Kipala
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 3,763
- 700
Wikipedia ya Kiswahili imeanzisha makala za karibu kila kata ya Tanzania. Makala hizi mara nyingi ni mafupifupi tu lakini kila msomaji ni huru kuongeza habari. Kwa sasa kata zote za mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Kigoma, Lindi, Mara, Mwanza, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Pwani na Tanga zina makala tayari. Zinazobaki zitafuata.
Wote mnakaribishwa kuongeza habari za mahali mnapotoka au mnapoishi.
Kupitia kurasa za mikoa unafika kurasa za wilaya, na kwenye ukurasa wa kila wilaya kuna sanduku la kata zote.
Mifano ni makala ya kata ya Utengule Usongwe katika Wilaya ya Mbeya Vijijini au Kariakoo zilizopanushwa tayari.
Elimu inajenga taifa na wikipedia hii ni chombo cha kisasa kabisa! Karibuni