Kujenga nyumba ni usumbufu sana

Kwanini fundi asi shauri zinazofaa na kusema sababu?

Wezi wezi tu, fundi anaye jithamini hawezi kufanya kazi mbovu

Mwizi mwizi tu.. na kutokutumia akili za kujiwekea level ya juu kikazi

Kataeni kazi kwani lazima?
Unapopata fundi wa level hizo, Basi jua na wewe wa level hizo. Hata jengo lako litakuwa la level hizo
 
Na kuna nyumba zinauzwa hizo,,,, ukiwasha sabufa YAKO volume 7 tu! Nyumba yote inaanguka...

Cha msingi ni malezi tu.. mijitu mingi ya bongo inaamini maisha bora yanapatikana katika kuiba na ubadhilifu pale Inapopata nafasi mahala..... Na ndivyo ilivyo lelewa hivyo... Ndoyo maana umasikini hauishi...
 
Uko sawa kujenga lazima uwe na muda wa kusimamia na wala usimwamini mtu. Ukimwamini mtu inabidi ukubali sub standard job. Kuna mtu alijengewa gorofa bila nguzo za zege, kwenye nguzo walilaza matofali tu. Yeye yuko Sweden na wakapiga lipu faster na kunyoosha nguzo za tofali.
 
Unapopata fundi wa level hizo, Basi jua na wewe wa level hizo. Hata jengo lako litakuwa la level hizo
Mkuu hata kama wewe si wa hivyo fundi hata umlipe vipi yaani hawathamini kazi zao. Akikufanyia vizuri basi jua anatega kazi ingine hapo ameiona. Hawaoni kuuza mfuko wa cement kwa sh 5000. Kuna jamaa alitaka kunifanyia tuagize mirunda ya ziada akawa kimbelembele. Mirunda tulitakiwa tuongeze 350, akaagiza ikaja ikamwagwa ovyo ovyo na akawa na haraka ya kuitumia nikamwuliza iko mingapi? akasema 350 basi nikasema usiitumie kwanza nikaweka mtu akahesabu ikawa 270. Na huyo mtu graduate kabisa engineer na mimi nipo. Nilipomwuliza vipi yaani akajibu poa tu niliona nijaribu kwanza hii tutaleta ile 80 kama hii haitapungua. Watu si wakweli. Ukiagiza cement huwa zinarudishwa dukani kwa bei ya hasara hata 5000 ili uambiwe iongezwe tena ikiisha.
 
Hii ni kweli kabisa. Kuna majilani wawili mmoja ni mdau haswa kila kitu alimwachia fundi. Huyu mmoja ni kawaida tu ila huyu jilani kawaida alikua anashawishiwa na fundi w mdau kuuziwa material ya uizi kutoka kwa site ya boss wake. Nyumba mbili zilijengwa na material ya yule mshua fundi alikua anauza chochote kile kwa jilani mpk aibu. Kuja kushtuka yule boss nyumba imefika 98% kwa jilani. Mafundi n wezi haswa hata ukimtapia alicho taka.
 
BOT, TRA na Bandari ndio wanaongoza kwa wizi japo wanalipwa vyema kuliko wengi
 
Wewe ni mwizi tu. Maandishi yako yanaonesha umeibia watu wengi sana.
 
Yes......pamoja na wizi wanaofanya ,wengi wao hakuna cha maana walichonacho.
 
Tatizo ni muda. Wengi wanataka sifa kuwa jamaa kajenga nyumba chap tu imesimama.
Jenga nyumba yako taratibu, huko ndiyo mji wako na heshima ya familia yako.
Ukijenga taratibu kama miaka mnne(4) minimum huibiwi, na utaisimamia vizuri.
 
Watanzania kwenye uaminifu ni 0

Ndio maana watanzania wengi na waafrika kwa ujumla wakiwa Ughaibuni, Huwekewa vigezo na masharti mengi kuthibitisha Uaminifu wao.

Wabongo wana asili ya wizi, Utapeli.
 
Tabia ya mafundi ni sawa na tabia ya sehemu kubwa ya jamii yetu.

Ndio maana kuanzia wakubwa serikalini na kwenye siasa tunaona rushwa, ubabaishaji na kutaka utajiri wa kutouhenyea vimetawala.

Ndio maana nasi mitaani tunamsifia mtoto wa jirani anayenunua gari na kujenga katika miaka miwili tu ya ajira, na tunamponda mwajiriwa anayesota kimaisha kwa kukosa fursa za wizi/ rushwa kazini, au kwa kuwa mwaminifu.

Kwa hiyo ni mporomoko wa maadili wa jamii yetu nzima.
 
Mkuu mi nilishaacha kuchukua mafundi wa mjini, Huwa nawatoa kwetu mkoani ni waaminifu balaa. Unaweza usikanyage site kusimamia hata wiki. Yaani hata msumari ukibaki utakuta we sema neno nikuletee hao utanishukuru baadae.
 
Enzi hizo naanza kujenga,

Nyumba yangu ya kwanza nilikazia mwenyewe fundi alitoroka,nyumba yangu ya pili nilipigana na mmoja licha ya kuwa alinizidi nguvu ila sikumlipa.
Mimi kuna fundi mmoja mwaka 2014 , tukiwa site nilitaka nimgonge na gari. Alivuruga kazi akanitia hasara kubwa sana. Alinijibu majibu mabaya sana. Namshukuru Mungu aliniepusha na lile tukio, lingenilitea shida sana. Siku hizi najizuia kabisa na hasira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…