mtaji wako ukue
Vikindu napafahamu, nakushauri kwanza ufanye utafiti wa baadhi ya vitu. 1. Kodi za frem ni bei gani, 2. Ni frem za aina gani zinazopata wateja, maana ukijenga frem za gharma kubwa na kodi yake itabidi iwe kubwa. 3. Vipi kuhusu upatikanaji wa vifaa vya ujenzi, maana gharama za vifaa zikiwa chini itakusaidia kupumguza gharama za ujenzi. Pia ni muhimu kufanya maamuzi ya busara kuusu aina ya uwekezaji unaoufanya, kwa maana kwamba uwekezaji wa frem za biashara inakuchukua muda mrefu kurudisha mtaji ulio uweka lakini ni uwekezaji mzuri/endelevu. Kwa msaada zaidi watafute wataalamu wa masuala ya ujenzi.
Mkuu asante sana kwa ushauri wako,sehemu ninapotaka kujenga ni karibu sana na campus mpya ya SAUT hapo kwa masista wa Vikindu,chuo kitaanza mwezi november mwaka huu. Mimi nafikiri sehemu ambapo kuna chuo soon or later frem zitahitajika au unaonaje mkuu?

Kuhusu kupatikana kwa maeneo sehemu hiyo sina uhakika maana mimi nipo mbali,lakini nitaulizia kama bado kuna maeneo.
Kwa hapo mkuu nakuunga mkono, anza kutekeleza mradi, pia tuwasiliane hata mimi naweza kupata frem hapo kama zitakuwa eneo zuri kibiashara.
Kuhusu kupatikana kwa maeneo sehemu hiyo sina uhakika maana mimi nipo mbali,lakini nitaulizia kama bado kuna maeneo.