Kujenga nyumba ni usumbufu sana

Yes......pamoja na wizi wanaofanya ,wengi wao hakuna cha maana walichonacho.
Wewe linganisha tu nchi za watu waaminifu KWa asilimia kubwa... Ni nchi tajiri.. na watu wake wanamaisha bora... Kuna jamaa flani alikuwa japani anafundisha shule hizi za chekea na primary.. anasema mara kibao sana watoto wanasahau vitu madarasani nje.. sehemu za kucheza lakini unaweza kuta vitu vipo pale pale hakuna mtoto wala mtu mzima anaye gusa hadi walio poteza wanavikuta pale... Maana wanajua sio vyao.. na haijalishi vikae mwezi, wiki au mwaka...

Mimi nakumbuka nishawahi ibiwa yeboyebo zangu mpirani kipindi nipo primary, yeboyebo ndo zinaingia kipindi hiko bongo, namaliza mechi (cha ndimu) kutafuta yebo sizioni... Wiki inakata nakaona kajamaa kamevaa.. nakauliza yebo umetoa wapi hizo.. kana babaika.. nikakavua... SAsa Hapo fikiria mtoto mdogo yupo primary anafanya hivyo... Na mzazi anamwona mwanae anavaa viatu ambavyo hajamnunulia hamuulizi tena anamsifia mjanja.....

Tanzania,, mapinduzi ya malezi muhimu kufanyika
 
Naona fundi unajaribu kujitetea , ukwel ni kwamba wengi wenu ni waongo na sio waaminifu hasa mkishalipwa pesa yote hua mnatokomea na kuacha kazi ,
Siku zote kabla ya kuanza ujenzi lazima mkubaliane kati ya fundi na boss , Sasa kama ukiona hii kazi maslahi ni madogo Kwa nn ukubali kufanya wakati unatambua haikulipi .
Mafundi wa bongo badilikeni
 
Hii ni hatari sana tena sana.
 
Kama anaona haina maslahi si aache eboo
 
Wajenge juma pilinukiwepo.
 
Mafundi wengi wa mtaani Wana hali ngumu kimaisha. Anakubali kufanya kazi hata ambayo Haina maslahi.
Lakini kumbuka numbers haziongopi.
Mwishowasiku hela inakata kazi bado mbichi.

Epuka Sana cheap labour

Hao ni matapeli tu kama hawajui kazi wanayofanya inakuwaje n.k.

Waambie wajifunze kazi.. wapoge kazi nzuri.. wapate kipato na kujifunza kupanda sio utapeli na kuharibika watu kazi na kuchezea pesa zao huku bado wanaiba.

Njaa haimaliziki kwa utapeli Bali kwa ukweli, bidii na kuji value....
 

Unajenga mkoa gani nikusaidie kusimamia now ni fundi simu ila kwa uzoefu niliopitia kwenye vibarua vya kujenga kipindi najitafuta naweza kusimamia
 
Mimi Mafundi wangu wa ujenzi wa nyumba wako Smart sana kwenye kazi. Kwa kweli nawashukuru sana.
 
Hapa umenena mkuu
Kuna boss alinipaga kazi material kila kitu nimechukua dukani kwa mkataba kuwa kazi ikiisha tu skh hyhy narudshiwa pesa nipeleke dukan na kuwalipa watu wangu aisee kazi nmepga sku4 ila hela pesa nmekuja kupewa baada ya week kupta tena hapo tuesumbuana sana.....nkajisemea tu ww ngja unipe kazi ingne akinipa hela ya kununua material na mm namzngusha mpka maji aite mma maana wanapnda kutuzngua wao tukizngua ss tunaonekana waswahili
 
Tatizo linaanzia kwenye bei. Ila kazi zakuuziana inabidi usimamie haswa. Za day yaani kutwa ikifika jioni unakagua kisha unalipa.
 
Nimeona wengine wanalaumu
Mafundi wengine wanalaumu wenye nyumba

Iko hv kaz ambayo unataka kuifanya iwe kujenga nyumba au wiring umeme au mambo ya mabomba ya maji.. na hata fundi wa gari lako cha kwanza kabla hujampa fundi kazi mfanyie usaili wa kiufundi .../

Sababu mafundi wetu wengi wa mtaan kaz zao wamejifunza kupitia mikonon mwa mtu awe alikaa Garage au alikuwa kibarua kwenye ujenz baadae anajiita fundi.. hawana uelewa mpana wa kiutaalam.. amekariri kama alivyokuwa anakaririshwa shida sie wenye mali we una focus kwenye gharama unamuacha fundi akufanyie upembuz ya kinifu bila kujiridhisha kuwa kama ana uwezo huo...

Anaweza akawa anajua kulaza tofal au kufungua Engine au kuunga wire wa umeme ila
Asijue kwa nn wire size flan utumike kwenye kifaa hiki ama
Kile au kwa nn kuna msingi wanyumba unaweka zege chini au unaweka mchanga tu.. au kama Ni gari hajua kifaa flan kina matumiz gan ya ziada

UNAMFANYIAJE USAILI FUNDI...

Kwanza bila kujali fani yako kama
Unajenga anza kufanya reserach nyumba bora ina sifa zipi.. dunja kijiji jipe mda kaa mtandaonj je nondo size ipi inatumika wapi.. je chombo kipi cha umeme kinaungwa na wire
Upi.. kama ni gari umeona lina tatizo la missfire ingia google angalia sababu mbali mbali..

Ukimuita Fundi mfanyie usaili kwa maana akikwambia msingi wa nyumba haina haja ya zege laza tofali muulize sababu ukiona anakupa sababu za kupiga ramli achana nae.. maana alipaswa kukupa sababu za kiutaalam au ukimuuliza nondo zipi zinafaa kwa mkanda wa juu Au wa chini au nguzo akawambia ww tu chagua zote zinafaa.. wakat unajenga ghorofa

au bomba zipi zinafaa akakuchagulia Kisa ni bomba za bei rahis au kifaa cha umeme kisa bei ndogo achana nae maana anatakiwa akwambie kiufundi kwan nini tutumie material A na sio material B swala la gharama libak kwako..

Unampelekea fundi gar ina miss au haina nguvu anakwambia plug mbovu au pump mbovu unamwambia kwa nn imetokea anakwambia ndo mambo ya magar au gar ishachoka.. alitakiwa akambie pumo au plug inafanyaje kaz na kwa nn imeshindwa na jinsi ya kuepuka Isijirudie

Mafundi wa kibongo watumie kama kitendea kazi wachache anaweza akakupa sababu ya kiufundi kwa nn tusifanye A tufanye B.. sasa fundi amekulia garage au kawa kibarua kwenye ujenzi.. hajua kwa nn nondo zinasukwa hv ama vile au bomba clasa A na bomba class c zinatumika wapi na wapi.. ww ndo unataka awe mtaalam wako wa kukujengea nyumna bora utabaki kumlaumu tu..

Mafundi wa mtaan unatakiwa ww ndo uwe mkandaras wao watendaji tu hata kama
Sio fan yako fanya reseach..

Na haya makampun ya kujenga wana wataalm ila njaa inawasumbua wanakosa
Weledi.. mtu anakupa Mchanganuo wa kitaalam na material bora ile ukimpa kaz anatumia vifaa duni mbao ataweka
Sio Alizokwambia ratio ya cement ataweka tofaut ilimrad apate faida zaid
 
Kutegemea upate fundi ujenzi smart ni sawa na kutafuta bikra wodi ya wazazi!.
Halafu usifanye ujenzi ukawa serious sana utajipa tu stess , we jenga kwa nafasi na kwa ku enjoy, uone how fun it is kushuhudia fundi anaficha mfuko wa cement kwenye rundo la mchanga
 
Tusiwalaumu mafundi tu, hii ni tabia ya watanzania kwa ujumla wetu, huko serikalini ni wizi na ufisadi tu, popote watu wakipata nafasi wanaiba tu.

Muhimu ni, kuwa na ABC za ujenzi, simamia kazi yako mwanzo mwisho, hakikisha unafatilia materials mwenyewe...hii ya kumwambia fundi waambie jamaa walete mchanga fuso moja, waambie washushe tofali 1000 ndio utaanza kuchapwa hapo hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…