Kujenga magodown ndio ubunifu pekee wa wakurugenzi wengi wa taasisi za Serikali?

Kujenga magodown ndio ubunifu pekee wa wakurugenzi wengi wa taasisi za Serikali?

tutafikatu

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2011
Posts
3,435
Reaction score
4,788
Wakurugenzi wengi wa mashirika na taasisi za serikali hawana ubunifu. Kila siku ardhi zinazomilikiwa na taasisi zao wanazigeuza kuwa magodown, tena sijui hata kama mapato yake yanaingia serikalini.

Hili ni tatizo la mifumo yetu kushindwa kufanya vetting sahihi. Mtu hata banda lake la kuku hajawahi kumiliki, lakini anapewa ukurugenzi wa taasisi inayohitaji ubunifu mkubwa. Wengine wanateuliwa kwa sifa ya kutokuwa wabadhirifu, wakati huko walikotoka hawakuwa hata na bajeti ya kusimamia hadi waitwe waadirifu.

Halafu kuna wengine wanakaa kwenye nafasi hizo zaidi ya miaka kumi, utadhani hakuna Watanzania wengine wenye uwezo wa kuongoza taasisi hizo.

Hivi kweli tunakosa watu wenye ubunifu wa kuendeleza taasisi zetu zaidi ya kujenga magodown kwenye kila kiwanja kilichobaki?
 
Back
Top Bottom