ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,040
- 7,303
Usijenge gorofa kama huna pesa ambayo ni determine utaacha gofu mjini hapo
Hahahahahaha umenivunja mbavu ujue...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Usijenge gorofa kama huna pesa ambayo ni determine utaacha gofu mjini hapo
Kujenga kama unatumia fundi mchundo/engineer wa mtaani. Lazima ugawe kwa phase lakini kaka umegawa kwa bei rahisi sana. Msingi umegawanyika, kwanza kuna kuchimba msingi hapa sio chini ya 800,000 kisha baada ya hapo kuna kumwaga zege la blinding hapa napo weka kama 500,000 kisha kuna kusuka nondo za beam za chini na base vitako hapa weka kama 300,000. Kisha kuna kupandisha kuta za msingi weka kama 800,000. Kisha kuna kutoa udongo ulioza, kujaza mchanga na kupanga mawe weka 1,000,000. Baada ya hapo kuna kusuka nondo za beam kabla ya slab hapo weka 500,000. Kisha unamwaga jamvi weka 1,250,000.
Sijakuchanganulia slab ya juu ambayo imegawanyika sehemu kuu tatu. kwanza kuna foarmwork ambayo sio chini ya 1.25 million, kuna kusuka chuma ambapo ni kama 1.25 million, kuna fundi umeme weka 700,000 kumwaga slab weka 1.5 million.
Ushauri tuu kumbuka muoshwa huoshwa. Usijenge gorofa kama huna pesa ambayo ni determine utaacha gofu mjini hapo
cjengi kwa kutegemea hayo nimeeleza tu wapi pa kupata urahis wa vifaa vya ujenzi kwa wasio na uwezo na sio lazma ghorofa hata za kawaida.na usishangae watu wanajenga sana kwa bei nafuu na mie ninayeongea najua nn namaanisha.
Ninakushauri fuata taratibu na kanuni zote za ujenzi,
Bodi ya ukandarasi ipo makini sana kwa wale waendao kinyume!
Tumia kampuni ya ukandarasi iliyosajiliwa kihalali na bodi ya ukandarasi nchini,
Gharama za mkandarasi zisikufanye ukavunja sheria za ujenzi kwa hasara utakayopata nikubwa zaidi ikiwa utabainika kuvunja sheria husika!
Maeneo uliyoyataja Kigamboni nk ni sehemu inayomulikwa kwa ukaribu zaidi na CRB,
Usiogope gharama mkuu, ninakushauri kwa uzoefu wangu kama mkandarasi hapa nchini!
Wasiliana nami mkuu ikiwa utapendezwa kujenga kwakuzingatia sheria tajwa!
Nimekuandikia pm, umeiona?
Mkuu Bei zako utafikiri tenda ya Halmashauri!
Hizi bei ni kubwa mno. Au umeipa tenda kampuni ya mhindi ikujengee?
Gorofa sio lele mama, ukiona mtu kalijenga basi lione hivyo hivyo. Ufundi msingi wa gorofa sio chini ya Million 5 muulize aliyeujenga.
Ninakushauri fuata taratibu na kanuni zote za ujenzi,
Bodi ya ukandarasi ipo makini sana kwa wale waendao kinyume!
Tumia kampuni ya ukandarasi iliyosajiliwa kihalali na bodi ya ukandarasi nchini,
Gharama za mkandarasi zisikufanye ukavunja sheria za ujenzi kwa hasara utakayopata nikubwa zaidi ikiwa utabainika kuvunja sheria husika!
Maeneo uliyoyataja Kigamboni nk ni sehemu inayomulikwa kwa ukaribu zaidi na CRB,
Usiogope gharama mkuu, ninakushauri kwa uzoefu wangu kama mkandarasi hapa nchini!
Wasiliana nami mkuu ikiwa utapendezwa kujenga kwakuzingatia sheria tajwa!
Kujenga kama unatumia fundi mchundo/engineer wa mtaani. Lazima ugawe kwa phase lakini kaka umegawa kwa bei rahisi sana. Msingi umegawanyika, kwanza kuna kuchimba msingi hapa sio chini ya 800,000 kisha baada ya hapo kuna kumwaga zege la blinding hapa napo weka kama 500,000 kisha kuna kusuka nondo za beam za chini na base vitako hapa weka kama 300,000. Kisha kuna kupandisha kuta za msingi weka kama 800,000. Kisha kuna kutoa udongo ulioza, kujaza mchanga na kupanga mawe weka 1,000,000. Baada ya hapo kuna kusuka nondo za beam kabla ya slab hapo weka 500,000. Kisha unamwaga jamvi weka 1,250,000.
Sijakuchanganulia slab ya juu ambayo imegawanyika sehemu kuu tatu. kwanza kuna foarmwork ambayo sio chini ya 1.25 million, kuna kusuka chuma ambapo ni kama 1.25 million, kuna fundi umeme weka 700,000 kumwaga slab weka 1.5 million.
nmekujibu mkuu
pale kutakuwa na makampun 17 yatayofanya kazi ni mradi wa nssf phase 3,mkabala na nyumba za NHC.kuna ujenzi wa magorofa means ghorofa 2na kuendelea. mi npo kwenye moja ya kampun zitazojenga na kipindi kilichopita tulijenga kwa hiyo ni mzoefu wa zaga.mfano wa bei za vitu
cement mfuko 10,000 zaga zikiwa nyingi hadi 5000 kwa mfuko.
-nondo tunanunua
mm :12 sh.10,000 kwa
mm: 16 sh. 15,000-20,000
mm: 10 had 8 sh.8000
ndoo za rangi weather guard ya 150,000 dukani tunanunua 50,000 zikizidi hadi 30,000
ndoo za rangi nyeupe au za kawaida 15,000 hadi 20,000.
bati za kisasa maelewano hata 3000 kwa moja unachukua kutegemea mafundi wamefulia vp.
marine plywood hata mi nimeuza sana sh.15,000 moja
mbao 4by 2 sh.3000,
mbao 3 by 2 sh.2500
mbao 2by 2 sh.1500
milunda sh 500
malumalu,grill jamani.nani na nani wa kuwapata ntawajulisha naogopa kurusha no. za watu humu usije ukawa unaeuliza ni bosi wangu kibarua kitaota nyasi ila kwa atayetaka sisemi uongo cku mtu tembelea ufanye utafiti kuna muda zaga zinakosa watu mafundi wanatafuta pesa za misokoto tuu.kaka zangu dada zangu kwa mshahara wangu ningestaafu cna nyumba ila nimejenga watu wakiiona nyumba yangu hawanisomi.ila siri ni zaga na bonge la project linakuja kwa maskin ni furaha kwetu.ntajua watu gani wa zaga watakuwepo safari hii ntarusha no. zao shughuli itapoanza kwan tunasubir muda wowote kazi zianze.kwa wenye muda unaweza fanya upelelez mwenyewe utapata wauza saga wataokuletea hadi ulipo ila cjui wao huko mtaan wanafanya bei gani kama una muda unatafuta vijana wananunua na kukuletea kwa bei nlizoandika au chini ya hizo.nadhan nimeeleweka ndugu zangu.
Wakubwa zangu:
Kuna rafiki yangu anataka kujenga nyumba ya ghorofa moja. Ukubwa wa nyumba ni wastani wa mita za mraba 350 (chini chumba kimoja, jiko, sebule, store, public toilet, study room na dinnig. Juu (Vyumba vitatu) na kila chumba ni self contained.
Materials mwenye nyumba atanunua mwenyewe kulingana na alivyopewa na engineer wake. Gharama za material mpaka kupaua inakadiriwa kuwa 80m
Swali: Engineer na mafundi wake walipwe kiasi gani kwa kuanzia setting ya nyumba, kujenga mpaka kupaua (kuweka vigae) basi. Kiwanja kiko maeneo ya mbweni ni eneo tambarare sana. Kwa mwenye uzoefu naomba asaidie makadirio inaweza kuwa kiasi gani (kwa gharama za mafundi fundi peke yake).
Shukrani sana
Wabongo kweli ni noma, mtu ana justify wizi wake kwa kigezo cha umaskini! Ninyi ndo mnasababisha maghorofa yanaanguka na kuua watu kutokana na wizi mnaoufanya, sababu sehemu iliyopangwa ijengwe kwa mifuko mitano ya cement mnaiba hapo mitatu na hivyo inajengwa kwa mifuko miwili tu.
Pole yako, unaingizwa mtegoni na huyu mzee wa system nawe unaingia kichwakichwa kufunguka jinsi mnavyoiba kupitia makampuni ya ujenzi. Kama huwajui wazee wa sekta nyeti wamejazana humu we subiri muziki wake.